Pages

Ads 468x60px

Tuesday, December 15, 2015

BANK YA MKOMBOZI YAFUNGUA TAWI JIPYA MJINI BUKOBA.


Mhashamu Baba Askofu Desiderius Rwoma wa Jimbo Katoliki Bukoba leo wakati wa Ufunguzi wa Tawi Jipya la Benki ya Mkombozi, Ndiye aliyelifungua Rasmi.
Mheshimiwa Mama Edwina Lupembe, Mkurugenzi wa “Mkombozi Commercial Bank"  akiteta jambo kwa furaha na Mhashamu Baba Askofu Desiderius Rwoma wa Jimbo Katoliki Bukoba leo wakati wa Ufunguzi wa Tawi Jipya la Benki ya Mkombozi.
Taswira nje ya Jengo hilo la Benki hiyo!

Maeneo tofauti ya Benki hiyo kwa ndani iliyofunguliwa rasmi leo hii

Pongezi kwa Mama Mama Edwina Lupembe, Mkurugenzi wa “Mkombozi Commercial Bank" kwa Kusogezea Wakaazi wa Mji wa Bukoba na Vitongoji Vyake Bank hiyo.
Mbunge wa Bukoba Mjini(Chadema) Bw. Wilfred Lwakatare akisalimiana na Mama Mama Edwina Lupembe, Mkurugenzi wa “Mkombozi Commercial Bank" leo Mjini Bukoba.
Bw. Wilfred Lwakatare Mbunge wa Bukoba Mjini(Chadema) akitoa Neno wakati wa Afra hiyo ya Ufunguzi wa Tawi Jipya la Mkombozi Benki.Picha za Pamoja


MVUA ILIONYESHA LEO JIJINI DAR


 Mvua zilizonyesha asubuhi ya leo zimesabisha baadhi ya barabara kufunikiwa na maji na kusabisha adha ya usafiri  leo jijini Dar es Salaam.

CHAMA CHA SANAA CHA TINGATINGA CHATILIANA SAINI MKATABA WA MIAKA MITANO WA KUFANYA KAZI NA KAMPUNI YA BRICOLEUR HOLDINGS YA NCHINI JAPAN

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan, Bi. Yu Shiran (katikati) akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu kushirikiana kufanya kazi za sanaa na Kikundi cha Sanaa cha Tingatinga, leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). Kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Sanaa (Tingatinga), Bwana Zachi Chimwanda na kushoto ni Mkurugenzi pia wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan, Bwana Shoji Tsuchiya.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bwana Godfrey Mngereza (kushoto) akifafanua jambo wakati wa utiaji saini wa Mkataba wa makubaliano kati ya Kikundi cha Sanaa cha Tingatinga na Kampuni ya Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan. Katikati ni Wakurugenzi wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan Bwana Shoji Tsuchiya pamoja na Bi. Yu Shiran.

Na Tupokigwe Marco na Mwanahamisi Matasi

Chama cha Sanaa cha uchoraji picha maarufu kama Tinga Tinga kimetiliana saini Mkataba wa Makubaliano wa miaka mitano wa kufanya kazi kwa pamoja na Kampuni ya  Bricoleur Holdings Co. Ltd ya nchini Japan utakaokiwezesha chama hicho kunufaika kwa kuuza kazi zake Kimataifa.

Akiongea leo wakati wa utiaji saini wa Mkataba huo, Mwenyekiti wa Chama cha Sanaa cha Tinga Tinga, Bwana Zachi Chimwanda ameeleza kuwa, utiaji saini wa Mkataba huo utakua chachu ya maendeleo katika kuwakomboa wasanii wachoraji katika kipato chao na kuboresha hali zao za kimaisha kwakuwa kazi zao sasa zitakuwa zikiuzwa ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Wasanii la Taifa (BASATA), Bwana Godfrey Mngereza alieleza kuwa Mkataba waliosaini kati ya Tinga Tinga na watu wa Bricoleur Holdings Co. Ltd utaimarisha kazi za Wasanii katika fani ya uchoraji ikiwemo kuongeza vipato vyao.

''Sanaa ni kazi lakini pia ni biashara, imefika wakati kwa wasanii kufaidika na jasho lao, kampuni hii watakua wakitafuta masoko kule Japan ili kazi hizi za wachoraji toka Tanzania ziweze kununuliwa hali ambayo itawaongezea kipato'', alisema Mngereza.

Aliongeza kuwa Mkataba uliosainiwa kati ya pande zote mbili umepitia taratibu zote za kiserikali na Taasisi zinazohusika na mambo ya sanaa na maslahi ya msanii na msanii yule aliyehusika katika kuchora picha fulani atanufaika na mkataba huo.

''Kwa msanii atakehusika binafsi na uchoraji picha mkataba utamwezesha kujua atanufaika vipi na kwa muda gani'', aliongeza Mngereza.Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Bricoleur Holdings Co. Ltd, Bi. Yu Shiran ameeleza kuwa mpango huo wa Mkataba kati yao na Tingatinga una lengo la kukitangaza Chama hicho cha wachoraji wa Tanzania Kimataifa.

‘’Kwa kutumia taarifa za kidijiti za Tingatinga tutaweza kushirikiana na watengenezaji mbalimbali wa bidhaa, na ili kulithibitisha hili, sisi na Tingatinga tumekuwa katika mjadala wa takriban mwaka mzima sasa’’, alisema Bi. Shiran.

Tinga Tinga Arts Group lilianzishwa nchini Tanzanja na Edward Saidi Tingatinga ambaye alifariki mwaka 1972 ambapo kwa sasa kundi hilo lipo maeneo ya Oysterbay jijini Dar es Salaam kikijihusisha na sanaa ya uchoraji.

TAFFA YAIBUA MAPYA YA UTOROSHAJI WA KONTENA

Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha (Taffa), Stephen Ngatunga (kulia), akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na njia zinazotumika kuiba mapato ya serikali bandarini na katika Idara ya Forodha, Jijini Dar es Salaam jana. kushoto ni maofisa waandamizi wa chama hicho. Picha na Mpigapicha Wetu

Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha (Taffa), Stephen Ngatunga (kushoto), akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na njia zinazotumika kuiba mapato ya serikali bandarini na katika Idara ya Forodha, Jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Ofisa Mwandamizi wa chama hicho, Ernest Kallaghe.


Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
CHAMA cha Mawakala wa Forodha nchini (TAFFA) kimesema kuwa wizi wa kontena bandari ya Dar es Salaam na kusababisha serikali kukosa mapato ni tatizo la muda mrefu ambalo ni limekuwa likisababishwa na watumishi wa bandari.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Rais wa TAFFA, Steven Ngatunga amesema tatizo lilojitokeza ya uondoshaji wa kontena 329 katika bandari Kavu ya Azam ilitokana na baadhi ya watumishi wa baadhi ya benki na Bandari kuingilia taarifa katika mfumo na kusababisha serikali kukosa mapato. 
Ngatunga amesema kuwa tatizo la serikali kukosa mapato katika bandari ya Dar es Salaam walishagundua lakini serikali ilishindwa kuchukua hatua mpaka serikali ya awamu ya tano kugundua hilo na hatua zimechukuliwa kwa wale waliohusika.
Amesema TAFFA itatoa ushirikiano kwa kile ambacho wanakiona katika bandari ya Dar es Salaam juu ya watu wanaosababisha serikali kukosa mapato kwa maslahi yao binafsi.
Aidha amesema kuwa kuna kampuni zilionekana kuwa zipo kwa ajili ya kukwepa kodi ya serikali ambazo chama kiliona na kupeleka malalamiko ambayo mwisho wa siku kukawepo urasimu wa kukutana viongozi ambao wanaweza kushughilikia hilo.
Amesema baadhi ya mawakala walilipia kontena lakini wanaambiwa malipo hayakufanyika huku wakiwa na kumbukumbu za malipo na kusababisha kutilia shaka juu ya uadilifu wa watumishi wa benki pamoja na bandari.
TAFFA imesema haiko tayari kwenda na mawakala ambao wanaharibu taaluma hiyo na kusababishia serikali kukosa mapato ambayo ndio ya kufanyia maendeleo nchini.
Amesema kuwa kuna kampuni 73 zimefungwa wakati hawahusiki katika katika uondoshaji wa kontena katika bandari na bandari kavu kutokana na kampuni hizo kuwa kulipia kontena zinazodaiwa kukwepa kodi.

MAWAKILI ZINGATIENI MAADILI YA TAALUMA YA SHERIA - JAJI MKUU



Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande akizungumza na Mawakili 104 walioapishwa leo jijini Dar es salaam. Mhe. Chande amewataka Mawakili hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia weledi na maadili ya taaluma yao.

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande (katikati) akiwa na Majaji na Watendaji wa Mahakama wakati wa zoezi la kuwaapisha Mawakili wapya 104 katika viwanja vya Karimjee leo jijini Dar es salaam.
Juu na Chini - Mawakili wakiwa wamesimama mbele ya Jaji Mkuu kabla ya kuapishwa.

Mawakili walioapishwa wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu Mhe. Othman Chande na Watendaji wa Mahakama ya Tanzania.


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande akiongoza maandamano ya Majaji na Watendaji wa Mahakama wakati wa hafla ya 53 ya kuwapokea na kuwaapisha Mawakili wapya 104 iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee leo jijini Dar es salaam.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju (kulia) akiwasili katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo wakati wa hafla ya 53 ya kuwapokea na kuwaapisha Mawakili wapya 104.


                                           (Na. Aron Msigwa - Dar es salaam).


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande amewataka Mawakili kote nchini kufanya kazi zao kwa kuzingatia weledi na maadili ya taaluma ya Sheria na kwamba wasisite kuwaeleza ukweli wateja wao wanaopeleka mashauri Mahakamani ili kuepuka kupoteza muda na gharama katika masuala yanayoweza kupatiwa ufumbuzi nje ya Mahakama.


Akizungumza na Mawakili wapya 104 waliohitimu Shule ya Sheria  kwa mwaka 2015 wakati wa hafla ya 53 ya kuwapokea na kuwaapisha iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee leo jijini Dar es salaam amesema kuwa msingi mkubwa wa kazi yao umejengwa katika uzingatiaji wa maadili ya taaluma ya sheria.


Amewataka Mawakili hao kubadilika kifikra kwa kuwa Mawakili Bora ili kujenga imani na uaminifu kwa jamii wanayoihudumia na kuongeza kuwa sasa wameingia kwenye utaratibu wa kutambuliwa rasmi na Mahakama ya Tanzania kwa kuwezeshwa kufanya shughuli za uwakili kwenye mahakama ya Tanzania maeneo mbalimbali nchini.


Naomba mtambue kuwa kila Wakili ni Ofisa wa Mahakama hivyo mnao wajibu na jukumu la kusoma, kufuatilia mashauri mbalimbali ili kuwa na uhakika wa kesi mnazosimamia kuliko kuzitegemea Mahakama


Aidha, ameeleza kuwa yapo mambo ambayo yamekua yakifanywa na baadhi ya Mawakili wasio waaminifu yanayochafua sura ya Taaluma ya Sheria ikiwemo kutumia nyaraka za kughushi, kuvunja Kanuni na Maadili ya Taaluma huku baadhi yao wakijikuta wakiingia katika mgogoro na Mamlaka zinazosimamia kitaaluma taaluma hiyo.

Nawataka mzingatie sheria, kanuni na Maadili ya Uwakili, hata hivyo tuna chombo kinachosimamia maadili yenu, wapo takribani 176 waliokiuka maadili na hawa wanashughulikiwa kwa mujibu wa Sheria ili kulinda maadili na utendaji wa taluma yenu Amesisitiza Mhe. Othman.

Amewataka  watimize wajibu wao kwanza kwa wananchi watakaouhudumia pamoja na Mahakama ya Tanzania ambayo inawataka kufanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria,  kanuni na taratibu zilizowekwa.

Mhe. Othman amefafanua kuwa Mahakama ya Tanzania inaendelea na Mkakati wa kupunguza mrundikano wa Kesi Mahakamani kwa kuhakikisha kuwa kesi zote zinazofikishwa Mahakamani  zinamalizika katika kipindi cha chini ya mwaka 1.

Ameeleza kuwa silimia 47 ya kesi zaidi ya 200 zilizokuwepo Mahakama Kuu katika kipindi cha miaka 4 iliyopita zimeendelea kusisikilizwa kwa ubora na sasa zimebaki asilimia 17 ya kesi hizo jambo linaonyesha kuongezeka kwa ufanisi wa Mahakama.

Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju akiwakaribisha Mawakili hao katika familia ya sheria Tanzania amesema kuwa katika jamii wanao mchango mkubwa katika kuhakikisha Haki na Usawa vinadumishwa nchini.

Amesema mawakili hao kabla ya kuapishwa na kuingizwa kwenye utaratibu wa kutambuliwa kuwa Mawakili wamepitia na kufauru vigezo vya kitaaluma vilivyowekwa ili kulinda heshima ya Taaluma ya sheria nchini.Amewaeleza kuwa mara baada ya kupokea viapo vyao wameingia kwenye utumishi wa umma kutekeleza majukumu yao ya kikatiba na kuongeza kwamba wao kama wanasheria wanatakiwa kuzingatia weledi wa taaluma yao. 

Amewataka kuwa makini katika utendaji wao kwa kuepuka kuwa sehemu ya migogoro na kuepuka kuegemea upande wowote watakapokuwa wakitimiza majukumu yao ili kuendelea kujenga jamii ya kistaarabu na ya kidemokrasia.

" Naomba mkumbuke kuwa mna wajibu mkubwa kwa watu mtakaokuwa mnawahudumia, zingatieni maadili maana ninyi sasa ni sehemu ya Mahakama ya Tanzania, fanyeni kazi kwa weledi na umakini mkubwa" Amesisitiza.Amesema utekelezaji wa majuku yao ya kila siku ni sehemu ya utumishi wao katika umma hivyo wasiruhusu aina yoyote ya ukiukwaji wa maadili yakitika kutimiza majukumu yao na kuwasaidia wananchi wasiokuwa na kipato/ wananchi masikini watakakao omba msaada wao wa kisheria.  

Aidha amewataka wawe wabunifu, kufanya kazi kwa bidii na kujiendeleza pale inapowezekana ili waweze kuwa msaada kwa wananchi walio na kiu ya kupata huduma kutoka kwao.Kwa upande wake Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Charles Rwechungura akizungumza wakati wa wa kuwakaribisha mawakili hao 134 amesema kuwa wao kama Chama cha Wanasheria wanayofuraha ya kuwakaribisha wanachama wapya kwenye uwanja wa Sheria nchini.

Amesema mawakili hao wameingia katika wakati muafaka kuongeza nguvu katika kuwahudumia wananchi huku akieleza kuwa shule ya Wanasheria Tanzania itaendelea kutoa mafunzo na kusimamia viwango vya taaluma ya sheria nchini na kuwataka mawakili hao kulinda heshima ya taaluma ya sheria kwa kutoa huduma bora kwa umma.

WAZIRI UMMY MWALIMU AWATAKA WATUMISHI WA SEKTA YA AFYA KUTOFANYA KAZI KWA MAZOEA


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo (15.12.2015) Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donald Mmbando na wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Hamis Kigwangalla.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo (15.12.2015) Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donald Mmbando na kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Hamis Kigwangalla.

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo (15.12.2015) Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii mara baada ya kulifungua Baraza hilo leo (15.12.2015) Jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Hamis Kigwangalla (wa tano kutoka kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donald Mmbando.

PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO 

Na Ismail Ngayonga
MAELEZO
Dar Es Salaam
15.12.2015
SERIKALI imewataka watumishi wa sekta ya afya nchini kutofanya kazi kwa mazoea na badala yake kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kufikia malengo yaliyowekwa.
Hatua hiyo inaelezwa itasiaidia kurahisisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi kwa kutoa huduma bora na zinazofikiwa kwa wakati.
Akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema kila mtumishi wa umma anapaswa kutekeleza kwa bidii ilani ya Chama Tawala ya mwaka 2015.
“Sekta ya Afya imeingizwa kwenye mpango wa Tekeleza kwa Matokeo makubwa sasa, ili tuyakifia matokeo makubwa sasa pamoja na mambo mengine tunahitaji kubadilika sana katika utendaji wetu wa kazi” alisema Mwalimu.
  Aidha Waziri huyo alisema alisema pamoja na mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa katika sekta ya afya, Wizara hiyo hiyo hiyo haina budi kuakabiliana na chyangamoto mbalimbali zinazojitokeza ikiwemo vifo vya akina mama wajawazito wakati wa kujifungua.
Kwa mujibu wa Waziri Mwalimu aliwataka watumishi wa Wizara hiyo kutekeleza kwa vitendo maagizo yaliyotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika hotuba yake ya kuzindua Bunge la 11, kwani hotuba yake ni dira ya maelekezo rasmi ya masuala muhimu yanayopaswa kutekelezwa na kusimamiwa katika kipindi cha miaka mitano.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donald Mmbando alisema katika kutekeleza mpango wa tekeleza kwa matokeo makubwa sasa, Serikali imeanisha maeneo 4 ya utekelezaji ili kuboresha huduma bora za afya kwa wanachi.
Dkt. Mmbando alianisha maeneo hayo kuwa ni pamoja mgawanyo wa watumishi wa kada ya afya, upatikanaji wa dawa, vifaa,  vifaa tiba na vitendanishi, ubora wa huduma pamoja na kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.
“Katika kutekeleza haya, wiki ijayo tutazindua mpango mkakati wa miaka 5 wa sekta ya afya (2016-20), ambapo tutahakikisha kuwa yote yaliyoanishwa katika Ilani ya Chama Tawala tunaweza kuyafikia na kuyatekeleza” alisema Dkt. Mmbando

KAMPUNI YA TINGATINGA IMEINGIA MKATABA NA KAMPUNI YA BRICOLEUR HOLDINGS Co.LIMITED YA JAPAN.




Mkurugenzi wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan, Bi. Yu Shiran (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu kushirikiana kufanya kazi za sanaa na Kikundi cha Sanaa cha Tingatinga, leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). Kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Sanaa Tingatinga, Bwana Zachi Chimwanda na kushoto ni Mkurugenzi pia wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan, Bwana Shoji Tsuchiya.
Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bwana Godfrey Mngereza akiwa na wanakikundi cha Sanaa cha Tingatinga na wajapani wakonyesha vibao vilivyochorwa na kikundi cha Sanaa cha Tinga Tinga jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bwana Godfrey Mngereza (kushoto) akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kusaini Mkataba wa makubaliano kati ya Kikundi cha Sanaa cha Tingatinga na Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan. Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan Bwana Shoji Tsuchiya pamoja na Bi. Yu Shiran. 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan Bwana Shoji Tsuchiya (kulia) wakibadilishana mikataba na kupeana mikono na Mwenyekiti wa Kikundi cha Sanaa cha Tingatinga, mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika wa mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Japan Bi. Yu Shiran. 
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwasikiliza na wakati wa kusaini wa Mkataba wa Makubaliano ya kufanya kazi na Kikundi cha Sanaa cha Tingatinga na Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan uliofanyika leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO)
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii..
Na Zainabu Hamis,Globu ya Jamii. 
CHAMA Cha Wasanii wa uchoraji picha aina ya Tingatinga imeingia mkataba wa miaka tano (5) na kampuni ya Bricoleurholdings Co.Limited ya nchini Japan, kwa ajili ya kuwatafutia soko nchini Japan 
Makabidhiano ya Mkataba huo yamefanyika leo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. 
Mwakilishi wa Kampuni ya Bricoleurholdings Co.Limited, Shoji Tsuchiya amemkabidhi mkataba huo Mwenyekiti wa Chama Cha Tingatinga, Zack Chimwanda, amesema kuwa kazi hii ya uchoraji wa picha aina ya Tingatinga imeanza nchini Tanzania ikiwa na mwanzilishi wake Edward Said Tingatinga ambaye alifariki dunia mwaka 1970 na jina la hilondipo lilipopatikana kutokana na yeye. 
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Hakimiliki Nchini (Cosota) Doreen Sinane,amesema kuwa kampuni ya BricoleurholdingsCo,Limited itakuwa inafanya kazi ya kuuza na kutafuta soko la picha zinazotengenezwa na wanachama wa Tingatinga. 
Kwa upande wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Ngereza, amesema kuwa sanaa ya uchoraji ni kazi kama kazi nyingine pia ni biashara inayomfanya msanii kupata kipato pamoja na kuliingizia taifa mapato.

SIMBACHAWENE AAGIZA TAKA ZILIZOKUSANYWA WAKATI WA UHURU ZIZOLEWE


wafanyakazi wa wizara ya ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora wakimsikiliza waziri wao George Simbachawene.
WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora George Simbachawene akizungumza na wafanyakazi wa wizara hiyo mjini Dodoma.
WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora George Simbachawene akipokelewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Jumanne Sagini alipowasili makao makuu ya ofisi hizo mjini Dodoma.
Naibu waziri nchi ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora, Selemani Jaffo akipokelewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Jumanne Sagini alipowasili makao makuu ya ofisi hizo mjini Dodoma
WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora George Simbachawene akisaini kitabu mara baada ya alipowasili makao makuu ya ofisi hizo mjini Dodoma.
 
WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora George Simbachawene amewaagiza wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurungenzi wote wa halmashari nchini kuhakikisha wanazoa taka zote zilizokusanywa wakati wa siku ya uhuru kabla ya tarehe 20 mwezi huu.Kauli hiyo aliitoa wakati alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati wa kikao cha kumkaribisha katika ofisi ya Tamisemi mjini Dodoma.

Alisema kuwa hataki kuona hadi ifikapo tarehe 20 ya mwezi huu kuwa uchafu wa siku ya uhuru bado unaendelea kulalamikiwa na watu kuwa bado haijaondolewa katika maeneo uliokusanywa.“Hadi ifikapo tarehe hiyo sitaki kusikia uchafu bado haujaondolewa katika maeneo ulipokusanywa toka siku ya uhuru lakini pia unapoondolewa huo kuna uchafu mwingine unakuja hivyo basi watendaji wanaohusika wa hakikishe kuwa wanaanda maeneo ya kuupeleka”alisema Simbachawene.

Aidha aliwataka watumishi wa Tamisemi kubadilika katika utendaji wa kazi zao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani awamu ya tano ya haitaendelea kuwalea watendaji wavivu.Kwa upande wake,Naibu Waziri wa wizara hiyo Suleiman Jaffo, aliwataka watumishi wa Tamisemi kubadilika katika utendaji wao wa zamani ili waweze kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuweza kuboresha maisha ya wananchi.

Uongozi wa Wizara yenye dhamana na Sanaa wakutana na Viongozi wa Mashirikisho ya Sanaa kujadili namna ya kuboresha tasnia ya Sanaa nchini

E51
: Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akizungumza na viongozi wa mashirikisho ya sanaa wakati wa kikao cha kuchanganua changamoto zilizopo katika tasnia ya sanaa jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Sanaa Bibi. Leah Kihimbi na kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo
E52
Rais wa Shirikisho la Sanaa za Maonyesho Bibi. Agnes Lukanga (wapili kulia) akichangia mada wakati wa kikao kilichoandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuchanganua changamoto zilizopo katika tasnia ya sanaa jana Jijini Dar es Salaam.
E53
Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifamba (wapili kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao kilichoandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuchanganua changamoto zilizopo katika tasnia ya sanaa jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni msemaji wa Shirikisho la Filamu Bw. John Kallage.
E54
Baadhi ya viongozi wa mashirikisho ya sanaa wakifuatilia kwa makini mada zilizokua zikiendelea wakati wa kikao kilichoandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuchanganua changamoto zilizopo katika tasnia ya sanaa jana Jijini Dar es Salaam.
E55
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (watatu kulia waliokaa) katika picha ya pamoja na viongozi wa mashirikisho ya sanaa baada ya kumaliza kikao cha kuchanganua changamoto zilizopo katika tasnia ya sanaa jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Sanaa Bibi. Leah Kihimbi, wapili kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo na watatu kushoto ni Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifamba.Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo

ENHANCE AUTO YAKABIDHI GARI KWA MSHINDI WA SHINDANO LA MATUMIZI BORA YA MITANDAO YA KIJAMII




Kamanda wa Kikosi Usalama barabarani, Mohamed Mpinga (kulia) akimkabidhi zawadi ya gari aina ya Toyota Sarf, mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Jackson Kapongo aliyeshinda kupitia mchezo wa Matumizi bora ya Mitandao ya Kijamii iliyoendeshwa na Kampuni ya Enhance Auto ya Jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Enhance Auto, Aatif Farooq Butt.Picha na Father Kidevu Blog.

Mkurugenzi wa Enhance Auto, Aatif Farooq Butt akionesha stika za kuhamasisha usalama barabarani ambazo pia zilizinduliwa na Kamanda Mpinga.

Meneja Mauzo Enhance Auto, Ayaka Kashida akionesha shindano jipya ambalo mshindi atajishindia Toyota Noah mpya.

Jackson Kapongo akiwa katika gari yake Toyota Sarf na pembeni yake ni Kamanda Mpinga.

Hii ndio gari jipya Toyota Sarf aliyo jishindia Kapongo. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA





Wageni mbalimbali waalikwa wakifuatilia tukio hilo.

Bahati na sibu ilichezeshwa na wateja kujishindia mipira .

Mkurugenzi wa Enhance Auto, Aatif Farooq Butta akitoa maelezo ya bahati nasibu ya kushinda mipira.

Na Father Kidevu

MHITIMU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jackson Kapongo ameibuka mshindi na kukabidhiwa gari aina ya Toyota surf lenye thamani ya zaidi ya sh milioni 24 katika shindano lililochezeshwa na kampuni ya kuuza magari ya Enhance Auto.

Kapongo alikabidhiwa gari lake hilo na Kamanda wa Polisi Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga baada ya kushinda katika shindano lililoendeshwa na Enhance Auto likiwataka washiriki kuonesha ni namna gani wanaweza kutumia mitandao ya kijamii na kujiletea manufaa.

Akizungumza kampuni hiyo, Mpinga alisema imekuwa ikichezesha shindano hilo kila mwaka na kushirikisha nchi mbalimbali Afrika ambapo kwa mwaka jana mshindi alipatikana kutoka Zambia lakini kwa mwaka huu ameshinda mtanzania hivyo ni jambo la kujivunia.

Alisema mbali na kutoa zawadi lakini kampuni hizo za magari zinajukumu kubwa la kutoa mchango kwa usalama barabarani kwa kutoa elimu sambamba na kuuza magari yenye viwango vinavyokubalika ili kuepusha ajali zisizo za lazima.

"Natoa wito kwa kampuni zingine kuwekeza katika usalama barabarani na wasifikirie tu kuuza magari bali wahakikishe magari yanakuwa salama na wanaoendesha wanakuwa salama... tuagize magari yenye viwango mana ajali nyingi pia zinasababishwa na ubovu wa magari" alisema.

Mapema Mkurugenzi wa Enhance Auto, Aatif Farooq Butt alisema shindano hilo mshiriki anatakiwa kushiriki kwa kuchagua mitandao yao ya kijamii kwa wingi zaidi na lilishirikisha nchi ambazo wanafanya nao biashara ikiwemo Botswana, Burundi, Jamhuri ya Kongo, Malawi, Msumbiji, Sudan ya Kusini, Uganda, Zambia, Zimbabwe na Tanzania.
 
Blogger Templates