Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa
Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi ya ngao kutoka kwa Bibi. Dorice
Assenga (katikati) kwa niaba ya Vijana kutoka Tanzania walioshiriki
mkutano wa tatu wa Vijana kutoka nchi za Bonde la Mto Nile uliofanyika
nchini Misri kuanzia tarehe 9 – 16 Novemba 2015 ukiwa na lengo la
kubadilishana uzoefu kutoka nchi washiriki. Kulia ni Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa
Elisante Ole Gabriel akizungumza na Vijana wa Tanzania walioshiriki
mkutano wa tatu wa Vijana kutoka nchi za Bonde la Mto Nile (hawapo
pichani) uliofanyika nchini Misri kuanzia tarehe 6 – 14 Novemba 2015
ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu kutoka nchi washiriki. Kulia ni
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi
Baadhi ya vijana wa Tanzania walioshiriki
mkutano wa tatu wa Vijana kutoka nchi za Bonde la Mto Nile uliofanyika
nchini Misri kuanzia tarehe 9 – 16 Novemba 2015.Kutoka kushoto ni Baraka
Chedego, Paul Simango na Rwihula Daniel
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa
Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na Vijana kutoka
Tanzania walioshiriki mkutano wa tatu wa Vijana kutoka nchi za Bonde la
Mto Nile uliofanyika nchini Misri kuanzia tarehe 9 – 16 Novemba 2015
ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu kutoka nchi washiriki.
0 comments:
Post a Comment