Rais
wa Chama cha Mawakala wa Forodha (Taffa), Stephen Ngatunga (kulia),
akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na njia
zinazotumika kuiba mapato ya serikali bandarini na katika Idara ya
Forodha, Jijini Dar es Salaam jana. kushoto ni maofisa waandamizi wa
chama hicho. Picha na Mpigapicha Wetu
Rais
wa Chama cha Mawakala wa Forodha (Taffa), Stephen Ngatunga (kushoto),
akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na njia
zinazotumika kuiba mapato ya serikali bandarini na katika Idara ya
Forodha, Jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Ofisa Mwandamizi wa chama
hicho, Ernest Kallaghe.
Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
CHAMA cha Mawakala wa Forodha nchini (TAFFA) kimesema kuwa wizi wa
kontena bandari ya Dar es Salaam na kusababisha serikali kukosa mapato
ni tatizo la muda mrefu ambalo ni limekuwa likisababishwa na watumishi
wa bandari.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Rais
wa TAFFA, Steven Ngatunga amesema tatizo lilojitokeza ya uondoshaji wa
kontena 329 katika bandari Kavu ya Azam ilitokana na baadhi ya watumishi
wa baadhi ya benki na Bandari kuingilia taarifa katika mfumo na
kusababisha serikali kukosa mapato.
Ngatunga amesema kuwa tatizo la serikali kukosa mapato katika
bandari ya Dar es Salaam walishagundua lakini serikali ilishindwa
kuchukua hatua mpaka serikali ya awamu ya tano kugundua hilo na hatua
zimechukuliwa kwa wale waliohusika.
Amesema TAFFA itatoa ushirikiano kwa kile ambacho wanakiona katika
bandari ya Dar es Salaam juu ya watu wanaosababisha serikali kukosa
mapato kwa maslahi yao binafsi.
Aidha amesema kuwa kuna kampuni zilionekana kuwa zipo kwa ajili ya
kukwepa kodi ya serikali ambazo chama kiliona na kupeleka malalamiko
ambayo mwisho wa siku kukawepo urasimu wa kukutana viongozi ambao
wanaweza kushughilikia hilo.
Amesema baadhi ya mawakala walilipia kontena lakini wanaambiwa
malipo hayakufanyika huku wakiwa na kumbukumbu za malipo na kusababisha
kutilia shaka juu ya uadilifu wa watumishi wa benki pamoja na bandari.
TAFFA imesema haiko tayari kwenda na mawakala ambao wanaharibu
taaluma hiyo na kusababishia serikali kukosa mapato ambayo ndio ya
kufanyia maendeleo nchini.
Amesema kuwa kuna kampuni 73 zimefungwa wakati hawahusiki katika
katika uondoshaji wa kontena katika bandari na bandari kavu kutokana na
kampuni hizo kuwa kulipia kontena zinazodaiwa kukwepa kodi.
0 comments:
Post a Comment