Pages

Ads 468x60px

Tuesday, November 10, 2015

Siku moja baada ya Dk. Magufuli kwenda Muhimbili Hosp.. nini kimefata kwenye zile mashine?



Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili sambamba na kumsimamisha kazi kaimu Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo Dk. Hussein Kidantu na kumteua Prof. Lawrence Mseru kushika nafasi hiyo.
Kati ya maagizo Rais aliyoacha ni pamoja na mashine za CT Scan pamoja na MRI kuhakikisha zinatengenezwa ndani ya wiki mbili.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma Aminiel Eligaisha amesema baada ya kukutana na kamati tendaji ya hospitali hiyo leo na Kaimu Mkurugenzi aliyeteuliwa Prof.Lawrence Mseru ametoa maelezo na kuhakikisha watafanyia kazi maagizo yaliyotolewa na Rais ndani ya muda waliopewa.
“Tayari suala la CT Scan na MRI limeanza kufanyiwa kazi na ameanza kuzungumza na wataalamu kutoka kampuni ya Philips ya Uholanzi ili waweze kuanza kutengeneza mashine hizi, wameanza mazungumzo leo, kuanzia kesho tutaanza kuona mabadiliko yakifanyika, tutahakikisha suala hili linafanyiwa kazi kwa muda uliopangwa ili wananchi waweze kupata huduma” Eligaesha
Wagonjwa wanaotumia mashine za MRI kwa siku ni wagonjwa 10 hadi 15 na kila mgonjwa hutumia zaidi ya dakika 40 kutumiwa na kipimo cha CT Scan wagonjwa wenye uhitaji ni kati ya 20 hadi 25..“Wagonjwa wamekuwa wakipata taabu sana baada ya mashine hizi kuharibika na imewabidi kwenda hospitali binafsi ili kuweza kupata vipimo ambavyo huku ni gharama zaidi ya hapa” Eligaisha.
Amesema kwa sasa wanafanya juu chini kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma hiyo.
Pia amesema Serikali ndiyo ilisaini mkataba wa kutengeneza mashine hizo na ndio sababu wameweza kulipa fedha kwa ajili ya matengenezo hayo.

VITENDO VYA UDHALILISHAJI NA UBAKAJI WATOTOTO WILAYA YA TEMEKE VYAONGEZEKA



 Mkuu wa Dawati la Jinsia katika Kituo cha Polisi Mkoa wa Kipolisi Chang'ombe, Thecla Kitajo.
 Mkuu wa Dawati la Jinsia katika Kituo cha Polisi Mkoa wa Kipolisi Chang'ombe, Thecla Kitajo (kulia), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo mchana, ambao wanatembelea vituo vya polisi na masoko ya Manispaa za Ilala na Temeke kujionea jinsi vitendo hivyo vilivyo pungua baada ya Shirika la Equality for Growth (EfG) kutoa mafunzo ya kupinga ukatili huo katika maeneo hayo. Kushoto ni Ofisa wa Polisi wa Dawati la Jinsia wa Kituo hicho, Meshack Mpwage.
 Ofisa wa Polisi wa Dawati la Jinsia wa Kituo hicho, Meshack Mpwage, akizungumza katika mkutano huo.
 Ofisa wa Jeshi la Polisi wa Kituo cha Chang'ombe, Digna Ngatena (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Mwanasheria wa Shirika la EfG, Grace Mate)
Maofisa wa Jeshi la Polisi wa Dawati la Jinsia wa Kituo cha Polisi Chang'ombe. Kutoka kushoto ni Albentina Aloyce, Nuni Munisy na Rose Lukanga.

Dotto Mwaibale

WAKATI vitendo vya ubakaji na udhalilishaji kwa watu wakubwa vikipungua matukio ya vitendo hivyo kwa watoto wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam vimekuwa vikiongezeka kila siku.

Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Dawati la Jinsia wa Kituo cha Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke Chang'ombe Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Thecla Kitajo wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, ambao wanafanya ziara katika masoko ya Manispaa ya Ilala na Temeke na vituo vya polisi kujua vitendo vya ukatili wa kijinsia ulivyopungua katika maeneo hayo baada ya Shirika la Equality for Growth (EfG), kutoa mafunzo ya kupinga ukati huo.

"Vitendo vya ukatili wa kijinsia na ubakaji kwa watu wakubwa umepungua kwa kiasi fulani lakini kwa upande wa watoto bado tunachangamoto kubwa kwani kila siku tunapokea kesi ambapo kwa mwezi tunapokea matukio zaizi ya 25 na zaidi" alisema Kitajo.

VYOMBO HABARI VIMECHANGIA KUFANYA UCHAGUZI KUWA WAZI NA HAKI NA HURU –NEC


Mkuu wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Giveness Aswile, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuvishukuru vyombo vya habari kwa kuripoti vizuri katika kipindi chote cha uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani.  Mkuu wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Giveness Aswile, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuvishukuru vyombo vya habari kwa kuripoti vizuri katika kipindi chote cha uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Emmanuel Kavishe.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii. 
 TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)imesema kuwa waandishi wamechangia kufanya uchaguzi kuwa haki na uhuru kutokana na kutoa taarifa zao bila kuegemea upande. 

 Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya sheria wa NEC, Emmanuel Kawishe amesema kuwa mwenendo wa uchaguzi tume ilifanya kuwa wazi kwa kuhakikisha wananchi wanapata habari kupitia vyombo habari.

 Amesema kuwa NEC haina uwezo wa kufikia watu milioni 26 kutokana na kuwepo kwa vyombo vya habari kwani vimekuwa ni daraja la kufanya wananchi wafikiwe na habari kwa wakati.

 Kawishe aliongeza kuwa katika kipindi chote cha uchaguzi amekuwa akishiri katika vyombo habari katika kutoa taarifa kwani bila kufanya hivyo zoezi la upigaji kura lisingekuwa rahisi kama wananchi wasingepata elimu ya mpiga kura.

 ’’Upigaji wa kura umeisha napita kwa kujidai na watu wengi wananikaribisha katika kushiriki hata kunywa kahawa nisingefanya hivyo kama vyombo vya habari vingeongea vibaya kuhusu mimi juu ya elimu niliyokuwa nikitoa katika vyombo hivyo.’’amesema Kawishe.

 Nae Mkuu wa Idara ya Habari NEC, Giveness Aswile amesema katika uchaguzi ujao watajipanga waandishi waweze kufika sehemu zote ili wananchi wajue kazi za tume.

 Amesema Tume imekuwa wazi na kufanya waandishi wajitume katika kutoa taarifa ambazo zimefanya uchaguzi kuwa wa wazi na huru zaidi kwa kupata habari katika kila hatua ambayo tume ilikuwa ikifanya.

SERIKALI IMEOMBWA KUINGILIA KATI SAKATA LA FAMILIA YA JUMA ISANGU, ARUMERU

 Mkazi wa eneo la Duluti wilayani Arumeru mkoani Arusha, Juma Isangu akiwa na mkewe Janet Tinai pamoja na mwanao, Issa Juma (katikati) wakiangalia nyaraka mbalimbali nje ya nyumba yao mara baada ya kufukuzwa na kisha kuvunjiwa nyumba yao wilayani humo na kampuni ya Majembe Auction Mart kwa amri ya mahakama.
Mkazi wa eneo la Duluti wilayani Arumeru mkoani Arusha, Janet Tinai akilalamika mbele ya waandishi wa habari akiwa na baadhi ya vyombo vyake  mara baada ya kuhamishwa kwa amri ya mahakama na kampuni ya Majembe Auction Mart.
 Mkazi wa eneo la Duluti wilayani Arumeru mkoani Arusha, Juma Isangu akiwa na mkewe, Janet Tinai wakitafakari nje ya nyumba yao mara baada ya kuhamishwa na kisha kuvunjiwa nyumba yao na kampuni ya Majembe Auction Mart kwa amri ya mahakama.
(Picha na moses mashalla).

Mahmoud Ahmad.
SERIKALI imeombwa kuingilia kati sakata la familia ya Juma Isangu mkazi wa eneo la Duluti wilayani Arumeru mkoani Arusha kuondolewa na kisha kuvunjiwa nyumba waliyokuwa wakiishi kwa amri ya mahakama kwa madai haki haikutendeka.

Familia hiyo iliondolewa juzi majira ya saa 6:30 mchana na kampuni ya udalali wa mahakama ya Majembe Auction Mart Ltd  tawi la Arusha kwa madai kwamba waliagizwa na msimamizi wa mirathi wa nyumba hiyo aitwaye,Janeth Fosbrooke kuwaondoa  kwa kuwa hawastahili kuwepo ndani yake.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari waliofika katika eneo hilo, Isangu akiwa na mkewe, Janet Tinai pamoja na mtoto wao wa kiume, Issa Juma alisema alisema kwamba kwa sasa hawaelewi ni wapi wataishi kwa kuwa kitendo cha kuondolewa katika nyumba hiyo na kisha kutupiwa virago hakikufuata sheria.

Alisema kwamba wameondolewa kinyemela ndani ya nyumba waliyokuwa wakiishi bila taarifa ingawa  hapo awali waliwahi kushinda kesi ya mgogoro wa nyumba hiyo nambari 33 ya mwaka 2011 iliyofunguliwa katika mahakama ya ardhi.

Akielezea tukio hilo Tinai alisema kwamba mnamo juzi majira ya saa 6;30 mchana watu wapatao sita ambao walijitambulisha kwamba ni madalali  wa mahakama kutoka kampuni ya Majembe Auction Mart walifika katika nyumba wanayoishi wakiambatana na askari wa jeshi la polisi na kuwataka kutoka nje ya nyumba hiyo.

Tinai,alisema kwamba wakiwa wanajiuliza ndipo watu hao waliingia ndani na kisha kuanza kutoa baadhi ya mali mbalimbali na kisha kuzipeleka ndani ya lori mojawapo lililokuwa limeegeshwa nje ya nyumba hiyo na kuacha baadhi ya vitu nje ya  eneo la nyumba hiyo.

Alisema kwamba na mara walipohoji walijibiwa ya kwamba hawakutakiwa kuendelea kuishi ndani ya nyumba hiyo kwa kuwa kuna  amri kutoka mahakama kuu inayowataka kuondoka mara moja ndani ya nyumba hiyo .

Hatahivyo, kwa nyakati tofaiti wanafamilia hao walisema kwamba nyumba hiyo ni halali kwa kuwa walipewa na marehemu Henry Fosbrooke ambaye alikuwa mmiliki halali wa eneo hilo  tangu mwaka  1980 ambaye aliacha wosia waliuwasilisha mbele ya mahakama kuu kanda ya Arusha kama moja ya vielelezo na kisha kukubaliwa.

Hatahivyo,Mwenyekiti wa kitongoji cha Duluti,Elias Kaaya akihojiwa na waandishi wa habari katika eneo la tukio alisema kwamba hivi karibuni baadhi ya watu ambao walijitambulisha kwamba ni madalali wa mahakama kutoka  kampuni ya Majembe Auction Mart walifika ofisini kwao na kuwapa taarifa kuwa wataendesha zoezi la kumtoa mpangaji aitwaye,Isangu kwenye kitongoji chake.

Huku akionyesha barua ya mnamo Novemba 11 mwaka huu yenye KUMB No,REF.NO.MAM/ARJHF/10/2015  mwenyekiti huyo alidai kwamba watu hao waliomba uwepo wa usimamizi kutoka ofisi yake kumtoa mkazi huyo na kudai waliwasilisha pia taarifa kwake na jeshi la polisi wilayani Arumeru.

“Majembe Auction Mart Ltd madalali ya baraza la ardhi na nyumba (court blockers) ukiwa msimamizi wa amani kwenye kata yako ya Akheri tunakuomba uwepo katika zoezi la kumhamisha/kumtoa mpangaji ndugu Juma Isangu aliyekuwa amepangishwa na marehemu Henry Albert Fosbrooke ambapo kwa sasa msimamizi wa mirathi aliyeteuliwa m/s Janeth Fosbrooke ndiye ametuteua kutekeleza zoezi hili la kumtoa mpangaji kwenye nyumba”ilisema sehemu ya barua hiyo

Hatahivyo, msimamizi wa mirathi wa nyumba hiyo, Fosbrooke hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo lakini msimamizi wa  kampuni ya Majembe Auction Mart Ltd tawi la Arusha, Suleiman Mdoe alisema ya kwamba wao walifuata taratibu zote kabla ya kuwahamisha wakazi hao ikiwa ni pamoja na kubandika notisi ya siku 44 kabla ya zoezi kufanyika.

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATANGAZA MFUMUKO WA BEI WA MWEZI



 Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu akizungumza na waandishi wa habari  leo Jijini Dar es Salaam Kuhusu Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2015 ambao umepanda hadi kufikia asilimia 6.3 kutoka asilimia 6.1 kwa mwezi Septemba, 2015.
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu akizungumza na waandishi wa habari  leo Jijini Dar es Salaam Kuhusu Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2015 ambao umepanda hadi kufikia asilimia 6.3 kutoka asilimia 6.1 kwa mwezi Septemba, 2015. Kulia kwake ni Mtakwimu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Muhdin Mtindo. (PICHA NA VERONICA KAZIMOTO)


Na Veronica Kazimoto
09/11/2015
Dar es Salaam.

MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2015 umeongezeka hadi kufikia asilimia 6.3 kutoka asilimia 6.1 mwezi Septemba mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo amesema kuongezeka kwa Mfumuko wa Bei kumesababishwa na kupanda kwa bei za bidhaa na huduma zingine za kijamii ikiwemo chakula na nishati.

“Kupanda kwa Mfumuko wa Bei wa mwezi Oktoba, 2015 kumechangiwa na ongezeko la bei za vyakula kama vile Mchele ambao umeongezeka bei kwa asilimia 0.8, unga wa muhogo umeongezeka hadi asilimia 0.7, nyama kwa asilimia 0.8, samaki kwa asilimia 5.5, ndizi za kupika asilimia 0.7 na choroko kwa asilimia 0.9”, amesema Kwesigabo.

Bidhaa zisizokuwa za vyakula kama vile vitambaa kwa ajili ya nguo za kike zimepanda kwa asilimia 1.6, viatu vya kiume asilimia 1.1, mkaa asilimia 1.4 na gharama za kupata ushauri kwa daktari pia zimepanda hadi kufikia asilimia 1.4.

Kwa upande Mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.1 ambao ni ongezeko sawa na mwezi Septemba, 2015. Fahirisi za bei pia zimeongezeka kutoka 159.04 hadi kufikia 159.17 kwa mwezi Oktoba, 2015.

“Fahirisi za bei za vyakula vya nyumbani na migahawani iliongezeka kidogo hadi kufikia asilimia 10.0 kutoka asilimia 9.4 kwa mwezi Septemba, 2015 ambapo bidhaa zisizokuwa za vyakula zimepungua kidogo kutoka asilimia 1.9 hadi asilimia 1.7 kwa mwezi Oktoba, 2015,” amefafanua Kwesigabo.

Kwesigabo amesema kuwa Mfumuko wa Bei ambao haujumuishi vyakula na nishati kwa mwezi Oktoba, 2015 umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 2.1 kutoka asilimia 2.2 kwa mwezi Septemba, 2015.

Viongozi wateule wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakutana na Watumishi wote

 Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Aloyce Msigwa (kushoto) akifungua kikao kilichowakutanisha watumishi  wa Ofisi ya Rais-Utumishi, na Taasisi zake katika hafla fupi ya kuwapokea Katibu Mkuu mteule Bw. HAB Mkwizu (wa pili kutoka kushoto) na Naibu Katibu Mkuu mteule Bw. Tixon Nzunda (wa pili kutoka kulia).
 Naibu Katibu Mkuu Bw. Tixon Nzunda (aliyesimama) akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi katika hafla fupi, iliyowakutanisha watumishi wote, wa kwanza kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Bw. HAB Mkwizu.
 Mkurugenzi  wa Idara ya Utawala katika Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Nyakimura M. Muhoji akizungumza kwa niaba ya watumishi wa Ofisi ya Rais-utumishi wakati wa hafla fupi ya kuwapokea viongozi walioteuliwa kuongoza Utumishi.
 Katibu Mkuu  wa Ofisi ya Rais- Utumishi Bw. HAB Mkwizu akizungumza na na watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi katika hafla iliyowakutanisha watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.
 Viongozi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, na Menejimenti katika picha ya pamoja.
Viongozi wa Ofisi ya Rais-Utumishi pamoja na watumishi wa Idara ya Ukuzaji Maadili katika picha ya pamoja, Naibu Katibu Mkuu-Utumishi Bw. Nzunda aliwahi kuwa Afisa katika Idara ya Ukuzaji Maadili.

KAMPUNI YA STAR MEDIA TANZANIA LIMITED YASHINDA TUZO YA UBORA YA WQC


 Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na tuzo ya utoaji huduma bora waliyoipokea nchini Ufaransa mwishoni mwa mwezi Oktoba kutoka kwa kampuni ya Business Initiative Directions (BID). Pamoja naye kulia ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes, Bw. Lanfang Liao.
 Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto), akisisitiza jambo katika mkutano huo na wanahabari.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes, Bw. Lanfang Liao akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na tuzo ya utoaji huduma bora waliyoipokea nchini Ufaransa mwishoni mwa mwezi Oktoba kutoka kwa kampuni ya Business Initiative Directions (BID).
 
 
Kampuni ya Business Initiative Directions (BID) ya nchini Ufaransa imeitunuku kampuni ya StarTimes kutoka nchini tanzania tuzo ya World Quality Commitment (WQC) kwa utoaji huduma bora kwa wateja wake.
 
Sherehe za tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya 29 ziliyofanyika jijini Paris ambapo makampuni mbalimbali yalishinda yalishiriki.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kuonyesha tuzo hiyo Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao amesema kuwa hiyo ni habari njema si tu kwa kampuni bali kwa taifa kwa ujumla kwa utoaji wa huduma bora kwa wateja wake.
 
“Tuzo hii imetolewa jijini Paris, Ufaransa mwishoni mwa mwezi Oktoba ambapo kampuni ya Business Initiative Directions (BID) ndio waandaaji wakuu wa tuzo hizi ambazo zimefanyika mara ya 29 kwa mwaka huu.” Alisema Bw. Liao

RAIS MAGUFULI AMJULIA HALI DKT. HELLEN KIJO BISIMBA, AFANYA ZIARA YA GHAFLA MUHIMBILI



 Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliolazwa kwenye hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya Novemba 9, 2015




Rais Dkt.John Pombe Magufuli akimjulia hali Mkurugenzi wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) Dkt.Helen Kijo Bisimba aliyelazwa katika hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es Salaam leo Novemba 9, 2015. Dkt. Bisimba aliujeruhiwa katika ajali gari jijini Dar es Salaam, Novemba 8 2015. Rais pia alifanya ziara ya kushtukiza kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili, MNH, ili kujionea yeye mwenyewe jinsi wafanyakazi wanavyotekeleza majukumu yao katika kuhudumia Watanzania


Rais Dkt.john Pombe Magufuli akizungumza na kuwapa moyo wauguzi katika hospitali ya taifa Muhimbili wakati alipofanya ziara ya ghafa kujionea hali halisi.
 Rais Dkt.John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili wakati alipofanya ziara ya kushtukiza hospitalini hap oleo na kuwafariji wagonjwa.

 Rais akiagana na wauguzi na wafanyakazi wa hospitali ya taifa Muhimbili


Rais akipungia mkono, wagonjwa na wananchi wakati alipotembelea hospitali ya taifa Muhimbili
 
Blogger Templates