Pages

Ads 468x60px

Thursday, November 26, 2015

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN, AKUTANA NA VIONGOZI WA MTANDAO WA ULINGO TANZANIA (UMOJA WA WANAWAKE WANASIASA).

has1 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na baadhi ya Wanawake wanaounda Umoja wa Wanawake Wanasiasa kutoka Vyama mbalimbali vya Siasa Tanzania walio katika Mtandao wa Ulingo, wakati alipokutana nao katika kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo hao maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
has3 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na baadhi ya Wanawake wanaounda Umoja wa Wanawake Wanasiasa kutoka Vyama mbalimbali vya Siasa Tanzania walio katika Mtandao wa Ulingo, wakati alipokutana nao katika kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo hao maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
has4 
Baadhi ya Wanawake Wanaulingo wakimsikiliza Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akiwahutubia kwenye katika kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo hao maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
has5 
Balozi Getrude Mongela, akichangia moja ya kati ya mada zilizokuwa zikizungumziwa katika kikao hicho leo. Picha na OMR
has6 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya Wanaulingo alipokuwa akipokelewa alipowasili kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria kwenye Kikao maalum kilichoandaliwa na Wanaulingo Tanzania kwa ajili ya kumpongeza . Picha na OMR

has7 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki kuimba wimbo maalum wa mshikamano kwa wanawake wakati wa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo Tanzania maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OM
has8 has9 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki kuimba wimbo maalum wa mshikamano kwa wanawake wakati wa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo Tanzania maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OM
has10Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi ya ‘Dua’ kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar na Katibu wa Ulingo Tanzania, Salama Aboud Talib, baada ya kumalizika kwa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo Tanzania maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
has11 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi ya picha baada ya kumalizika kwa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo Tanzania maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
has12 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifurahia jambo na Balozi Getrude Mongela baada ya kumalizika kwa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo Tanzania maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
has13Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Mtandao wa Ulingo Tanzania, wanaounda Umoja wa wanawake Wanasiasa wa Vyama mbalimbali vya Siasa Tanzania, baada ya kumalizika kwa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo hao maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
has15Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Mtandao wa Ulingo Tanzania, wanaounda Umoja wa wanawake Wanasiasa wa Vyama mbalimbali vya Siasa Tanzania, baada ya kumalizika kwa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo hao maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
has18Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na baadhi ya Viongozi wa Mtandao wa Ulingo Tanzania, wanaounda Umoja wa wanawake Wanasiasa wa Vyama mbalimbali vya Siasa Tanzania, baada ya kumalizika kwa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo hao maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015.

Serikali imejipanga kukuza na kuendeleza Stadi za Kazi nchini

za1
Mkurugenzi Msaidizi Toka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi Dkt.Jonathan Mbwambo akifafanua kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mpango wa Serikali wa kuendeleza stadi za kazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuongeza tija katika sekta zote nchini,kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Bi. Zamaradi Kawawa.
za2Mkurugenzi Msaidizi Toka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi Dkt.Jonathan Mbwambo akiwaeleza waandishi wa Habari kuhusu faida za kuendeleza stadi za kazi ikiwemo kuongeza uzalishaji katika sekta zote nchini,kulia Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Bi. Zamaradi Kawawa.
za3 
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi na vyombo vya habari leo jijini Dar eS Salaam uliolenga kueleza mpango wa Serikali kuwawezesha wananchi kupitia mpango wa kuendeleza stadi za kazi unaotarajiwa kuanza mwaka wa fedha 2016/2017.Picha Zote na Fatma

JK ATINGA OFISINI KWAKE LUMUMBA


Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye mara baada ya kuwasili kwenye Makao Makuu ya Chama Ofisi Ndogo Lumumba.

Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ofisini kwake Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba .

Serikali yajidhatiti kupambana na kemikali zenye madhara maeneo ya bandari

 
Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele akifungua mafunzo ya kujiandaa kukabiliana na dharura ya kemikali zenye madhara kwa afya na mazingira kwenye maeneo ya bandari leo jijini Dar es salaam. 
Meneja wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Mashariki Bw. Daniel Ndiyo akiwakaribisha wadau wa masuala ya kemikali kutoka Mataifa mbalimbali kushiriki katika mafunzo ya kujiandaa kukabiliana na dharura ya kemikali zenye madhara kwa afya na mazingira kwenye maeneo ya bandari leo jijini Dar es salaam. 
Wadau wa masuala ya kemikali kutoka Mataifa mbalimbali wakifuatilia mafunzo ya kujiandaa kukabiliana na dharura ya kemikali zenye madhara kwa afya na mazingira kwenye maeneo ya bandari leo jijini Dar es salaam. Mwakilishi kutoka nchini Ujerumani Bibi. Stefane Deuser akichangia mada kwenye warsha ya kujiandaa kukabiliana na dharura ya kemikali zenye madhara kwa afya na mazingira kwenye maeneo ya bandari.  
Mratibu wa Kanda kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mazingira (UNEP) Bw.Patrick Mwesigye akizungumza leo jijini Dar es salaam kwenye warsha ya kujiandaa kukabiliana na dharura ya kemikali zenye madhara kwa afya na mazingira kwenye maeneo ya bandari.

MAGUFULI ATINGA OFISINI KWA MAJALIWA


Rais John Magufuli akitia saini kitabu cha wageni wakati alipomtembelea Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa ofisini kwake jijini Dar es salaam Novemba 26, 2015 na kuzungumza nao kwa takribani saa moja (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Rais John Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa wakati alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam Novemba 26, 2015 na kuzungumza nae kwa takribani saa moja. Rais John Magufuli akiagana na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa wakati alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam Novemba 26, 2015 na kuzungumza nae kwa takribani saa moja.

Askofu Mkuu wa Tabora Kuongoza ujumbe wa Tanzania kumuona Papa Francis Uganda.


Na Joseph Ishengoma, MAELEZO
Askofu Mkuu wa jimbo kuu la Tabora Mhashamu Paulo Ruzoka kesho (tarehe 27.11.2015) anatarajia kuongoza ujumbe wa Tanzania kwenye ziara ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu Francis nchini Uganda.Baba Mtakatifu Francis anatarajia kuwasili nchini Uganda kesho kwa ziara ya siku mbili akitokea Kenya kabla ya kuelekea Afrika ya Kati. 

Hii ni ziara ya kwanza kwa kiongozi huyo Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani kutembelea Bara la Afrika tangu alipoliongoza Kanisa Katoliki mwaka 2013.
Katibu wa Baraza la Maaskofu (TEC) nchini Padre Raymond Saba amesema Mabaraza ya Maaskofu ya Kenya na Uganda kwa pamoja yalitoa mwaliko kwa TEC kushiriki katika ziara ya Baba Mtakatifu katika nchi hizo. 

“Tulipata mwaliko kutoka Kenya na Uganda, lakini tumeangalia nafasi yetu na jinsi ya kushiriki katika ziara hii. Hatukuweza kutuma mwakilishi Kenya, lakini Askofu Ruzoka ataiwakilisha TEC Uganda,” amesema. 

Kwa mujibu wa msemaji huyo, jana mabasi mawili ya waumini wa dini ya Kikristo yaliondoka mjini Mwanza kuelekea Namugongo, Uganda ambapo Baba Mtakatifu atakapofanyia ibada. Eneo la Namugongo ndipo Mfalme Kabaka Mwanga II alipowachoma na kuwaua mashahidi 22 wa Uganda waliofia dini katika karne ya 18. 

“Natoa wito kwa waumini wa Kanisa Katoliki nchini, wafuatilie na kusikiliza kwa makini ujumbe wa Baba Mtakatifu aliouleta katika Barani Afrika kwa sababu unagusa moja kwa moja amani na ushirikiano miongoni mwa jamii,” amesema. 

Kwa mujibu wa Padre Saba, Baba Mtakatifu hufanya ziara kufuatia mwaliko wa kanisa na serikali ya mahali husika au tukio la kimataifa linalohusiana na imani Katoliki. Amesema, “Kanisa pekee yake haliwezi kufanikisha ziara ya Baba Mtakatifu. Ndio maana alipofika Kenya alipokelewa na Rais Uhuru Kenyatta na hata alipokuwa Marekani alipokelewa na Rais Baraka Obama ingawa sio rahisi kwa kiongozi wa Marekani kumpokea mgeni uwanja wa ndege.” 

Ziara ya Baba mtakatifu nchini Marekani ilipangwa kabla hajawa kiongozi Mkuu wa kanisa Katoliki. Ziara hiyo ilitokana na kongamano la kimataifa la familia lililofanyika mjini Filadelphia. Papa Francis anatarajia kuhudhulia kongamano la vijana ulimwenguni nchini Poland mwaka 2016.

MBUNGE WA UBUNGO SAID KUBENEA AWATEMBELEA WANANCHI WAKE KUWASHUKURU KUMCHAGUA NA KUJUA CHANGAMOTO ZAO


 Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Said Kubenea akiongea na wananchi Stendi ya Mabasi ya Ubungo Dar es Salaam leo, kuwashukuru kwa kumchagua na kujua changamoto zao mbalimbali. Mbunge huyo jana alitembelea Soko la Ndizi la Mabibo, Soko la Mabibo, Kituo cha Mabasi cha Mawasiliano  na kumpa pole ya sh. milioni 1.1 Diwani wa Kata ya Manzese, Ramadhani Kwangaya ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Mus’ab kilicho chomwa moto na kuunguza magodoro 30.
 Kubenea akizungumza na waandishi wa habari na wananchi katika Soko la Ndizi la Mabibo.
 Hapa akiwaunga mkono wananchi kununua mananasi katika soko la ndizi la mabibo
 Mbunge Kubenea akisalimiana na wananchi katika soko hilo.
 Wafanyabiashara katika soko la ndizi la mabibo wakimsikiliza mbunge wao Said Kubenea.

Mbunge wa Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD Akiwashukuru Wapiga Kura Wake Wananchi wa Jimbo la Chumbuni

Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwasalimia Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakati wa mkutano wake wa kutowa shukrani kwa Wapiga kura wake mkutano uliofganyika katika Afisi za Jimbo Tawi la CCM Muembemakumbi Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwasalimia Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakati wa mkutano wake wa kutowa shukrani kwa Wapiga kura wake mkutano uliofganyika katika Afisi za Jimbo Tawi la CCM Muembemakumbi Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar wakati wa mkutano wake wa kutowa shukrani kwa Wananchi wa Jimbo hilo kwa kumchagua kuwa Mbunge wao na kuwataka kuwa wamoja na kujiandaa na maendekleo katika jimbo lake.
 Na kusema sasa makundi basi iliobaki ni Kazi Tu kwa maendeleo ya Wananchi wa Jimbo hilo na kusema yeye ni Mbunge wa Wananchi wa Chumbuni wote 
Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakimsikiliza Mbunge wao wakati wa hafla ya kuwashukuru 
Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakimsikiliza Mbunge wao wakati akitowa shukrani kwa wapiga kura wake katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Afisi ya Jimbo Tawi la CCM Muembemakumbi Zanzibar. 
Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakimsikiliza Mbunge wao wakati akitowa shukrani kwa wapiga kura wake katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Afisi ya Jimbo Tawi la CCM Muembemakumbi Zanzibar.

Serikali kuendelea kushirikiana na Vijana katika kutatua changamoto zao


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi ya ngao kutoka kwa Bibi. Dorice Assenga (katikati) kwa niaba ya Vijana kutoka Tanzania walioshiriki mkutano wa tatu wa Vijana kutoka nchi za Bonde la Mto Nile uliofanyika nchini Misri kuanzia tarehe 9 – 16 Novemba 2015 ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu kutoka nchi washiriki. Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza na Vijana wa Tanzania walioshiriki mkutano wa tatu wa Vijana kutoka nchi za Bonde la Mto Nile (hawapo pichani) uliofanyika nchini Misri kuanzia tarehe 6 – 14 Novemba 2015 ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu kutoka nchi washiriki. Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi
 Baadhi ya vijana wa Tanzania  walioshiriki mkutano wa tatu wa Vijana kutoka nchi za Bonde la Mto Nile uliofanyika nchini Misri kuanzia tarehe 9 – 16 Novemba 2015.Kutoka kushoto ni Baraka Chedego, Paul Simango na Rwihula Daniel
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na Vijana kutoka Tanzania walioshiriki mkutano wa tatu wa Vijana kutoka nchi za Bonde la Mto Nile uliofanyika nchini Misri kuanzia tarehe 9 – 16 Novemba 2015 ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu kutoka nchi washiriki.

Muhimbili Yapokea Mashine ya kusaidia wagonjwa kupumua


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN), Profesa Lawrence Mseru akipokea mashine ya ventilator ya kusaidia wagonjwa kupumua endapo wamezidiwa baada ya kuugua. Kushoto ni Mkurugenzi Mauzo wa Mashariki ya Kati na Afrika, Qasem Sumrein akikabidhi mashine hiyo leo.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN), Profesa Lawrence Mseru akitoa ufafanuzi baada ya kupokea mashine hiyo

Daktari Bingwa wa Magonjwa Mahututi na Uzingizi, Moa Kalunga katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akiwaeleza waandishi wa habari umuhimu wa mashine hiyo kwa wagonjwa.

Meneja Mauzo barani Afrika, Gordon Blair akimalizia kufunga mashine ya ventilator ambayo imekabidhiwa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa mashine mojaya Ventilator ya kumsaidia mgonjwa kupumua yenye thamani ya Dola za Kimarekani 36,000 sawa na Shilingi milioni 80. Msaada huo umetolewa leo na Kituo cha kitabibu cha Halmiton chenye makao yake makuu nchini Switzerland . 

Akikabidhi mashine hiyo mpya na kisasa , Mkurugenzi Mauzo wa Mashariki ya Kati na Afrika kutoka Halmiton , Qasem Sumrein amesema pamoja na kutoa msaada huo wataendelea kutembela MHN ili kutoa mafunzo jinsi ya kuitumia pamoja kufanya matengenezo endapo itahitajika kwa kuwa mashine hiyo ina waranti ya miaka miwili. 

Akipokea msaada huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MHN, Profesa Lawrence Mseru ameshukuru msaada huo ambao una lenga kuboresha huduma za afya na kueleza kwamba hospitali hiyo inahitaji kutengeneza ICU nyingine ikiwamo ya mama na mtoto hivyo bado zinahitajika mashine 120 kwa sababu MHN inapokea wagonjwa wengi. 
Akielezea kuhusu mashine hiyo Daktari Bingwa wa Magonjwa Mahututi na Usingizi Moa Kalunga amesema mashine hiyo itamsaidia mgonjwa aliye mahututi kupumua na hivyo kuokoa maisha yake na mgonjwa akirejea katika hali ya kawaida mashine hiyo inaonyesha

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA JESHI LA POLISI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (katikati), akishiriki kuimba wimbo wa mshikamano kwa wafanyakazi wakati wa kufungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Polisi uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Polisi, Kilwa road, jijini Dar es Salaam. Washiriki wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Polisi wakishiriki kuimba wimbo wa mshikamano kwa wafanyakazi, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza hilo uliofanyika Chuo cha Polisi Kilwa Road jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Polisi kilichofanyika Chuo cha Polisi, Kilwa Road jijini Dar es Salaam. Washiriki wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Polisi wakiwa katika mkutano Baraza hilo uliofanyika Chuo cha Polisi, Kilwa Road jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Abubakari Akida, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi) .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto), akipokelewa na Maofisa wa Jeshi la Polisi alipowasili Chuo cha Polisi Kilwa Road, kufungua Kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Jeshi hilo, jijni Dar es Salaam. 
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 
Blogger Templates