Pages

Ads 468x60px

Sunday, November 8, 2015

BALOZI MULAMULA AWASINDIKIZA MRAIS WA DRC NA MSUMBJIA


Rais wa Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo, Mhe. Joseph Kabila (wa kwanza kushoto) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula wakitizama Kikundi cha Ngoma kilichokuwa kikitoa Burudani kwenye Uwanja wa Ndege, Rais Kabila alikuja nchini kuhudhuria Sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli iliyofanyika hapo jana katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Rais Kabila (katikati) akielekea kwenye ndege, kulia ni Balozi Mulamula na kushoto ni Balozi wa Kongo nchini Mhe. Khalifani Mpango
Mhe. Rais Kabila akipita kwenye gwaride la heshima lililoandaliwa na Jeshi la wananchi Tanzania.
Katibu Mkuu Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) akiagana na Rais Joseph Kabila tayari kwa kuanza safari ya kuelekea nchini kwake.

0 comments:

Post a Comment

 
Blogger Templates