Pages

Ads 468x60px

Tuesday, November 3, 2015

MAZOEZI YA KUAPISHWA KUWA RAIS DK MAGUFULI YAPAMBA MOTO JIJINI DAR

Kibanda cha kitakachotumika wakati wa kuapishwa kwa Rais Mteule, Dk John Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kesho kutwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Askari wa Jeshi la Wananchi akiigiza kama Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange na mwingine akiigiza kama Rais anayemaliza muda wake, Jakaya Kikwete wakati wa mazoezi ya sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange (wa pili kulia), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Maangu (wa tatu kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick wakipiga saluti ulipokuwa unaimbwa wimbo wa Taifa wakati wa mazoezi ya sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Maofisa mbalimbali wakiwa katika kibanda cha kiapo wakipanga jinsi viongozi watakavyokaa wakati wa sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam


Kikundi cha sarakasi kikitumbuiza wakati wa maandalizi hayo
Wasanii kutoka Zanzibar wakicheza ngoma ya kibati wakati wa mazoezi hayo
Mtu aliyeigiza kama Rais Jakaya Kikwete, akiwa amesimama alipokuwa akipigiwa mizinga ikiwa ni ishara ya kuagwa kwa rais huyo kabla ya kuapishwa Rais mpya wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli wakati wa mazoezi hayo.
Viongozi mbalimbali wakiwemo wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiwa Jukwaa Kuu wakati wa maandalizi hayo.
Baadhi ya wananchi wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa na Bendi ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakati wa maandalizi hayo.
Mtu aliyeigiza kama Rais Jakaya Kikwete, akielekea kukagua gwaride la heshima la kumuaga wakati wa mazoezi hayo

MHUBIRI MAARUFU DUNIANI TB JOSHUA WA NIGERIA ATUA DAR ES SALAAM KUSHUHUDIA DKT MAGUFULI AKIAPISHWA




Mtume TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations nchini Nigeria  ametua jijini Dar es salaam leo  tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.
Mara tu baada ya kutua uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, TB Joshua alikwenda Ikulu moja kwa moja kumsalimia Rais Jakaya Mrisho  Kikwete  kumsabahi na kumpongeza kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa uhuru na amani, huku akiondoka madarakani akiwa mtu mwenye furaha. TB Joshua amepongeza Rais Kikwete pia kwa kupata Dkt Magufuli kama mrithi wake, akimtaja Rais huyo mpya mteule kama Rais wa Tanzania wa Baraka na Fanaka tele katika awamu hii mpya.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Mtume TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii. TB Joshua ametua jijini Dar es salaam  tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.



 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mtume TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii.



 Dkt Magufuli ampokea TB Joshua Uwanja wa ndege Dar jioni hii. Mhubiri huyo aliyekuja na watu 40 kwa ndege yake mwenyewe, amekuja kushuhudia Dkt Magufuli akiapishwa

TANZAONE: MMEA WA ‘LOZERA’ HAUFAI KWA MATUMIZI YA BINADAMU


  Tabibu Gonzaga Marwa akiangalia baadhi ya mkopo ya Dawa jijini Dar es Salaam leo

TAASISI isiyo ya Kiserikali ya Tanzaone Herbal Clinic chini ya mradi wake wa ‘Tanzaone’ hatimaye imethibitisha pasipo shaka kuwa mmea ujulikanao kama Lozera na bidhaa zitokanazo na mmea huo hazifai kwa matumizi ya binadamu na wanyama.

Akizungumza na waandishi wa habari, sanjari na kuonyesha majibu ya vipimo vya kitaalamu kutoka Wakala wa Maabara ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa serikali kupitia utafiti uliofanywa chini ya mradi huo, Mratibu wa mradi.

 Tabibu Gonzaga Marwa, amesema  matokeo ya uchunguzi wa sampuli za mmea huo yameonesha una ukuvi yaani ‘fangasi’ aina ya Aspergillus ambao hutoa sumu ya Aflatoxin ambayo huweza kusababisha saratani ya maini.

Aidha, Tabibu Marwa ameiomba serikali kupitia Wizara ya Afya, na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA, kuhakikisha wanachukua hatua za haraka kunusuru afya za walaji, sambamba na kushauri wadau wa tiba asili nchini kufanya utafiti wa kina wa dawa za mitishamba na bidhaa zake kabla ya kumfikia mlaji.

Hati ya uchunguzi ya Mradi huo, namba 241/2013, uliopewa jina la ‘Tanzaone Red Tea Juice’ na kudumu kwa miaka mitatu 2010/2013, kwa kushirikisha watuamiaji wakubwa wa Lozera zaidi ya 250 nchini kote, ilichunguzwa, kuidhinishwa na kuthibitishwa na Mkemia Mkuu wa Serikali

NAIBU KATIBU MKUU MPYA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AANZA KAZI RASMI NA KUWATAKA WATUMISHI KUTEKELEZA KAULI MBIU YA “HAPA KAZI TU”

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi aliyeteuliwa hivi karibuni, John Mngodo, akijitambulisha kwa Watumishi  mara baada ya kuanza kazi rasmi  katika Wizara hiyo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Lilian Mapfa na kushoto ni Mwenyekiti wa TUGHE,  Obedi Mbaga.

Mkurugenzi wa Idara ya Sheria katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marlin Komba akijitambulisha mbele ya Naibu Katibu Mkuu mpya, John Mngodo (hayupo pichani) wakati wa Mkutano kati ya Watumishi na Naibu Katibu Mkuu huyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara.
Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, akizungumza na Watumishi mara baada ya kuanza kazi rasmi katika Wizara hiyo.
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara (hayupo pichani) alipofanya mkutano na watumishi hao mara baada ya kuanza kazi rasmi katika Wizara hiyo.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

MVUA ILIYONYESHA JIJINI MWANZA YASABABISHA MAAFA IKIWEMO VIFO NA UWANJA WA NDEGE KUFUNGWA KWA MUDA.




Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Jijini Mwanza, zimesababisha Uwanja wa ndege wa Jiji hili kufungwa kwa muda wa masaa matano kutokana na kujaa maji.

Meneja wa Uwanja huo Easter Madale alisema kuwa shughuli za usafirishaji uwanjani hapo, hii leo zilikwama kuanzia majira ya saa tatu asubuhi hadi saa nane mchana, baada ya maji ya mvua kujaa katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la kukimbilia ndege.

Alisema kuwa tatizo la maji kujaa uwanjani hapo halikusababishwa na ubovu wa miundombinu, bali ni kutokana na uwanja huo kuzungukwa na vilima vipatavyo saba ambavyo wakati wa mvua za masika hutiririsha maji ambayo huingia hadi uwanjani.

Madale alibainisha kuwa mara ya mwisho maji kujaa uwanjani hapo ilikwa mwaka 2012 na kwamba tatizo hilo lilishughulikiwa kwa kujengewa mifereji mikubwa kwa ajili ya kuzuia maji kuingia katika uwanja huo huku akiongeza mvua iliyonyesha leo imesababisha mifereji na mitaro kuharibika.

Baadhi ya wasafiri wamelalamikia hali hiyo kwa kile walichoeleza kuwa ni ratiba zao za kusafiri kwa ajili ya shughuli zao kukwama na hivyo kuingia kupata usufumbu mkubwa.

Katika hatua nyingine,Mvua hiyo zimesababisha athari mbalimbali kwa wakazi wa Jiji la Mwanza wakiwemo wakazi wa Kihewa, baada ya nyumba zao kujaa maji na hivyo baadhi ya kaya kuhifadhiwa katika shule ya Msingi Kilimahewa.


Kwa mjibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza Charles Mkumbo, mvua hiyo imesababisha vifo vya watu wawili, mmoja akifahamika kwa jina la Zainab Shaban (18) ambae alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Nyamanoro aliesombwa na maji wakati akijaribu kuwahi kwenye mtihani wa kuhitimu kidato cha nne pamoja na dereva pikipiki ambae jina lake halikufahamika mara moja.

Alfajiri ya leo Jiji la Mwanza lilikumbwa na mvua ambayo ilidumu kwa zaidi ya masaa matano, hali iliyosababisha adha mbalimbali kwa wakazi na wageni wa Jiji hili.

Hata hivyo Meneja wa Mamlaka ya hali ya hewa Kanda ya Ziwa Augustino Duganda amebainisha kuwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa itaendelea kuwa na mvua nyingi hadi kufikia mwezi wa 12 mwaka huu hivyo ni vyema wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi ikiwemo yenye mafuriko na mkondo wa maji wakahama kutoka kwenye maeneo hayo ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza.
Karibu Uwanja wa ndege wa Mwanza ila si wakati wa Mvua
BINAGI MEDIA GROUP, KWA PAMOJA TUIJUZE JAMII

Miongoni mwa nyumba zilizopo Mtaa wa Kilimahewa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza ambazo huathirika na kero ya Maji kuingia ndani pindi mvua zinapoanza kunyesha.
Pichani ni mmoja wa wakazi wa Kilimahewa akitoa maji ndani ya nyumba yake kutokana na mvua iliyoanza kunyesha majira ya saa kumi na mbili alfajiri hii leo. Hadi tunaenda hewani (saa 10:30 asubuhi) Mvua hiyo inaendelea kumiminika mdogomdogo.
Mbali na Kilimahewa, Pia wakazi wa Mabatini Jijini Mwanza hukumbwa na kero ya Mafuriko wakati wa Mafuriko na kwa miaka mingi juhudi za kuwahamisha zimekuwa zikigonga mwamba linapokuja suala la kuwatafutia makazi mapya.
Mara kadhaa mafuriko katika maeneo hayo yamekuwa yakisababisha athari mbalimbali ikiwemo vifo.
Maji hadi ndani, hakika ni hatari
Maji yakitolewa ndani
Kilimahewa Manispaa ya Ilemela
Binagi Media Group, Kwa Pamoja Tuijuze Jamii

TAWI LA CCM EMPRESS KWA MUSA MTAA WA SAMORA WASHEREHEKEA USHINDI WA DK. JOHN POMBE MAGUFULI.

1
MBUNGE mteule wa Muleba Kaskazini (CCM) na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Mwijage akisalimiana na Godson Kaligo Mjumbe wa tawi la CCM Epress Social lililopo mtaa wa Samora maarufu kwa Musa Shoeshine alipowatembelea wakati wa sherehe yao ya kusherehekea ushindi wa Rais Mteule Dr. John Pombe Magufuli mara baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu nchini kote, Wana CCM hao wamesherehekea kwa muziki na kupata supu ya mbuzi na nyama choma huku wakiwakaribisha wananchi mbalimbali bila kujali itikadi zao kwani Dr John Pombe Magufuli ni Rais wa Watazania wote.(PICHA NA RASHID SHOTI-DAR ES SALAAM)
3
MBUNGE mteule wa Muleba Kaskazini (CCM) na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Mwijage akibadilishana mawazio na Godson Kaligo na wana CCM wa tawi hilo.
4
Katibu wa Tawi hilo Musa Mtulia ambaye pia ni Shoeshine Maarufu mtaa wa Samora akiendelea na kazi yake huku wana CCM wengine na wadau wengine wakiendelea na sherehe hiyo kwa kupata supu.
5
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa tawi hilo Hassan Mneo. Mjumbe Godson Kaligo pamja na wadau wengine wakipata supu kutoka kulia ni Bw. Haogwa na Mzee Mnonji shabiki maarufu wa timu ya Simba.
6
Mwana CCM Richard Wambura aliyesimama nyuma naye alijumuika na wana CCM wenzake wakati alipowatembelea tawini hapo
7
Hapa ni mwendo wa kutafuna mbuzi tu.
8 9
Mwenyekiti Hassan Mneo kushoto na we nzake wakipata supu na kahawa katika wtawi hilo.
10
Katibu wa tawi Musa Mtulia akifurahi na wadau mbalimbali waliofika katika tawi hilo wakati wa sherehe hiyo.

WATALAAM WA TAKWIMU BARANI AFRIKA WAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM.

mku1
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza leo na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa siku tano ambao umekutanisha watalaam wa takwimu kutoka nchi mbalimbali barani Afrika kujadili Mfumo wa Uongozi Bora katika Ofisi za Takwimu pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu. Mkutano huo unafanyika katika hoteli ya Golden Tulip iliyopo Jijini Dar es Salaam.
mku2
Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Afrika Kusini Risenga Maluleke akizungumza leo na waandishi wa habari kuhusu madhumuni ya mkutano wa watalaam wa takwimu kutoka nchi mbalimbali barani Afrika ambapo wamekutana kujadili Mfumo wa Uongozi Bora katika Ofisi za Takwimu pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu. Mkutano huo ni wa siku tano na unafanyika katika hoteli ya Golden Tulip iliyopo Jijini Dar es Salaam.
mku3
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa watalaam wa takwimu kutoka nchi mbalimbali barani Afrika ambao wamekutana kujadili Mfumo wa Uongozi Bora katika Ofisi za Takwimu pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu. Kushoto kwake ni Mtakwimu kutoka Kamisheni ya Uchumi Afrika Bw. Andry Andriantseheno.
mku4
Baadhi ya wakuu wa Ofisi za Takwimu kutoka barani Afrika wakifuatilia kwa makini majadiliano wakati wa mkutano wa kujadili Mfumo wa Uongozi Bora katika Ofisi za Takwimu pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu. Mkutano huo ni wa siku tano na unafanyika katika hoteli ya Golden Tulip iliyopo Jijini Dar es Salaam.

Vyuo Vikuu wampongeza Dkt. Magufuli

 Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (CCM) Bi. Zainabu Abdallah akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akitoa pongezi  kwa Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli kwa niaba ya Shirikisho hilo leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Habari( MAELEZO).
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (CCM) Bi. Zainabu Abdallah (katikati)akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akitoa pongezi  kwa Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli kwa niaba ya Shirikisho hilo leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Habari( MAELEZO). Kushoto ni Katibu Msaidizi wa Shirikisho hilo Bw. Daniel Zenda na kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari

HANDENI MJINI KURUDIA KURA ZA MAONI

 Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba.

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM iliyokutana leo, Novemba 02,2015 chini ya Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete imejadili kwa kina mapendekezo ya wana CCM walioomba ridhaa ya kugombea ubunge katika jimbo la Handeni mjini.

 Kamati Kuu imetengua mapendekezo ya awali na kuagiza kurejewa kwa mchakato wa kura za maoni kwa wana -CCM wawili walioongoza kura za maoni za awali.

Wana- CCM hao watakaopigiwa kura za maoni tena kesho Novemba 03,2015 ni pamoja na Omari Abdallah Kigoda na Hamis Hamad Mnondwa.

Aidha Kamati Kuu imeteua wajumbe watatu kusimamia zoezi hilo ambao ni Dk. Maua Daftari, Dk.Emmanuel Nchimbi na Alhaji Abdallah Bulembo.
 
Blogger Templates