MBUNGE
mteule wa Muleba Kaskazini (CCM) na Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Charles Mwijage akisalimiana na Godson Kaligo Mjumbe wa tawi la CCM
Epress Social lililopo mtaa wa Samora maarufu kwa Musa Shoeshine
alipowatembelea wakati wa sherehe yao ya kusherehekea ushindi wa Rais
Mteule Dr. John Pombe Magufuli mara baada ya kushinda katika uchaguzi
mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu nchini kote, Wana CCM hao
wamesherehekea kwa muziki na kupata supu ya mbuzi na nyama choma huku
wakiwakaribisha wananchi mbalimbali bila kujali itikadi zao kwani Dr
John Pombe Magufuli ni Rais wa Watazania wote.(PICHA NA RASHID SHOTI-DAR
ES SALAAM)
MBUNGE
mteule wa Muleba Kaskazini (CCM) na Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Charles Mwijage akibadilishana mawazio na Godson Kaligo na wana CCM wa
tawi hilo.
Katibu
wa Tawi hilo Musa Mtulia ambaye pia ni Shoeshine Maarufu mtaa wa Samora
akiendelea na kazi yake huku wana CCM wengine na wadau wengine
wakiendelea na sherehe hiyo kwa kupata supu.
Kutoka
kushoto ni Mwenyekiti wa tawi hilo Hassan Mneo. Mjumbe Godson Kaligo
pamja na wadau wengine wakipata supu kutoka kulia ni Bw. Haogwa na Mzee
Mnonji shabiki maarufu wa timu ya Simba.
Mwana CCM Richard Wambura aliyesimama nyuma naye alijumuika na wana CCM wenzake wakati alipowatembelea tawini hapo
Hapa ni mwendo wa kutafuna mbuzi tu.
Mwenyekiti Hassan Mneo kushoto na we nzake wakipata supu na kahawa katika wtawi hilo.
Katibu wa tawi Musa Mtulia akifurahi na wadau mbalimbali waliofika katika tawi hilo wakati wa sherehe hiyo.
0 comments:
Post a Comment