Pages

Ads 468x60px

Monday, December 7, 2015

RAIS MAGUFULI AVUNJA BODI YA MAMLAKA YA BANDARI

* Atengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu TPA

* Amsimamisha kazi Katibu Mkuu Uchukuzi

* Waziri Mkuu awasimamisha kazi watumishi wengine 13 wa bandari


RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amevunja Bodi ya Mamlaka ya Bandari (TPA) na kutengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari, Prof. Joseph Msambichaka pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari, Bw. Awadhi Massawe.


Dkt. Magufuli pia ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaban Mwinjaka kuanzia leo (Jumatatu, Desemba 7, 2015), na kwamba atapangiwa kazi nyingine.


Akitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika leo ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hatua hizo zimechukuliwa kufuatia ziara mbili za kushtukiza alizozifanya katika mamlaka ya bandari Novemba 27 na Desemba 3, mwaka huu.


Waziri Mkuu amesema Rais Magufuli amevunja bodi hiyo na kutengua uteuzi wa viongozi hao kutokana na utendaji mbovu wa muda mrefu wa Mamlaka ya Bandari na kwa kitendo cha viongozi hao kutochukua hatua kwenye vyanzo.


Pia alisema Katibu Mkuu amesimamishwa kazi kwa sababu ya kutosimamia kwa makini mashirika mawili ya Bandari na Reli ambayo yako chini ya wizara yake ambako yeye mwenyewe alizuru Shirika la Reli (TRL) Desemba 3, 2015 na kukuta kuna ubadhirifu wa sh. bilioni 16.5/-.


“Tarehe 3 Desemba mwaka huu nilifanya ziara ya kushtukiza pale TRL nikakuta wametumia visivyo sh. bilioni 13.5/- walizopewa na Serikali. Pia nilikuta wamekopa sh. bilioni 3/- kutoka benki ya TIB lakini nazo wamezitumia nje ya utaratibu. Fedha hizi zilikuwa ni za kusaidia kuboresha miradi ya shirika lakini wao wamezitumia visivyo. Uchunguzi bado unaendelea,” alisema Waziri Mkuu.


Wakati huo huo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi kuanzia leo viongozi watano wa sekta zilizotoa ruhusa ya makontena kutoka ndani ya bandari pamoja na watumishi wanane wa bandari kavu ambao walihusika na ukwepaji kwa makontena 2,387.


“Viongozi hawa hawakuwemo kwenye ripoti ya ukaguzi lakini ni wahusika wakuu. Hawa ndiyo waliotoa ruhusa ili makontena yaende kwenye ICDs. Nao ni aliyekuwa Meneja Mapato ambaye kwa sasa amehamishiwa Makao Makuu kitengo cha Fedha, Bw.  Shaban Mngazija; aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Mkuu wa Bandari Kavu (ICD) – ambaye amehamishiwa Makao Makuu kwa Naibu Mkurugenzi Co-operate Services, Bw. Rajab Mdoe; Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Bw. Ibin Masoud; na Meneja Bandari Msaidizi – Fedha, Bi. Apolonia Mosha


Pia amewasimamisha kazi wasimamizi wanane wa Bandari Kavu (ICDs) ambao ni Happygod Naftari, Juma Zaar, Steven Naftari Mtui, Titi Ligalwike, Lydia Prosper Kimaro, Mkango Alli, John Elisante na James Kimwomwa ambaye alihamishiwa Mwanza lakini kuanzia sasa anasimamishwa kazi huko huko aliko.


“Bila wao kuidhinisha hakuna kontena linaweza kutoka au kwenda kokote. Watumishi wote hao wawe chini ya ulinzi na waisaidie polisi kupata taarifa hayo makontena ni ya nani na yana thamani gani,” Waziri Mkuu alisema.


Waziri Mkuu Majaliwa aliwaeleza waandishi wa habari kwamba Desemba 3, mwaka huu aliamua kurudi tena bandarini kufuatilia na kuangalia hatua ya udhibiti wa upitishaji wa bidhaa mbalimbali kinyume cha utaratibu. “Ziara yangu ilinipitisha hatua zote za upitishaji mizigo ambazo pia kwa mujibu wa Taarifa ya Ukaguzi wa Ndani ya tarehe 30 Julai 2015, Mamlaka ya Bandari iligundulika kuwepo kwa mianya mingi ya ukwepaji kodi ikiwemo makotena 2,387 yaliyopitishwa kati ya Machi – Septemba 2014 kinyume cha utaratibu”.


“Vitendo hivi vinaonyesha kuwa bandari yetu hupitisha makontena mengi bila ya kulipiwa kodi na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa. Serikali haitavumilia kuona watu wachache au kikundi chochote kilichojipanga kuhujumu mifumo au kuiibia Serikali kwa namna yoyote ile kwa manufaa ya wachache kwani bandari ni eneo muhimu ambalo likisimamiwa vizuri, linaweza kukusanya fedha nyingi na kuchangia Pato la Taifa,” alisema.



Desemba 3, mwaka huu, Waziri Mkuu alimpa saa tatu tu Kaimu Meneja wa Bandari, Bw. Hebel Mhanga amletee ofisini majina ya watumishi wote waliohusika na ukwepaji kodi huo. Pia alimpa Meneja huyo wiki moja kuhakikisha kuwa mamlaka hiyo inabadilisha mfumo wa utozaji malipo kutoka kwenye billing system na badala yake kuweka mfumo wa malipo wa kielektroniki (e-payment). Mwisho wa kukamilisha zoezi hilo ni Desemba 11, 2015.

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA URAFIKI

 Askari wakipita karibu na kiwanda cha urafiki jijini Dar es Salaam huku wakiwaangalia kwa makini wafanyakazi wa kiwanda hicho waliomo katika mgomo wakidai manejimenti yakiwanda hicho kiasi cha shilingi Bilioni 9.

Bidhaa zinazouzwa katika moja ya eneo la kiwanda cha urafiki yaliyokodishwa na uongozi wa menejimenti ya kiwanda hicho unaolalamikiwa na wafanyakazi kwamba wanajipatia mapato kwenye maeneo ya kiwanda hicho huku wao wakiwalipa kiduchu.
 Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha urafiki wakiwa kwenye geti la kuingilia kiwandani hapo wakimngoja Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ili kuzungumza nao.

Mkuu wa Wilaya ya kinondoni Paul Makonda, akiwasili na msafara wake kiwandani hapo kwa ajili ya kuzungumza na wafanyakazi walio katika mgomo. 
Mkuu wa Wilaya ya kinondoni Paul Makonda akizungumza na wafanyakazi wa Kiwanda cha Urafiki leo jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Urafiki wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.

MWENYEKITI WA CCM JAKAYA MRISHO KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA CCM, AKUTANA NA MWAKILISHI WA BENKI YA DUNIA

 Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho kikwete akiongozana na Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli , Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahmana Kinana kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015.
  Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho kikwete akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015.
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipigiwa saluti na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahmana Kinana kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015.


Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahmana Kinana.
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim. wengine ni Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa, Makamu wa Rais Mhe samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahmana Kinana kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015.
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015

EFM NA BENKI YA DTB KUFANYA USAFI DESEMA 9 MWAKA HUU JIJINI DAR ES SALAAM

 Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Efm Radio, Denis Ssebo akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya wasanii zaidi ya 50 wa Bongo Movie akiwamo Steve Nyerere, Wema Sepetu na Vicent Kigosi (Rey) wataungana na kituo cha redio cha EFM na Benki ya DTB kufanya usafi Desema 9 mwaka huu. Usafi huo utaanzia katika barabara ya Morocco hadi Magomeni, mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkuu wa Bidhaa na Masoko wa benki ya Diamond Trust Bank (DTB), Sylvester Bahati.
 Mkuu wa Bidhaa na Masoko wa benki ya Diamond Trust Bank (DTB), Sylvester Bahati akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya usafi ni nguzo moja wapo katika benki hiyo na si kwa ajili ya agizo la Rais John magufuli bali ni zoezi endelevu, kulia ni Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Efm Radio, Denis Ssebo.
Wandishi wa habari wakimsikiliza Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Efm Radio, Denis Ssebo, mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii.

 WASANII  wa 
Bongo Movie zaidi ya 50 akiwamo Steve Nyerere, Wema Sepetu na Vicent Kigosi (Rey) wataungana na kituo cha redio cha EFM na Benki ya DTB kufanya usafi Disemba 9 mwaka huu.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa EFM, Denis Ssebo, amesema usafi huo utaanzia katika barabara ya Morocco hadi Magomeni.

Ssebo amesema katika usafi huo EFM, DTB pamoja na wasanii hao watashirikiana na viongozi mbalimbali walioko madarakani pamoja na wakazi wa Kinondoni chini ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.

Kauli mbiu ya siku hoyo isemayo ‘Naona aibu kuishi na uchafu’ huku tukiunga kauli mbiu ya kinondoni ‘Usafi uanze na mimi’ endapo kila mmoja atatambua umuhimu wa usafi wake, mazingira yake tutaweza kwa pamoja kulimaliza tatizo la uchafu nchini,”amesema Ssebo. 


Kwa upande wake mwakilishi wa DTB Silvesta Bahati alisema usafi ni nguzo moja wapo katika benki hiyo na si kwa ajili ya agizo la Rais John magufuli bali ni zoezi endelevu.

NEC YATAOA TAMKO KUHUSU UCHAGUZI WA WABUNGE ARUSHA MJINI NA HANDENI.



 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu uchaguzi wa wabunge unaotarajiwa kufanyika Tarehe 13/12/2015 katika jimbo Handeni na Arusha Mjini, (kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura Bw.Clarence Nanyaro kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva(ambaye hayupo katika picha) leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waaandishi wa habari kuhusu taratibu zitakazo tumika katika uchaguzi wa wabunge katika jimbo la Arusha na Handeni.

RAIS MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI MKAZI WA BENKI YA DUNIA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli akisalimiana na mwakilishi mkazi wa Benki ya dunia Bi. Bella Bird alipomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli akizungumza na mwakilishi mkazi wa Benki ya dunia Bi. Bella Bird Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli akiagana  na mwakilishi mkazi wa Benki ya dunia Bi. Bella Bird Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

BENKI YA EXIM YAENDESHA DROO YA MWISHO YA KAMPENI YAKE YA AKAUNTI YA MALENGO.

Mmoja wa wateja wa Benki ya Exim Tanzania, Bw Kakili Juma (wa pili kushoto) akiokota karatasi yenye jina la mshindi wa droo ya mwisho na kubwa ya kampeni ya akaunti ya malengo ya Benki ya Exim Tanzania iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni kwa wiki.Wanaoshuhudia kushoto ni pamoja na Meneja Bidhaa ya benki hiyo, Bw Aloyse Maro, Mwakilishi kutoka Bodi ya Taifa michezo ya kubahatisha nchini (GBT), Bw Bakari Maggid, Meneja Masoko wa benki hiyo Bw. Abdulrahman Nkondo pamoja na Ofisa wa benki hiyo Bw. George Musetti.

BENKI ya Exim Tanzania imeendesha droo yake ya mwisho na kubwa ya kampeni ya akaunti ya malengo huku mteja wa benki hiyo Bw.Dileshkumar Solanki mkazi wa wa jijini Dar es Salaam akiibuka mshindi na hivyo kujishindia gari ndogo aina ya Toyota IST. 

Kampeni hiyo ilizinduliwa mwezi Mei mwaka huu ambapo kupitia kampeni hiyo benki hiyo imekua ikitoa zawadi mbalimbali za kila mwezi zikiwemo simu aina ya iPhone 6 kwa wateja waliobahatika kuibuka washindi kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini. 

Akizungumza kwenye hafla fupi ya uendeshaji wa droo hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, Meneja Bidhaa wa benki hiyo Bw Aloyse Maro alisema benki hiyo imeridhishwa na mwitikio mkubwa kutoka kwa wateja wake wakati wote wa kampeni hiyo inayolenga kuhamasisha utamaduni wa kuweka akiba miongoni mwa watanzania. 

“Kampeni hii imekuwa ni yenye mafanikio. Imepokelewa kwa mwamko mkubwa kutoka kwa wateja wetu hatua ambayo tumeitafsiri kwamba ni wazi wateja wetu wananufaika na wanafurahia huduma zetu,’’ alisema Bw Maro muda mfupi baada ya kufanyika kwa droo hiyo iliyosimamiwa na Bodi ya taifa michezo ya kubahatisha nchini (GBT) 

Bw. Maro aliongeza kuwa sambamba na zawadi hizo kampeni hiyo inaambatana na utoaji wa riba nzuri zaidi kwa wateja wanaofungua akaunti hiyo ya malengo. 

“Hatujaishia tu kwenye kutoa zawadi hizi kwenye kampeni hii bali tulihusisha pia utoaji wa riba nzuri zaidi kwa wateja wanaofungua akaunti yetu ya malengo,’’ alibainisha.

AIRTEL FURSA YATUA BUKOBA, YAONGEA NA VIJANA KUTOOGOPA VIKWAZO KATIKA UJASILIAMALI


 Mjasiliamali wa mjini Bukoba Adamu Hemed akipokea cheti kutoka kwa meneja biashara wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Mohamedi kabeke baada ya kuhudhuria mafunzo ya ujasiliamali yaliyoendeshwa na mradi wa Airtel FURSA kwa Zaidi ya vijana 200. kati ni Afisa ujasilimali wa VETA mjini bukoba Bw, Frabius Ngemela na Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando mwishoni mwa wiki hii mkoani Kagera.
 .Mkulima wa mboga mboga kutoka Bukoba mjini Agnetha Frenk akipokea cheti toka kwa meneja wa biashara Airtel BUkoba Mohamed kabeke baada ya kuhudhuria mafunzo ya ujasiliamali yaliyoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel mjini Bukoba kati ni Afisa ujasilimali wa VETA mjini bukoba Bw, Frabius Ngemela na anaefuata ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando. Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwa siku mmoja na kuhudhuriwa na vijana zaidi ya 200 mkoani Kagera.
Mkazi wa mtaa wa Nshambya mjini Bukoba Janath Shafi anayejishughulisha na biashara ya ufugaji wa mbuzi akipokea cheti toka kwa meneja wa biashara Airtel BUkoba Mohamed kabeke baada ya kuhudhuria mafunzo ya ujasiliamali kwa vijana yaliyandaliwa na kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Airtel mkoani Kagera. Cheti baada ya kuhudhuria mafunzo ya ujasiliamali yaliyoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Katikati ni mwalimu wa mambo ya ujasiliamali ambae pia ni Afisa ujasilimali wa VETA mjini bukoba Bw, Frabius Ngemela na anaefuata ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando. Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwa siku mmoja na kuhudhuriwa na vijana zaidi ya 200 mkoani Kagera.
 Kijana anayejishughulisha na ufugaji wa kuku kutoka Kijiji cha Katoka Wilaya ya Bukoba Vijijini Lucas Joseph akipokea cheti toka kwa meneja wa biashara Airtel BUkoba Mohamed kabeke baada ya kuhudhuria mafunzo ya ujasiliamali kwa vijana yaliyandaliwa na kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Airtel mkoani Kagera. Katikati ni mwalimu wa mambo ya ujasiliamali ambae pia ni Afisa ujasilimali wa VETA mjini bukoba Bw, Frabius Ngemela na anaefuata ni meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando. Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwa siku mmoja na kuhudhuriwa na vijana zaidi ya 200 mkoani kagera.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya ujasiliamali yaliyofanyika mjini Bukoba yaliondaliwa na kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa fursa tunakuwezesha. Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwa siku mmoja na kuhudhuriwa na vijana zaidi ya 200 mkoani kagera

· Bukoba zaidi ya wajasiliamali vijana 200 wanolewa na Airtel Fursa
KAMPUNI ya mawasiliano ya simu za mkononi airtel imewataka watanzania kuchangamkia fursa zilizopo kwa kufanya ujasiriamali kwa mtazamo mpana kwa lengo la kuondokana na umasikini au maisha duni yasiyo na kipato maalum.

Hayo yamesemwa na mwalimu wa mambo ya ujasiliamali ambae pia ni Afisa ujasilimali wa VETA mjini Bukoba Bw, Frabius Ngemela kwa zaidi ya wajasiliamali 200 waliohuduria semina ya ujasiliamali ya Airtel Fursa BUKOBA akiwataka vijana wajasiliamali kutumia ujuzi na maarifa katika kuboresha miradi yao kama njia mojawapo ya kukabiliana na suala la umasikini na kuwataka wajasiliamali hao kutokata tamaa ya maisha badala yake waongeze juhudi katika uzalishaji mali bila kuogopa vikwazo ili kujikomboa.

Airtel Fursa imekuja Bukoba leo kuwaambia msikate tamaa, nawafundisha leo kuvitambua vikwazo na msiviogope katika shughuli zenu, mkashirikiane na mradi wa Airtel Fursa ili kujikwamua.

Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alieleza “Airtel Fursa sio tu tunawasaidia vijana kuzitambua fursa pia tunawapatia mitaji na vitendea kazi muhimu ambavyo vimekua ni vikwazo vya kutimiza malengo yako ili uweze kuzalisha zaidi na kusaidia jamii zao.

“Hadi sasa tumeshazunguka mikoa zaidi ya 12 ndani ya miezi hii minne tukiwaeleza vijana jinsi wanavyoweza kukamata FURSA na kuwasaidia kupitia warsha kama hizi pia kuwapatia vitendeakuzalis kazi na vifaa mbalimbali waweze kuzalisha zaidi” alisema Mmbando.

wakiongea mara baada ya kupatiwa elimu ya ujasilimali baadhi ya wajasiliamali wadogo Peace Ruben MJASIRIAMALI, alisema licha ya kupatiwa elimu hiyo bado wanakabilina na changamoto mbalimbali ikiwemo mitaji ya kuendeshea biashara zao ambapo pia wametumia nafasi hiyo kuiomba kampuni ya airtel kwa kutumia mradio wao wa Airtel fursa kuwapatia mitaji itakayo wasaidia kuendesha biashara zao.

“Mi kazi yangu ni kufuma vitambaa na nguo za kuzuia baridi kwa watoto , wateja wangu wanapatikana kwa urahisi hapa bukoba na nje ya bukoba yaani hapo mpakani mwa Tanzania na Uganda lakini tatizo ni vitendea kazi vya kutosha ili kuongeza uzalishaji, ikiwa Airtel Fursa itanitoa nitafurahi sana” alieza Peace Ruben

MAHAFALI YA KWANZA YA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI (MoCU)

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) Pius Msekwa akitunuku Shahada ,Stashahada na Astashahada kwa wahitimu wa Chuo hicho wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho. 
Wahitimu wa kozi mbalimbali waliohitimu katika Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi,(MoCU) 
Miongoni mwa wageni waalikwa alikuwepo pia Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael. 
Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika (MoCU) Profesa Faustine Bee akizungumza wakati wa sherehe za mahafali ya kwanza ya Chuo hicho yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Chuo hicho. 
Miongoni mwa wahitimu walikuwepo pia Mbunge wa viti maalum,Sharry Raymond pamoja na Mkuu wa wilaya ya Mwanga ,Shaibu Ndemanga. 
Baadhi ya wakufunzi katika chuo hicho. 
Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro ,Severine Kahitwa (Kulia) akiteta jambo na Meneja wa benki ya NMB ,tawi la Mandela mjini Moshi ,Emanuel Kashusho wakatiwa mahafali ya kwanza katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi. 
Kaimu Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo (Utawala na Fedha) Ndayizera Manta (Kushoto) akiwa na Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) Profesa Gerald Monera wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo kikuu cha Ushirika Moshi. 
Muongozaji wa sherehe ya mahafali hayo Cyril Komba akitoa muongozo wa shughuli hiyo iliyofanyika viwanja ya Chuo kikuu cha Ushirika Moshi. 
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Pius Msekwa akitoka katika viwanja vya Ushirika mara baada ya kumalizika kwa sherehe ya mahafali ya kwanza ya chuo hicho. 
Baadhi ya wakufunzi wa Chuo hicho,Profesa Wakuru Magigi (kulia ) wakiwa na Mkuu wa Shule ya Polisi zamani Chuo cha Polisi Moshi,Matanga Mbushi . 
Mkuu wa wilaya ya Ilala,Raymond Mushi (kushoto) akiwa na mmmoja wa wakufunzi katika chuo hicho Dkt Kaleshu ,wakipozi katika picha ya pamoja na Mbunge wa Viti maalum CCM ,Sharry Raymond.

JUMUIYA YA KIMATAIFA YAOMBWA KUSAIDIA HUDUMA KAMBI YA NYARUGUSU

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) na ujumbe wake aliombatana nao Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (wa pili kushoto) pamoja na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (kushoto) kabla ya kuelekea kambi ya Nyarugusu walipita ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita kumsalimia pamoja na kusaini kitabu cha wageni. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

Na Mwandishi Wetu, Kigoma
JUMUIYA ya Kimataifa imekumbushwa kuisaidia Tanzania katika kuhudumia wakimbizi kutoka Burundi na Kongo ambao wanaishi katika kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma.

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakati akizungumza na waandishi wa habari mara tu baada ya kukamilisha ziara yake mkoani Kigoma.

Alisema kwamba serikali ya Tanzania kwa miaka mingi imekuwa na moyo wa huruma wa kusaidia majirani zake kwa kuhifadhi wakimbizi na kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kuona hilo na kusaidia Tanzania kufanikisha hifadhi ya wakimbizi.

Alisema Umoja wa Mataifa umekuwa ukishuhudia namna ambavyo serikali ya Tanzania inahudumia wakimbizi na kuridhika na hata pale ilipowapatia haki za kuwa Watanzania kwa kuwapa uraia na pia kusaidia kuwarejesha makwao wakati hali ilipokuwa njema.

Hata hivyo amesema kwa sasa hali ya Burundi na Kongo si njema na hivyo Watanzania kupata tena kazi yakuhifadhi wakimbizi.

Alisema Tanzania kwa huruma yake imetoa ardhi zaidi ili kupunguza msongamano katika kambi ya Nyarugusu na kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kusaidia kukamilisha makazi hayo mapema kabla ya mvua za masika ili wananchi hao waweze kuishi kwa amani.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita akimsikiliza kwa makini Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake kabla ya kuelekea kambi ya Wakimbizi Nyarugusu.

Alisema kambi ya Nyarugusu ni ya tatu kwa ukubwa duniani na inahifadhi zaidi ya wakimbizi 150,000 wakiwemo watoto na wanawake na wanahitaji huduma za shule, afya, maji na mengine.

Aidha wanahitaji nishati na hali hiyo haiwezi kuwezeshwa na serikali ya Tanzania pekee kwani watakuwa wakielemewa na huruma yake na moyo wa upendo kwa majirani zake.

“Dunia ikumbuke wema wa watanzania kwa miaka yote hii, na isaidie kuweka sawa hali ya kambi hiyo ili huduma zote muhimu za wananchi zipatikane” alisema mratibu huyo.

Akizungumza kuhusu wajibu wa Umoja wa Mataifa, alisema mashirika yake yamekuwa yakishirikiana na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kwamba wanatoa huduma kwa wakimbizi hao na kutaka wadau duniani kusaidia mashirika hayo na serikali ya Tanzania kufanikisha mahitaji muhimu kwa wakimbizi hao hadi hali itakapokuwa shwari katika nchi zao na kurejea kuishi makwao.

Tanzania imetoa maeneo matatu zaidi ya kupunguza msongamano katika kambi ya Nyarugusu na maeneo hayo yanahitaji huduma za msingi kama barabara, maji, vituo vya afya na shule.

Katika ziara hiyo ambayo aliambatana na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan, pamoja na kukagua maendeleo ya kambi ya Nyarugusu pia walikagua miradi inayofadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani ILO na ile ya Shirika la Mpango wa idadi watu duniani UNFPA.

ILO Kigoma inaendesha mafunzo ya ujasirimali kwa vijana kwa lengo la kuwawezesha kujiajiri wenyewe na kuhudumia familia zao kwa kuziwezesha kupata huduma bora za elimu na afya kutokana na kipato chao.
Katika msafara huo walikuwepo maafisa kutoka Shirika la linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) ofisi ya Kasulu mkoani Kigoma (walioipa mgongo kamera).

Alisema kwamba amefurahishwa na mradi huo ambao unawawezesha vijana kutambua fursa mbalimbali zilizopo na kuzitumia vyema kufanikisha maendeleo ya familia zao.

“Naona uwezekano wa vijana hawa kujiajiri na kuziwezesha familia zao kuondokana na tatizo la kipato.. elimu hii inaweza kutanzua mambo mengi na kuondoa changamoto nyingine zinazoambatana na kukosa kipato” alisema mratibu huyo.

Mkoa wa Kigoma una mashirika mengi ya Umoja wa Mataifa yakifanya kazi mbalimbali za maendeleo na za kutoa huduma za kibinadamu kwa wakimbizi.

Mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa yanayotekeleza miradi mbalimbali mkoani Kigoma ni pamoja na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Shirika la Afya Duniani ( WHO), Shirika la Mpango wa Uzazi (UNFPA), Shirika la Kazi la Kimataifa ( ILO), Shirika la Kuhudumia Watoto ( UNICEF), Shirika la Kuhudumia Wahamiaji ( IOM), Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Shirika la maendeleo (UNDP).

Akizungumza Afisa anayeshughulikia Ustawi na Usalama UNHCR, Kasulu, Bi. Zenobia Mushi, alisema shirika lake litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania na ya mkoa wa Kigoma katika kuhudumia wakimbizi kwa kuhakikisha kwamba mahitaji yao ya msingi yanapatikana.

Naye Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu Issa Machibya alishukuru Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kuwa tayari kusaidia mkoa wake.

“ Tunashukuru kwa mambo yanayofanywa na Umoja wa Mataifa katika dhima nzima ya ushirikiano katika kuhakikisha kwamba pengo la maskini na matajiri linazibwa na umaskini unaondolewa katika mkoa wa Kigoma.”
 

Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan akipiga picha kwenye bango linaloonyesha Serikali zinazofadhili misaada kwa Wakimbizi nchini Tanzania lililopo katika ofisi za UNHCR Kasulu.

Naye Mkuu wa wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita akizungumza kuhusu hali ya kambi ya Nyarugusu alisema kwamba hali ya kambi si nzuri na wakati msimu wa masika ukikaribia ni vyema Jumuiya ya Kimataifa ikaharakisha kukamilisha miundombinu ili kupunguza msongamano Nyarugusu.
Serikali imetoa maeneo mengine ya Nduta yaliyoko Kibondo na na Ntendeli, Kakonko kwa ajili ya kupunguza uwingi wa watu katika kambi hiyo.
DC huyo pia alisema kwamba kuna uharibifu mkubwa wa mazingira na lazima wadau wote washirikiane kuhakikisha kwamba mazingira yanaboreshwa pamoja na kupokea wakimbizi na kuwapa makazi.
Alisema kambi hiyo ilipangwa kuwa na watu elfu 50 kwa miaka ya 1996 lakini sasa inaweka wakimbizi wengi zaidi.
Aidha alisema kwamba pamoja na kupokea wakimbizi hao, inaonekana baadhi yao wameingia kufanya uhalifu na kuomba wakimbizi kushirikiana na polisi kuwataja wahalifu hao ili wadhibitiwe.
Kuwepo kwa kundi kubwa la wakimbizi kunasababisha uharibifu wa mazingira kama inavyoonekana pichani wakimbizi wakitoka kukata kuni kwenye misitu iliyopo karibu na kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Aidha katika mazungumzo ya shukurani kwa namna serikali ya Kigoma inavyotoa ushirikiano kwa Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika miradi ya maendeleo na misaada kwa wananchi na kwa wakimbizi, Mwakilishi wa Shirika la mpango wa idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem alisema kwamba kumekuwepo na mafanikio mengi kutokana na ushirikiano huo.
Alisema anachokiona yeye anaona hali ya baadae ya taifa la Tanzania kuwa bora zaidi kutokana na kuwapo kwa ushirikiano mzuri kati ya serikali, mashirika ya umma na kundi kubwa la vijana ambalo kwa sasa linapokea elimu mbalimbali kwa manufaa yao na ya baadae.
“Taifa la Tanzania nusu yake ni vijana na sehemu kubwa ni chini yake, taifa hili lina hali njema kabisa ya siku za usoni kutokana na ushirikiano wenye lengo la kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na wengi” alisema Kanem.
Anasema kwa kuangalia program zilizopo zinazotekelezwa kwa pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa na serikali anaona mafanikio ya mafunzo ya ujasiriamali na pia elimu inayotolewa kwa watu kwa malengo ya kufanikisha maendeleo.
Alisema UNFPA imefurahishwa sana namna mafunzo yanavyoendeshwa kwa vijana mafunzo ambayo yanaleta mshikamano wa pekee katika kufanikisha ustawi wa jamii na taifa kwa jumla.
Aidha alifurahi kuona kwamba wanawake wanashiriki katika kutoa elimu hivyo kuingiza sauti katika mafanikio ya jamii na uongezaji wa uelewa miongoni mwa jamii.
Mratibu huyo Mkazi wa UN Tanzania, Alvaro Rodriguez na timu yake wamerejea Dar es Salaam baada ya ziara ndefu kuangalia miradi ya Umoja wa Mataifa inavyoleta tija na ufanisi wa maisha katika jamii.
Mratibu huyo alitembelea mikoa ya Manyara, Singida, Tabora na Kigoma.
Katika ziara yake alioneshwa kufurahishwa na miradi hiyo inavyobadili jamii husika na kusema kwamba umoja huo utaendelea kufadhili miradi ya maendeleo nchini Tanzania.
 
Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile (kulia) akielezea changamoto mbalimbali zinazowakabili kambini hapo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) na ujumbe wake aliombatana nao Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (wa pili kushoto) pamoja na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (kushoto) kabla ya kutembelea makazi ya wakimbizi hao.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (kulia) na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan wakirekodi mambo muhimu wakati wa kupokea taarifa ya maendeleo ya kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu kutoka kwa Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile (hayupo pichani).
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem akizungumza jambo kwenye mkutano wa kupokea taarifa ya kambi hiyo.
Kutoka kushoto ni Afisa mahusiano wa UNHCR, Ofisi ya Kasulu, Agnes Mwangoka, Mshauri na Mtaalum wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Hoyce Temu, Mwandishi wa Habari, Prosper Kwigize pamoja na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan wakielekea kwenye kambi za Wakimbizi baada ya kupokea taarifa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem wakikagua ndani ya mahema wanakoishi Wakimbizi wapya wanaoendelea kuwasili katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem wakiuliza jambo kwa Ofisa Mtafiti Mshirikishi wa ofisi za UNHCR, Kasulu, Mariam Khokhar walipotembelea ndani ya mahema wanakoishi Wakimbizi wapya wanaoendelea kuwasili katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile.
Eneo la mahema ya kulalia familia za Wakimbizi wapya wanaoendelea kuwasili katika kambi ya Nyarugusu.
Mmoja wa Wakimbizi akiwa na mwanae nje ya chumba chake na mwanae katika kambi ya Nyarugusu.
Kuni zikitumika kupikia chungu cha Maharage kambini hapo.
Mtoto ambaye jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi akikoleza moto ulioonekana kufifia wakati akijiandalia chakula chake cha mchana kama alivyonaswa na kamera yetu. 
Moja ya familia ya Wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu wakiangalia msafara wa Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini uliotembelea kambini hapo mwishoni mwa juma.
Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan akipozi na moja ya familia katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisalimiana na Rais wa kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, Bi. Abilola Angelique wakati wa ziara yake ya kutembelea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
 
Blogger Templates