Pages

Ads 468x60px

Friday, November 27, 2015

KAHAMA NEWS TZ: BREAKING NEWZZ......: RAIS MAGUFULI AMSIMAMISHA KA...

KAHAMA NEWS TZ: BREAKING NEWZZ......: RAIS MAGUFULI AMSIMAMISHA KA...: Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania, Mh. Dkt John Pombe Joseph Magufuli amemsimamisha kazi kuanzia leo tarehe 27 Nov....

BREAKING NEWZZ......: RAIS MAGUFULI AMSIMAMISHA KAZI KAMISHNA MKUU WA MAMLAKA YA MAPATO (TRA).

Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania, Mh. Dkt John Pombe Joseph Magufuli amemsimamisha kazi kuanzia leo tarehe 27 Nov. 2015, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndugu Rished Bade kufuatia ziara ya kushtukiza ya Waziri Mkuu, Mh. Majaliwa Kasimu Majaliwa mapema leo asubuhi Bandarini jijini Dar es salaam.

Hatua hiyo imekuja baada kubaini kupitishwa kwa makontena zaidi ya 300 na kusababishia hasara Serikali ya zaidi ya shilingi bilioni 80.

Rais Magufuli pia amemteua  Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango kukaimu nafasi hiyo mpaka hapo uchuguzi utakapo kamilika.

Taarifa hiyo iliyosomwa na Katibu Mkuu Kingozi, Balozi Ombeni Sefue Ikulu jijini Dar es salaam, imewataka maofisa wote wa TRA kutosafiri nje ya nchi mpaka pale uchunguzi dhidi yao utakapo kamilika.

BREAKING NEWZZZZZ....WAZIRI MKUU MAJALIWA AVAMIA BANDARI LEO, AAMRISHA KUKAMATWA KWA MAAFISA KIBAO WA TRA

WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi maafisa watano na watumishi watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutokana na upotevu wa makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 80/-.

Akizungumza na viongozi wa Mamlaka ya Bandari pamoja na viongozi wa TRA katika ziara ya kushtukiza leo mchana (Ijumaa, Novemba 27, 2015), Waziri Mkuu amewataka Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Rished Bade na Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Lusekelo Mwaseba wahahakikishe wanashirikiana na polisi kufuatilia upotevu huo na kwamba fedha hizo zinapatikana na zinarudi Serikalini.

Akitangaza uamuzi huo baada ya kufanya kikao na baadhi ya viongozi wa Serikali bandarini hapo, Waziri Mkuu aliwataja maafisa waliosimamishwa kazi kuwa ni Kamishna wa Forodha, Bw. Tiagi Masamaki na Mkuu wa Kituo cha Huduma kwa Wateja, Bw. Habibu Mponezya.

“Hawa wanasimamishwa kazi. IGP ninaagiza hawa watu wakamatwe na kuisaidia polisi. Hati zao za kusafiria zikamatwe na mali zao zikaguliwe kama zinaendana na utumishi wa umma,” alisema Waziri Mkuu.

Maafisa wengine waliosimamishwa kazi ni Mkuu wa kitengo cha TEHAMA, Bw. Haruni Mpande, Bw. Hamisi Ali Omari (hakutaja ni wa idara gani), na Mkuu wa Kitengo cha Bandari Kavu (ICD In-Charge), Bw. Eliachi Mrema. “Hawa wanasimamishwa kazi hadi uchunguzi utakapokamilika na pia wawe mikononi mwa polisi,” alisema.

Pia aliagiza watumishi watatu wa mamlaka hiyo wahamishwe kutoka Dar es Salaam na kupelekwa mikoani. Watumishi hao ni Bw. Anangisye Mtafya, Bw. Nsajigwa Mwandengele na Bw. Robert Nyoni.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemwagiza Katibu Mkuu wa Hazina, Dk. Servacius Likwelile ambaye alikuwepo kwenye kikao hicho, kuhakikisha kuwa anapeleka wataalamu kutoka Wakala wa Serikali Mtandao (e-Govt) haraka iwezekanavyo ili wakakague mifumo ya taarifa na kubaini jinsi ambavyo wizi huo unafanyika.

“Ninataka uchunguzi uanze kufanyika mara moja, tafuteni njia ambazo zinatumika kama mianya ya wizi kutokea hapa bandarini hadi kwenye ICDs. Nataka hayo makontena yatafutwe hadi yajulikane yako wapi, na fedha hiyo ihakikishwe inarudi serikalini,” alisema.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Bw. Ernest Mangu, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM, Suleiman Kova, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Bw. Awadh Massawe na viongozi mbalimbali kutoka TRA na TPA.

Mapema akijibu maswali ya Waziri Mkuu, Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Bade alikiri kwamba kuna upotevu wa makontena ambao huwa unafanyika kati ya bandarini na ICDs na hasa ICD ya Ubungo. Akitoa ufafanuzi, alisema kwamba walifanya ukaguzi kwenye ICD moja na kukuta makontena 54 yamepotea kwa njia za wizi. “Hata hivyo, tulipoendelea na ukaguzi, namba iliongezeka na kufikia 327. Tunaendelea kufuatilia kwa kushirikiana na TAKUKURU. Mmiliki wa ICD ametakiwa kulipa faini sh. bilioni 12.6/- na ameshalipa sh. bilioni 2.4/-,” alifafanua.

Alipoulizwa na Waziri Mkuu kama ana majina ya watumishi wanaohusika na wizi huo, Bw. Bade akakiri kwamba anayo lakini siyo kwa wakati huo labda ayapate kutoka kwa wasaidizi wake. Ndipo Waziri Mkuu akamuonyesha orodha ya makontena 349 yenye taarifa zote hadi namba za magari yaliyobeba mizigo hiyo na Bw. Bade akakiri kwamba orodha hiyo ni ya kweli.

“Kwa utaratibu huo hatuwezi kufika, labda baadhi ya watu waondolewe kazini”. Ndipo akaanza kutaja majina ya maafisa hao waliosimamishwa kazi.
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na uongozi wa TRA na TPA alipofanya ziara ya kustukiza Bandarini leo asubuhi.
 Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea na viongozi wa TRA na TPA
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akikabidhi orodha ya makontena yaliyopotea na ambayo TRA haina taarifa nazo
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akiagana na viongozi wa TRA na TPA.

Maagizo ya Rais Magufuli kuhusu safari za nje za watendaji wa Serikali yaanza kutekelezwa

Kufuatia maagizo ya Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoyatoa hivi karibuni ya kusitisha safari za nje kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imeanza kutekeleza maagizo hayo kwa kutoa maelekezo mahsusi kwa Balozi zake nje.

Wizara imezielekeza Balozi zote zilizopo maeneo mbalimbali duniani kujipanga ili kushiriki kikamilifu katika kuiwakilisha Serikali kwenye mikutano yote ya kimataifa na kikanda inayofanyika katika maeneo yao ya uwakilishi. Tanzania inazo Balozi 35; Balozi Ndogo tatu; Vituo viwili vya Biashara; na Konseli za Heshima 17 katika nchi mbalimbali. Hizi zote zitahusika katika kuendeleza utekelezaji wa Diplomasia yetu ya Uchumi na uwakilishi wa maslahi ya nchi yetu.

Aidha, hadi sasa Mikutano ambayo tayari imefanyika na Balozi zetu kuwakilisha ni pamoja na Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) unaoendelea nchini Malta na Mkutano wa Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Habari wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika nchini Lesotho.

Aidha, Wizara inatoa wito kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali kuwasilisha mapema taarifa za mikutano inayohusu sekta zao ili kutoa fursa kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuzifanyia kazi kwa wakati ili kuhakikisha ushiriki wa Tanzania unakuwa wenye tija kwa taifa.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inaungana na wadau wengine kumpongeza Mhe. Rais Magufuli kwa hatua anazozichukua za kuleta ufanisi mkubwa wa kazi na kubana matumizi ili kuiwezesha Serikali kuwahudumia wananchi kikamilifu.

Imetolewa na:
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
27 Novemba, 2015

Makumbusho ya Taifa yazindua maonyesho ya picha za matukio yanayohusu Albino nchini

al2Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabulla (kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa Under The Same Sun Bw. Peter Ash, Mwakilishi wa Benki ya Dunia Dkt. Yutaka Yoshino wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maonyesho ya Picha za matukio ya watu wa jamii ya Albino zilizo pigwa katika kambi ya kuwahudumia Albino ya Kabanga.
al3Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabulla (kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa Under The Same Sun Bw. Peter Ash, Mwakilishi wa Benki ya Dunia Dkt. Yutaka Yoshino wakipongezana mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maonyesho ya Picha za matukio ya watu wa jamii ya Albino zilizo pigwa katika kambi ya kuwahudumia Albino ya Kabanga.
al4Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabulla (kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa Under The Same Sun Bw. Peter Ash, Mwakilishi wa Benki ya Dunia Dkt. Yutaka Yoshino wakifurahia mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maonyesho ya Picha za matukio ya watu wa jamii ya Albino zilizopigwa katika kambi ya kuwahudumia Albino ya Kabanga.

al1 
Mratibu wa Maonyesho ya Picha za Alibino kutoka Makumbusho ya Taifa Bibi. Flora Vicent akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa maonyesho hayo jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yanafanyika kuanzia tarehe 26 Novemba 2015 hadi tarehe 26 Januari 2016
al5 
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu akifuatilia maelekezo ya Picha wakati hafla ya uzinduzi wa mmaonyesho ya picha maonyesho ya Picha za matukio ya watu wa jamii ya Albino zilizopigwa katika kambi ya kuwahudumia Albino ya Kabanga.
al6 
Wakiwa katika picha ya pamoja.

KAMPENI YA ABIRIA PAZA SAUTI YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM LEO


Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Abel Swai (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo, kuhusu kampeni ya Abiria Paza Sauti iliyozinduliwa Dar es Salaam leo asubuhi.

Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna wa Polisi, Mohamed Mpinga amesema kila mwananchi anawajibu kuzuia ajali za barabarani badala ya kudhani kazi hiyo ni ya polisi pekee.

Mpinga alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Abiria Paza Sauti iliyozinduliwa Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam leo asubuhi, ambao ulikwenda sanjari na mabalozi wa Usalama barabarani  (RSA) ambao walitoa elimu  kwa abiria kuhusu usalama barabarani.

"Abiria pazeni sauti pale mtakapoona dereva anaendesha gari lake ndivyo sivyo na kama mtapaza sauti itasaidia kupunguza ajali hapa nchini" alisema Kamanda Mpinga.

Mwakilishi  wa Mwenyekiti wa Usalama Barabarani ambaye ni Mratibu wa kampeni hiyo , Jackson Kalikuntima, alisema kampeni hiyo itaendelea nchini kote kwa njia ya kutoa elimu, haki na wajibu wa raia wanapokuwa safarini.

Waziri Mkuu Majaliwa azindua ununuzi wa hisa za Benki ya Walimu- MCB

Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa akigonga kengelle kuashiria uzinduzi wa ununuzi wa hisa za Benki ya Walimu- MCB kwenye soko la hisa la Dar es salaam. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es salaam Novemba 27, 2015. Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua uuzaji wa hisa za Benki ya Walimu MCB kwenye soko la hisa la Dar es salaam, uliofanyika jijini Dar es salaam Novemba 27, 2015. Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akiteta na baadhi ya Viongozi wa Benki ya Walimu- MCB baada ya kuzindua uuzaji wa hisa za Benki hiyo katika soko la hisa la Dar es salaam. Uzinduzi huo uliyofanyika jijini Dar es salaam Novemba 27, 2015
Waziri Mkuu,Majaliwa Kassim Majlaiwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile baada ya kuzindua mpango wa Benki ya Walimu MCB – MCB kuanza kuuza hisa zake kwenye soko la hisa la Dar es salaam Novemba 27, 2015. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dares salaam.3065 (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MWILI WA MAWAZO KUAGWA KITAIFA KATIKA UWANJA WA FURAHISHA JIJINI MWANZA

Mkutano wa Naibu Katibu Mkuu Chadema Salum Mwalimu na Wanahabari Jijini Mwanza hii leo.
Naibu Katibu Mkuu Chadema, Salum Mwalimu akionyesha kibali kilichotolewa na Manispaa ya Ilemela ili kuruhusu ibada ya kumuaga Marehemu Mawazo Kufanyika kesho katika Uwanja wa Furahisha
Mkutano wa Naibu Katibu Mkuu Chadema Salum Mwalimu na Wanahabari Jijini Mwanza hii leo (hawapo pichani).
Kushoto ni Ezekiel Wenje na Kulia ni Grace Kihwelu ambae ni Mbunge Viti Maalumu Chadema Mkoani Kilimanjaro
Singo Kigaila Benson ambae ni Mkurugenzi wa Mafunzo Chadema (Kushoto) akiwa na Peter Mekele ambae ni Mwenyekiti Chadema Kanda ya Ziwa Victoria (Kulia)

Husna Amri Said ambae ni Mwenyekiti BAWACHA Wilayani Geita
Viongozi na Makada wa Chadema
Mkutano wa kutoa ratiba za kuuaga mwili wa Marehemu Mawazo kwa wanahabari Jijini Mwanza hii leo
Wanahabari.
Na:Binagi Media Group
Mwili wa aliekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoa wa Geita Marehemu Alphonce Mawazo, kesho unatarajiwa kuagwa Jijini Mwanza kabla ya kusafirisha kwenda Mkoani humo kwa ajili ya Mazishi.

Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema Salum Mwalimu, amesema Marehemu Mawazo ataagwa Kitaifa kwa taratibu za chama hicho, katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.

Amesema ratiba hiyo itatanguliwa na ratiba ya kifamilia ya kuuaga mwili huo, ambayo itafanyika asubuhi Nyegezi Jijini Mwanza ambako ni nyumbani kwa Mchungaji Charles Lugiko ambae ni baba mdogo wa Marehemu Mawazo hiyo ikiwa ni baada ya mwili wake kutolewa katika Hospitali ya Rufaa Bugando ulikohifadhiwa.

Mwalimu amebainisha kwamba mwili huo utasafirishwa hiyo kesho kwenda Mkoani Geita kuanzia majira ya saa nane mchana ambapo wakazi wa Mkoa huo pia watapata fursa ya kuuagwa kesho kutwa jumapili.

Ameeleza kwamba kuanzia majira ya saa mbili asubuhi, shughuli za kuuaga mwili huo zitafanyika Kimkoa katika Uwanja wa Magereza Mjini Geita na baadae kusafirisha kwenda Katoro ambapo wakazi wa Jimbo lake la Busanda watapata fursa ya kuuaga mwili huo.

Mwalimu ametanabaisha kwamba, baada ya shughuli zote hizo kukamilika, mazishi ya Marehemu Mawazo yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu katika Kijiji cha Chikobe Jimbo la Busanda Mkoani Geita.

Shughuli zote hizo zinatarajiwa kuongozwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe, Viongozi waandamizi wa Chama hicho akiwemo Frederick Sumaye, aliekuwa mgombea urais wa Ukawa Edward Lowasa, wabunge pamoja na makada wa Chadema.

Ratiba za Mazishi ya Marehemu Mawazo ambae aliuawa Novemba 14 mwaka huu na watu wasiojulikana, zimejiri baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza jana kuondoa zuio la Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza, lililokuwa zinazuia mwili huo kuagwa Jijini Mwanza kutokana na hofu ya kiusalama pamoja na uwepo wa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambapo zuio hilo liliondolewa katika kesi iliyofunguliwa na baba mlezi wa Mawazo, Mchungaji Charles Lugiko baada mvutano mkali wa siku nne mahakamani hapo.

NHIF YAKAMILISHA UJENZI WA KITUO CHA KISASA CHA UCHUNGUZI NA MATIBABU KILICHOJENGWA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa NHIF, Michael Mhando akizungumza wakati wa makabidhiano ya  kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu kilichojengwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
 Mkurugenzi mtendaji kampuni ya ujenzi Tanzania Building Works Ltd, Mohamed Iqbal Moray(kushoto), akimkabidhi funguo za  kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu kilichojengwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa NHIF Michael Mhando.
 Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na uwezeshaji wa mfuko wa NHIF, Deusdedit Rutazaa akizungumza wakati wa makabidhiano ya kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu kilichojengwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma
Wafanyakazi wa mfuko wa NHIF na wa Hospitali ya rufaa ya Dodoma wakishiriki makabidhiano ya kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu kilichojengwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
 
  Jengo la ujenzi wa kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu kilichojengwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma
  Sehemu ya jengo la ujenzi wa kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu kilichojengwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma
  Sehemu ya jengo la ujenzi wa kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu kilichojengwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma

MFUKO wa Taifa wa Bima ya afya(NHIF) umekamilisha ujenzi wa kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu kilichojengwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma ambacho kitasaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali hiyo.
Akizungumza katika makabidhiano ya jengo hilo, Kaimu Mkurugenzi wa NHIF,  Michael Mhando, alisema kituo hicho kitakuwa cha kisasa na kitatoa huduma mbalimbali ikiwemo huduma za CT-Scan na kitafunguliwa kabla ya mwezi januari mwakani ili

“NHIF umelipatia ufumbuzi tatizo la msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma baada ya kukamilisha ujenzi wa jengo hili ambalo limegharimu kiasi cha sh. Bilioni sita ikiwa ni pamoja na vifaa vya matibabu na samani,”alisema Mkurugenzi huyo.

Alisema ujenzi wa huo umeanza tangu mwaka 2008 na litakuwa na uwezo wa kuchukua vitanda 34 vya
wagonjwa.
“Kituo hichi kitakuwa na vyumba vya madaktari, maabara,  upasuaji, chumba cha kutolea dawa, mapokezi,  chumba cha wagonjwa mahututi, chumba cha dharura, mfumo wa miito ya wauguzi, na vifaa tiba vya kisasa,”alisema Mhando

Alisema kitatoa huduma kwa wanachama wa mfuko huo, wananchi wa Mkoa wa Dodoma na mikoa jirani.

SERIKALI YAKANUSHA KUHUSU HAZINA KUACHWA TUPU

Na Jovina Bujulu-Maelezo

Serikali imekanusha taarifa zinazosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa amekomba fedha hazina na kuiacha Serikali bila fungu lolote.

Hayo yamesemwa jijini dare es salaam na Kamishina wa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha Bwa. John Cheyo huku akiwataka wananchi kupuuza habari hiyo kwani hazina ukweli wowote.

“Hazina inazo pesa za kutosha  na tunajivunia kufanya uchaguzi wa mwaka huu,  kununua mashine za BVR  kwa kutumia pesa za watanzania bila kutegemea msaada wowote kutoka nje ya nchi  na kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu mwaka huu” alisema Bwa. Cheyo.

Pia aliongeza kuwa serikali imeendelea kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa bomba la gesi ambalo limekamilika hivi karibuni, vinu vya kuchakata gesi na ujenzi wa barabara nchini.

Aliendelea kusema kwamba mfumo wa serikali wa bajeti unaiwezesha serikali kupanga vipaumbele vya matumizi kulingana na bajeti ilivyopangwa ambapo fedha zinazokusanywa kupitia mfuko mkuu wa serikali ndizo hutumika.

Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge kwa kipindi cha 2015-2016 ni shilingi Trilioni 22.5 na bajeti hiyo inatengenezewa mpango wa makusanyo na matumizi kwa kulipia mishahara ya wafanyakazi na miradi mbalimbali iliyoidhinishwa.

Pia katika matumizi mengine bajeti hiyo inalipia chakula cha wanafunzi, mikopo ya wanafunzi elimu ya juu, ununuzi wa dawa na vifaa tiba na chakula cha hifadhi ya taifa.

ROSE MUHANDO KUNOGESHA TAMASHA LA KUSHUKURU DIAMOND JUBILEE

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa matamasha ya muziki wa injili nchini Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati alipofafanua mambo mbalimbali kuhusu maandalizi ya tamasha la kushukuru baada ya kufanyika na  kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Tanzania salama salimini.

Msama amesema maandalizi yanaendelea vizuri na amemtangaza rasmi mwimbaji Rose Muhando kama mmoja wa waimbaji wa muziki wa injili watakaoshiriki katika tamasha hilo,  linalotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Desemba 25 na kushirikisha waimbaji wa kimataifa kutoka nchi za Afrika na Ulaya, ambapo ameongeza kwamba mazungumzo bado yanaendelea na waimbaji wengine kutoka nje ya nchi.

Katika picha katikati ni Mwimbaji wa muziki wa Injili Rose Muhando akishiriki katika mkutano huo na kushoto ni William Kapawaga mmoja wa waratibu wa Tamasha hilo kutoka Kampuni ya Msama Promotion.
Mwimbaji wa muziki wa Injili Rose Muhando akiwaelezea waandishi wa habari jinsi alivyojiandaa kutumbuiza katika tamasha hilo la kushukuru, Kulia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama.
baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion wakati alipokuwa akizungumza nao jijini Dar es salaam kuhusiana na Tamasha hilo.
 
Blogger Templates