Pages

Ads 468x60px

Tuesday, November 3, 2015

MVUA ILIYONYESHA JIJINI MWANZA YASABABISHA MAAFA IKIWEMO VIFO NA UWANJA WA NDEGE KUFUNGWA KWA MUDA.




Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Jijini Mwanza, zimesababisha Uwanja wa ndege wa Jiji hili kufungwa kwa muda wa masaa matano kutokana na kujaa maji.

Meneja wa Uwanja huo Easter Madale alisema kuwa shughuli za usafirishaji uwanjani hapo, hii leo zilikwama kuanzia majira ya saa tatu asubuhi hadi saa nane mchana, baada ya maji ya mvua kujaa katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la kukimbilia ndege.

Alisema kuwa tatizo la maji kujaa uwanjani hapo halikusababishwa na ubovu wa miundombinu, bali ni kutokana na uwanja huo kuzungukwa na vilima vipatavyo saba ambavyo wakati wa mvua za masika hutiririsha maji ambayo huingia hadi uwanjani.

Madale alibainisha kuwa mara ya mwisho maji kujaa uwanjani hapo ilikwa mwaka 2012 na kwamba tatizo hilo lilishughulikiwa kwa kujengewa mifereji mikubwa kwa ajili ya kuzuia maji kuingia katika uwanja huo huku akiongeza mvua iliyonyesha leo imesababisha mifereji na mitaro kuharibika.

Baadhi ya wasafiri wamelalamikia hali hiyo kwa kile walichoeleza kuwa ni ratiba zao za kusafiri kwa ajili ya shughuli zao kukwama na hivyo kuingia kupata usufumbu mkubwa.

Katika hatua nyingine,Mvua hiyo zimesababisha athari mbalimbali kwa wakazi wa Jiji la Mwanza wakiwemo wakazi wa Kihewa, baada ya nyumba zao kujaa maji na hivyo baadhi ya kaya kuhifadhiwa katika shule ya Msingi Kilimahewa.


Kwa mjibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza Charles Mkumbo, mvua hiyo imesababisha vifo vya watu wawili, mmoja akifahamika kwa jina la Zainab Shaban (18) ambae alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Nyamanoro aliesombwa na maji wakati akijaribu kuwahi kwenye mtihani wa kuhitimu kidato cha nne pamoja na dereva pikipiki ambae jina lake halikufahamika mara moja.

Alfajiri ya leo Jiji la Mwanza lilikumbwa na mvua ambayo ilidumu kwa zaidi ya masaa matano, hali iliyosababisha adha mbalimbali kwa wakazi na wageni wa Jiji hili.

Hata hivyo Meneja wa Mamlaka ya hali ya hewa Kanda ya Ziwa Augustino Duganda amebainisha kuwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa itaendelea kuwa na mvua nyingi hadi kufikia mwezi wa 12 mwaka huu hivyo ni vyema wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi ikiwemo yenye mafuriko na mkondo wa maji wakahama kutoka kwenye maeneo hayo ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza.
Karibu Uwanja wa ndege wa Mwanza ila si wakati wa Mvua
BINAGI MEDIA GROUP, KWA PAMOJA TUIJUZE JAMII

Miongoni mwa nyumba zilizopo Mtaa wa Kilimahewa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza ambazo huathirika na kero ya Maji kuingia ndani pindi mvua zinapoanza kunyesha.
Pichani ni mmoja wa wakazi wa Kilimahewa akitoa maji ndani ya nyumba yake kutokana na mvua iliyoanza kunyesha majira ya saa kumi na mbili alfajiri hii leo. Hadi tunaenda hewani (saa 10:30 asubuhi) Mvua hiyo inaendelea kumiminika mdogomdogo.
Mbali na Kilimahewa, Pia wakazi wa Mabatini Jijini Mwanza hukumbwa na kero ya Mafuriko wakati wa Mafuriko na kwa miaka mingi juhudi za kuwahamisha zimekuwa zikigonga mwamba linapokuja suala la kuwatafutia makazi mapya.
Mara kadhaa mafuriko katika maeneo hayo yamekuwa yakisababisha athari mbalimbali ikiwemo vifo.
Maji hadi ndani, hakika ni hatari
Maji yakitolewa ndani
Kilimahewa Manispaa ya Ilemela
Binagi Media Group, Kwa Pamoja Tuijuze Jamii

0 comments:

Post a Comment

 
Blogger Templates