Mkuu
wa Kitengo cha Elimu kwa Umma wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mrakibu
Msaidizi wa Polisi (ASP), Abel Swai (kulia), akizungumza katika mkutano
na waandishi wa habari Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo, kuhusu kampeni ya
Abiria Paza Sauti iliyozinduliwa Dar es Salaam leo asubuhi.
Na Dotto Mwaibale
MKUU
wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna wa Polisi,
Mohamed Mpinga amesema kila mwananchi anawajibu kuzuia ajali za
barabarani badala ya kudhani kazi hiyo ni ya polisi pekee.
Mpinga
alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Abiria Paza Sauti
iliyozinduliwa Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam leo
asubuhi, ambao ulikwenda sanjari na mabalozi wa Usalama barabarani
(RSA) ambao walitoa elimu kwa abiria kuhusu usalama barabarani.
"Abiria
pazeni sauti pale mtakapoona dereva anaendesha gari lake ndivyo sivyo
na kama mtapaza sauti itasaidia kupunguza ajali hapa nchini" alisema
Kamanda Mpinga.
0 comments:
Post a Comment