Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa matamasha ya muziki wa injili
nchini Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
salaam wakati alipofafanua mambo mbalimbali kuhusu maandalizi ya tamasha
la kushukuru baada ya kufanyika na kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa
Tanzania salama salimini.
Msama
amesema maandalizi yanaendelea vizuri na amemtangaza rasmi mwimbaji
Rose Muhando kama mmoja wa waimbaji wa muziki wa injili watakaoshiriki
katika tamasha hilo, linalotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Diamond
Jubilee Desemba 25 na kushirikisha waimbaji wa kimataifa kutoka nchi za
Afrika na Ulaya, ambapo ameongeza kwamba mazungumzo bado yanaendelea na
waimbaji wengine kutoka nje ya nchi.
Katika
picha katikati ni Mwimbaji wa muziki wa Injili Rose Muhando akishiriki
katika mkutano huo na kushoto ni William Kapawaga mmoja wa waratibu wa
Tamasha hilo kutoka Kampuni ya Msama Promotion.
Mwimbaji
wa muziki wa Injili Rose Muhando akiwaelezea waandishi wa habari jinsi
alivyojiandaa kutumbuiza katika tamasha hilo la kushukuru, Kulia ni
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama.
baadhi
ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion wakati alipokuwa akizungumza
nao jijini Dar es salaam kuhusiana na Tamasha hilo.
0 comments:
Post a Comment