
Kibanda
cha kitakachotumika wakati wa kuapishwa kwa Rais Mteule, Dk John
Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kesho kutwa kwenye
Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Askari wa Jeshi la Wananchi akiigiza kama Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi
nchini, Jenerali Davis Mwamunyange na mwingine akiigiza kama Rais
anayemaliza muda wake, Jakaya Kikwete wakati wa mazoezi ya sherehe za
kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa
Uhuru, Dar es Salaam.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange (wa pili kulia),
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Maangu (wa tatu kulia) na Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick wakipiga saluti ulipokuwa unaimbwa
wimbo wa Taifa wakati wa mazoezi ya sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu
ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.PICHA
ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Maofisa
mbalimbali wakiwa katika kibanda cha kiapo wakipanga jinsi viongozi
watakavyokaa wakati wa sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk
John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam

Kikundi cha sarakasi kikitumbuiza wakati wa maandalizi hayo

Wasanii kutoka Zanzibar wakicheza ngoma ya kibati wakati wa mazoezi hayo

Mtu
aliyeigiza kama Rais Jakaya Kikwete, akiwa amesimama alipokuwa
akipigiwa mizinga ikiwa ni ishara ya kuagwa kwa rais huyo kabla ya
kuapishwa Rais mpya wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli wakati wa mazoezi
hayo.

Viongozi mbalimbali wakiwemo wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiwa Jukwaa Kuu wakati wa maandalizi hayo.

Baadhi
ya wananchi wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa na Bendi
ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakati wa maandalizi hayo.

Mtu aliyeigiza kama Rais Jakaya Kikwete, akielekea kukagua gwaride la
heshima la kumuaga wakati wa mazoezi hayo
0 comments:
Post a Comment