Mbunge
 wa Jimbo la Ubungo, Said Kubenea akiongea na wananchi Stendi ya Mabasi 
ya Ubungo Dar es Salaam leo, kuwashukuru kwa kumchagua na kujua 
changamoto zao mbalimbali. Mbunge huyo jana alitembelea Soko la Ndizi la
 Mabibo, Soko la Mabibo, Kituo cha Mabasi cha Mawasiliano  na kumpa pole
 ya sh. milioni 1.1 Diwani wa Kata ya Manzese, Ramadhani Kwangaya ambaye
 ni Mkuu wa Chuo cha Mus’ab kilicho chomwa moto na kuunguza magodoro 30.
 Kubenea akizungumza na waandishi wa habari na wananchi katika Soko la Ndizi la Mabibo.
 Hapa akiwaunga mkono wananchi kununua mananasi katika soko la ndizi la mabibo
 Mbunge Kubenea akisalimiana na wananchi katika soko hilo.
 Wafanyabiashara katika soko la ndizi la mabibo wakimsikiliza mbunge wao Said Kubenea.
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment