Na Jovina Bujulu-Maelezo
Serikali
 imekanusha taarifa zinazosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa 
Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa amekomba 
fedha hazina na kuiacha Serikali bila fungu lolote.
Hayo
 yamesemwa jijini dare es salaam na Kamishina wa Bajeti kutoka Wizara ya
 Fedha Bwa. John Cheyo huku akiwataka wananchi kupuuza habari hiyo kwani
 hazina ukweli wowote.
“Hazina
 inazo pesa za kutosha  na tunajivunia kufanya uchaguzi wa mwaka huu, 
 kununua mashine za BVR  kwa kutumia pesa za watanzania bila kutegemea 
msaada wowote kutoka nje ya nchi  na kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu
 ya juu mwaka huu” alisema Bwa. Cheyo.
Pia
 aliongeza kuwa serikali imeendelea kugharamia miradi mbalimbali ya 
maendeleo ikiwemo ujenzi wa bomba la gesi ambalo limekamilika hivi 
karibuni, vinu vya kuchakata gesi na ujenzi wa barabara nchini.
Aliendelea
 kusema kwamba mfumo wa serikali wa bajeti unaiwezesha serikali kupanga 
vipaumbele vya matumizi kulingana na bajeti ilivyopangwa ambapo fedha 
zinazokusanywa kupitia mfuko mkuu wa serikali ndizo hutumika.
Bajeti
 iliyoidhinishwa na Bunge kwa kipindi cha 2015-2016 ni shilingi Trilioni
 22.5 na bajeti hiyo inatengenezewa mpango wa makusanyo na matumizi kwa 
kulipia mishahara ya wafanyakazi na miradi mbalimbali iliyoidhinishwa.
Pia
 katika matumizi mengine bajeti hiyo inalipia chakula cha wanafunzi, 
mikopo ya wanafunzi elimu ya juu, ununuzi wa dawa na vifaa tiba na 
chakula cha hifadhi ya taifa.
 
 
 
 
 
 

 
 
0 comments:
Post a Comment