Naibu
Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akiongea na
watendaji wa Wizara na Taasisi alipokutana nao katika ukumbi wa Wizara
ya Fedha na Mipango. Akizungumza na uongozi wa Wizara na Taasisi Mhe.
Dkt. Ashatu Kijaji aliwaasa viongozi kutekeleza majukumu waliyokabidhiwa
na kuhakikisha bajeti ya Serikali inalenga vipaumbele vinavyogusa
wananchi katika kutekeleza ahadi ya Serikali.
Naibu
Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akijadiliana
na watendaji wa Wizara na Taasisi kuhusu masuala mbalimbali ya Wizara
pamoja na Taasisi zilizo chini ya Wizara.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt.
Servacius Likwelile akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri Wizara ya Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji kabla ya kuanza majadiliano na
watendaji wa Wizara na Taasisi.
0 comments:
Post a Comment