Mkurugenzi
 wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini 
Tanzania, Peter Malika akizungumza na wageni waalikwa wakati wa 
makabidhiano ya misaada kwa miradi ya maendeleo iliyodhaminiwa na UNCDF 
Tanzania.
Naibu
 Katibu Mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba akisoma hotuba yake wakati 
wa kukabidhi hundi kwa mashirika binafsi na ya umma kwa ajili ya 
kuendeleza miradi ya maendeleo.
Naibu
 Katibu Mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba (katikati) akimkabidhi hundi
 bilioni moja na milioni sabini (1,070,000,000) Mkurugenzi wa Mji wa 
Kibaha, Bi. Jennifa C. Omolo (kulia) na kushoto ni Mkurugenzi wa Mfuko 
wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini Tanzania, 
Peter Malika.
Mkurugenzi
 wa Manispaa ya Moshi, Bw. Jeshi Godfrey Lupembe (kushoto) akikabidhiwa 
hundi ya shilingi milioni mia tano na tisa (509,000,000/=) na Naibu 
Katibu Mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba (kulia) pamoja na Mkurugenzi 
wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini 
Tanzania, Peter Malika.
Naibu
 Katibu Mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba pamoja na Mkurugenzi wa 
Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini 
Tanzania, Peter Malika wakiwakabidhi masisita hundi ya milioni miamoja 
na saba (107,000,000/=) wa kwanza kulia ni Msimamizi wa Mradi wa Umeme 
wa Lupali, Sister Imakulata Mlowe na Sister Helga Silinu ambaye ni fundi
 umeme katika mradi wa Lupali.
Mkuu
 wa wilaya ya Ileje , Mh. Rosemary Senyamule (kulia) akipokea hundi ya 
milioni mia mbili na milioni ishirini na sita (226,000,000/=) kutoka kwa
 UNCDF iliyotolewa na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, 
Kagyabukama E.Kiliba pamoja na Mkurugenzi wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo
 wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini Tanzania, Peter Malika.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiendelea kufuatilia kwa makini kinachozungumzwa na baadhi ya viongozi.
Mkurugenzi
 wa Mji wa Kibaha, Bi. Jenifa C. Omolo akitoa neno la shukrani kwa niaba
 ya sekta za umma na sekta binafsi zilizopata msaada huo ili kuendeleza 
miradi ya maendeleo hapa nchini.
Picha ya pamoja.
Na Mwandishi wetu 
  MFUKO
 wa Maendeleo ya Mtaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) umetoa msaada wa 
shilingi bilioni 2.4 kama kianzio cha mtaji kwa waandaaji wa miradi 
kutoka sekta binafsi na umma. Katika 
hafla iliyofanyika leo na kufunguliwa na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, 
Kagyabukama Kiliba hawala sita zilikabidhiwa wawakilishi wa waendeshaji 
katika miradi iliyotawanyika sehemu mbalimbali nchini. 
  Pamoja
 na hawala hizo za bilioni 2.4 imo pia shilingi bilioni 1.6 kwa ajili ya
 miradi yenye mwelekeo wa kibiashara inayoandaliwa na mamlaka za 
serikali za mitaa nchini Tanzania. Miradi
 iliyopewa kianzio cha mtaji ni pamoja na halmashauri ya mji wa Kibaha 
kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha basi na soko la kisasa, halmashauri ya 
manispaa ya Moshi kwa ajili ya kituo cha kisasa cha mabasi cha biashara 
na manispaa ya Ileje kwa ajili ya ujenzi wa mnara wa redio kwa 
kushirikiana na sekta binafsi. 
  Mradi
 mwingine ni wa uzalishaji wa umemejua (mtandao wa vijijini) 
unaotekelezwa wilaya ya Korogwe na kampuni binafsi ya Ensol, mradi 
binafsi wa uzalishaji umeme kwa maji unaoendeshwa na wanawake wa wilaya 
ya njombe vijijini na mradi mdogo binafsi wa uzalishaji umeme wa Maguta 
uliopo wilayani Kilolo. Akizungumza 
kumkaribisha mgeni rasmi kutoa hundi hizo, Mkuu wa UNCDF nchini Tanzania
 Peter Malika alisema msaada uliotolewa umelenga kuonesha mafanikio ya 
program ya mradi wa fedha za nahalia (LFI) wa UNCDF katika kusaidia 
waandaaji wanaojishughulisha na miradi inayotoa mchango katika maendeleo
 ya uchumi ya maeneo husika. 
  “Licha
 ya kuongezeka kwa upatikanaji wa mtaji wa uwekezaji kutoka vyanzo vya 
umma na binafsi kwa ajili ya miundombinu, ni kiasi kidogo sana 
kinachofikia miundombinu ambayo inaunda uti wa mgongo wa michakato ya 
uchumi. LFI ilibuniwa ili kushughulikia changamoto hizi na uliundwa ili 
kuonyesha kwamba miradi ya miundombinu ambayo inapewa kipaumbele na 
serikali za mitaa na jamii inaweza kuvutia fedha endapo matatizo ya soko
 la mtaji yaliyopo yatashughulikiwa” alisema Malika. 
  Aidha
 Malika alisema katika mwaka huu timu ya LFI ilitoa msaada wa kiufundi 
wa kulenga na kianzio cha mtaji kwa zaidi ya miradi 30,tisa kati ya hiyo
 ikiwa katika hatua za juu na kwa hiyo kuwa tayari kupokea uwekezaji 
ikiwemo miradi tisa iliyotunukiwa msaada jana. Tangu
 kuanzishwa kwake mwaka 2012 LFI-T imesaidia zaidi ya miradi ya 
maendeleo ya mahalia 30 nchini Tanzania katika hatua mbalimbali tangu 
uwekaji mipango hadi kuwa tayari kupokea uwekezaji kwa kufanyakazi kwa 
karibu na Tamisemi na taasisi za fedha. 
  Aidha
 LFI-T inasaidia miradi katika mikoa 18 iliyo katika sekta mbalimbali 
ikiwamo ya usindikaji mazao ya kilimo, tabia nchi, nishati salama na 
uzalishaji wa bidhaa za viwandani. Naye
 Naibu Katibu Mkuu Kiliba akizungumza na hadhara kabla ya kutunuku 
hawala hizo sita alisifu kazi ya ubunifu iliyofanywa na UNCDF katika 
utoaji fedha kwa maendeleo ya jamii na kusema hiyo ndiyo njia sahihi ya 
kusababisha maendeleo. Pia 
aliwapongeza waanzishaji wa miradi walipookea kianzia cha mtaji wa 
uwekezaji kutoka UNCDF na kuwatakia mafanikio mema huku akisema kwamba 
serikali ya Tanzania inakaribisha uendelezwaji wa program ya 
LFI-Tanzania. 
  Kiliba
 alisema kwamba wizara yake imeanzisha kitengo maalumu cha kuhakikisha 
kwamba miradi ya ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi katika 
halmashauri inafanikiwa.Mmoja wa 
wakurugenzi wa halmashauri waliopewa mtaji huo wa kianzio, Jenifa Omolo 
kutoka halmashauri ya mjui wa Kibaha alishukuru UNCDF kwa kufanikisha 
halmashauri ya Kibaha kuwa na soko la kisasa na kituo cha basi cha 
kisasa. 
  AlisemaUNCDF
 na Tamisemi wamekuwa mstari wa mbele katika kuwezesha kutekelezwa kwa 
wazo hilo kuanzia mwanzo hadi sasa wanapopata mtaji huo. Alihimiza
 halmashauri nyingine nchini kupata msaada wa kiufundi kwa mawazo yao 
kutoka UNCDF ili kuwa na uwezo wa kusimamia maendeleo ya umma na jamii.
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment