Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi aliyeteuliwa hivi
karibuni, John Mngodo, akijitambulisha kwa Watumishi mara baada ya
kuanza kazi rasmi katika Wizara hiyo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa
Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Lilian Mapfa na kushoto ni
Mwenyekiti wa TUGHE, Obedi Mbaga.
Mkurugenzi
wa Idara ya Sheria katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marlin
Komba akijitambulisha mbele ya Naibu Katibu Mkuu mpya, John Mngodo
(hayupo pichani) wakati wa Mkutano kati ya Watumishi na Naibu Katibu
Mkuu huyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara.
Naibu
Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo,
akizungumza na Watumishi mara baada ya kuanza kazi rasmi katika Wizara
hiyo.
Watumishi
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu
mpya wa Wizara (hayupo pichani) alipofanya mkutano na watumishi hao mara
baada ya kuanza kazi rasmi katika Wizara hiyo.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
0 comments:
Post a Comment