Mkurugenzi
 wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan, Bi. Yu Shiran 
(katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu 
kushirikiana kufanya kazi za sanaa na Kikundi cha Sanaa cha Tingatinga, 
leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). Kulia ni Mwenyekiti wa 
Kikundi cha Sanaa Tingatinga, Bwana Zachi Chimwanda na kushoto ni 
Mkurugenzi pia wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan, Bwana 
Shoji Tsuchiya.
Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), 
Bwana Godfrey Mngereza akiwa na wanakikundi cha Sanaa cha Tingatinga na 
wajapani wakonyesha vibao vilivyochorwa na kikundi cha Sanaa cha Tinga 
Tinga jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bwana 
Godfrey Mngereza (kushoto) akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati 
wa kusaini Mkataba wa makubaliano kati ya Kikundi cha Sanaa cha 
Tingatinga na Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan. Katikati ni
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan Bwana Shoji
 Tsuchiya pamoja na Bi. Yu Shiran. 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan Bwana 
Shoji Tsuchiya (kulia) wakibadilishana mikataba na kupeana mikono na 
Mwenyekiti wa Kikundi cha Sanaa cha Tingatinga, mbele ya waandishi wa 
habari leo jijini Dar es Salaam katika wa mkutano uliofanyika katika 
Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo
 ya Japan Bi. Yu Shiran. 
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwasikiliza na wakati wa kusaini 
wa Mkataba wa Makubaliano ya kufanya kazi na Kikundi cha Sanaa cha 
Tingatinga na Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan uliofanyika 
leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO)
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii..
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii..
Na Zainabu Hamis,Globu ya Jamii. 
CHAMA Cha Wasanii wa uchoraji picha aina ya Tingatinga imeingia 
mkataba wa miaka tano (5) na kampuni ya Bricoleurholdings Co.Limited ya 
nchini Japan, kwa ajili ya kuwatafutia soko nchini Japan 
Makabidhiano ya Mkataba huo yamefanyika leo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. 
Mwakilishi wa Kampuni ya Bricoleurholdings Co.Limited, Shoji 
Tsuchiya amemkabidhi mkataba huo Mwenyekiti wa Chama Cha Tingatinga, 
Zack Chimwanda, amesema kuwa kazi hii ya uchoraji wa picha aina ya 
Tingatinga imeanza nchini Tanzania ikiwa na mwanzilishi wake Edward Said
 Tingatinga ambaye alifariki dunia mwaka 1970 na jina la hilondipo 
lilipopatikana kutokana na yeye. 
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Hakimiliki Nchini (Cosota) Doreen 
Sinane,amesema kuwa kampuni ya BricoleurholdingsCo,Limited itakuwa 
inafanya kazi ya kuuza na kutafuta soko la picha zinazotengenezwa na 
wanachama wa Tingatinga. 
Kwa upande wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA)
 Godfrey Ngereza, amesema kuwa sanaa ya uchoraji ni kazi kama kazi 
nyingine pia ni biashara inayomfanya msanii kupata kipato pamoja na 
kuliingizia taifa mapato.
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment