Mratibu
 Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la 
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) na ujumbe wake 
aliombatana nao Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa 
linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia 
Kanem (wa pili kushoto) pamoja na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya 
Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
 Kimataifa, Maulidah Hassan (kushoto) kabla ya kuelekea kambi ya 
Nyarugusu walipita ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita
 kumsalimia pamoja na kusaini kitabu cha wageni. (Picha zote na Zainul 
Mzige wa Modewjiblog).
Na Mwandishi Wetu, Kigoma
JUMUIYA
 ya Kimataifa imekumbushwa kuisaidia Tanzania katika kuhudumia wakimbizi
 kutoka Burundi na Kongo ambao wanaishi katika kambi ya Nyarugusu mkoani
 Kigoma.
Kauli 
hiyo imetolewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na 
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakati 
akizungumza na waandishi wa habari mara tu baada ya kukamilisha ziara 
yake mkoani Kigoma.
Alisema
 kwamba serikali ya Tanzania kwa miaka mingi imekuwa na moyo wa huruma 
wa kusaidia majirani zake kwa kuhifadhi wakimbizi na kuitaka Jumuiya ya 
Kimataifa kuona hilo na kusaidia Tanzania kufanikisha hifadhi ya 
wakimbizi.
Alisema
 Umoja wa Mataifa umekuwa ukishuhudia namna ambavyo serikali ya Tanzania
 inahudumia wakimbizi na kuridhika na hata pale ilipowapatia haki za 
kuwa Watanzania kwa kuwapa uraia na pia kusaidia kuwarejesha makwao 
wakati hali ilipokuwa njema.
Hata hivyo amesema kwa sasa hali ya Burundi na Kongo si njema na hivyo Watanzania kupata tena kazi yakuhifadhi wakimbizi.
Alisema
 Tanzania kwa huruma yake imetoa ardhi zaidi ili kupunguza msongamano 
katika kambi ya Nyarugusu na kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kusaidia 
kukamilisha makazi hayo mapema kabla ya mvua za masika ili wananchi hao 
waweze kuishi kwa amani.
Mkuu 
wa Wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita akimsikiliza kwa makini Mratibu 
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la 
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) alipomtembelea 
ofisini kwake kabla ya kuelekea kambi ya Wakimbizi Nyarugusu.
Alisema
 kambi ya Nyarugusu ni ya tatu kwa ukubwa duniani na inahifadhi zaidi ya
 wakimbizi 150,000 wakiwemo watoto na wanawake na wanahitaji huduma za 
shule, afya, maji na mengine.
Aidha 
wanahitaji nishati na hali hiyo haiwezi kuwezeshwa na serikali ya 
Tanzania pekee kwani watakuwa wakielemewa na huruma yake na moyo wa 
upendo kwa majirani zake.
“Dunia
 ikumbuke wema wa watanzania kwa miaka yote hii, na isaidie kuweka sawa 
hali ya kambi hiyo ili huduma zote muhimu za wananchi zipatikane” 
alisema mratibu huyo.
Akizungumza
 kuhusu wajibu wa Umoja wa Mataifa, alisema mashirika yake yamekuwa 
yakishirikiana na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kwamba wanatoa
 huduma kwa wakimbizi hao na kutaka wadau duniani kusaidia mashirika 
hayo na serikali ya Tanzania kufanikisha mahitaji muhimu kwa wakimbizi 
hao hadi hali itakapokuwa shwari katika nchi zao na kurejea kuishi 
makwao.
Tanzania
 imetoa maeneo matatu zaidi ya kupunguza msongamano katika kambi ya 
Nyarugusu na maeneo hayo yanahitaji huduma za msingi kama barabara, 
maji, vituo vya afya na shule.
Katika
 ziara hiyo ambayo aliambatana na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya 
Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
 Kimataifa, Maulidah Hassan, pamoja na kukagua maendeleo ya kambi ya 
Nyarugusu pia walikagua miradi inayofadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani
 ILO na ile ya Shirika la Mpango wa idadi watu duniani UNFPA.
ILO 
Kigoma inaendesha mafunzo ya ujasirimali kwa vijana kwa lengo la 
kuwawezesha kujiajiri wenyewe na kuhudumia familia zao kwa kuziwezesha 
kupata huduma bora za elimu na afya kutokana na kipato chao.
Katika
 msafara huo walikuwepo maafisa kutoka Shirika la linalohudumia 
Wakimbizi (UNHCR) ofisi ya Kasulu mkoani Kigoma (walioipa mgongo 
kamera).
Alisema
 kwamba amefurahishwa na mradi huo ambao unawawezesha vijana kutambua 
fursa mbalimbali zilizopo na kuzitumia vyema kufanikisha maendeleo ya 
familia zao.
“Naona
 uwezekano wa vijana hawa kujiajiri na kuziwezesha familia zao 
kuondokana na tatizo la kipato.. elimu hii inaweza kutanzua mambo mengi 
na kuondoa changamoto nyingine zinazoambatana na kukosa kipato” alisema 
mratibu huyo.
Mkoa 
wa Kigoma una mashirika mengi ya Umoja wa Mataifa yakifanya kazi 
mbalimbali za maendeleo na za kutoa huduma za kibinadamu kwa wakimbizi.
Mashirika
 hayo ya Umoja wa Mataifa yanayotekeleza miradi mbalimbali mkoani Kigoma
 ni pamoja na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Shirika la Afya 
Duniani ( WHO), Shirika la Mpango wa Uzazi (UNFPA), Shirika la Kazi la 
Kimataifa ( ILO), Shirika la Kuhudumia Watoto ( UNICEF), Shirika la 
Kuhudumia Wahamiaji ( IOM), Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) 
na Shirika la maendeleo (UNDP).
Akizungumza
 Afisa anayeshughulikia Ustawi na Usalama UNHCR, Kasulu, Bi. Zenobia 
Mushi, alisema shirika lake litaendelea kushirikiana na serikali ya 
Tanzania na ya mkoa wa Kigoma katika kuhudumia wakimbizi kwa kuhakikisha
 kwamba mahitaji yao ya msingi yanapatikana.
Naye 
Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu Issa Machibya alishukuru 
Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kuwa tayari kusaidia mkoa wake.
“ 
Tunashukuru kwa mambo yanayofanywa na Umoja wa Mataifa katika dhima 
nzima ya ushirikiano katika kuhakikisha kwamba pengo la maskini na 
matajiri linazibwa na umaskini unaondolewa katika mkoa wa Kigoma.”
Ofisa 
wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara 
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan akipiga 
picha kwenye bango linaloonyesha Serikali zinazofadhili misaada kwa 
Wakimbizi nchini Tanzania lililopo katika ofisi za UNHCR Kasulu.
Naye Mkuu wa wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita akizungumza kuhusu 
hali ya kambi ya Nyarugusu alisema kwamba hali ya kambi si nzuri na 
wakati msimu wa masika ukikaribia ni vyema Jumuiya ya Kimataifa 
ikaharakisha kukamilisha miundombinu ili kupunguza msongamano Nyarugusu.
Serikali imetoa maeneo mengine ya Nduta yaliyoko Kibondo na na 
Ntendeli, Kakonko kwa ajili ya kupunguza uwingi wa watu katika kambi 
hiyo.
DC huyo pia alisema kwamba kuna uharibifu mkubwa wa mazingira na 
lazima wadau wote washirikiane kuhakikisha kwamba mazingira yanaboreshwa
 pamoja na kupokea wakimbizi na kuwapa makazi.
Alisema kambi hiyo ilipangwa kuwa na watu elfu 50 kwa miaka ya 1996 lakini sasa inaweka wakimbizi wengi zaidi.
Aidha alisema kwamba pamoja na kupokea wakimbizi hao, inaonekana 
baadhi yao wameingia kufanya uhalifu na kuomba wakimbizi kushirikiana na
 polisi kuwataja wahalifu hao ili wadhibitiwe.
Kuwepo kwa kundi kubwa la wakimbizi kunasababisha uharibifu wa 
mazingira kama inavyoonekana pichani wakimbizi wakitoka kukata kuni 
kwenye misitu iliyopo karibu na kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu 
mkoani Kigoma.
Aidha katika mazungumzo ya shukurani kwa namna serikali ya Kigoma 
inavyotoa ushirikiano kwa Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika miradi ya
 maendeleo na misaada kwa wananchi na kwa wakimbizi, Mwakilishi wa 
Shirika la mpango wa idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem 
alisema kwamba kumekuwepo na mafanikio mengi kutokana na ushirikiano 
huo.
Alisema anachokiona yeye anaona hali ya baadae ya taifa la 
Tanzania kuwa bora zaidi kutokana na kuwapo kwa ushirikiano mzuri kati 
ya serikali, mashirika ya umma na kundi kubwa la vijana ambalo kwa sasa 
linapokea elimu mbalimbali kwa manufaa yao na ya baadae.
“Taifa la Tanzania nusu yake ni vijana na sehemu kubwa ni chini 
yake, taifa hili lina hali njema kabisa ya siku za usoni kutokana na 
ushirikiano wenye lengo la kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na wengi”
 alisema Kanem.
Anasema kwa kuangalia program zilizopo zinazotekelezwa kwa pamoja 
na mashirika ya Umoja wa Mataifa na serikali anaona mafanikio ya mafunzo
 ya ujasiriamali na pia elimu inayotolewa kwa watu kwa malengo ya 
kufanikisha maendeleo.
Alisema UNFPA imefurahishwa sana namna mafunzo yanavyoendeshwa kwa
 vijana mafunzo ambayo yanaleta mshikamano wa pekee katika kufanikisha 
ustawi wa jamii na taifa kwa jumla.
Aidha alifurahi kuona kwamba wanawake wanashiriki katika kutoa 
elimu hivyo kuingiza sauti katika mafanikio ya jamii na uongezaji wa 
uelewa miongoni mwa jamii.
Mratibu huyo Mkazi wa UN Tanzania, Alvaro Rodriguez na timu yake 
wamerejea Dar es Salaam baada ya ziara ndefu kuangalia miradi ya Umoja 
wa Mataifa inavyoleta tija na ufanisi wa maisha katika jamii.
Mratibu huyo alitembelea mikoa ya Manyara, Singida, Tabora na Kigoma.
Katika ziara yake alioneshwa kufurahishwa na miradi hiyo 
inavyobadili jamii husika na kusema kwamba umoja huo utaendelea 
kufadhili miradi ya maendeleo nchini Tanzania.
Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile (kulia) akielezea 
changamoto mbalimbali zinazowakabili kambini hapo kwa Mratibu Mkazi wa 
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo 
(UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) na ujumbe wake aliombatana nao 
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya 
watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (wa pili kushoto) pamoja
 na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa 
katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah 
Hassan (kushoto) kabla ya kutembelea makazi ya wakimbizi hao.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi 
ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (kulia) na Ofisa wa 
Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya 
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan wakirekodi 
mambo muhimu wakati wa kupokea taarifa ya maendeleo ya kambi ya 
Wakimbizi ya Nyarugusu kutoka kwa Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu B, Fredrick
 Nisajile (hayupo pichani).
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi 
ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem akizungumza jambo 
kwenye mkutano wa kupokea taarifa ya kambi hiyo.
Kutoka kushoto ni Afisa mahusiano wa UNHCR, Ofisi ya Kasulu, Agnes
 Mwangoka, Mshauri na Mtaalum wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa 
Tanzania, Hoyce Temu, Mwandishi wa Habari, Prosper Kwigize pamoja na 
Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika 
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan 
wakielekea kwenye kambi za Wakimbizi baada ya kupokea taarifa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa 
Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa 
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani 
(UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem wakikagua ndani ya mahema wanakoishi 
Wakimbizi wapya wanaoendelea kuwasili katika kambi ya Nyarugusu iliyoko 
wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa 
Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa 
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani 
(UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem wakiuliza jambo kwa Ofisa Mtafiti 
Mshirikishi wa ofisi za UNHCR, Kasulu, Mariam Khokhar walipotembelea 
ndani ya mahema wanakoishi Wakimbizi wapya wanaoendelea kuwasili katika 
kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Wa pili 
kushoto ni Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile.
Eneo la mahema ya kulalia familia za Wakimbizi wapya wanaoendelea kuwasili katika kambi ya Nyarugusu.
Mmoja wa Wakimbizi akiwa na mwanae nje ya chumba chake na mwanae katika kambi ya Nyarugusu.
Kuni zikitumika kupikia chungu cha Maharage kambini hapo.
Mtoto ambaye jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi akikoleza 
moto ulioonekana kufifia wakati akijiandalia chakula chake cha mchana 
kama alivyonaswa na kamera yetu. 
Moja ya familia ya Wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu wakiangalia
 msafara wa Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini uliotembelea 
kambini hapo mwishoni mwa juma.
Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa 
katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah 
Hassan akipozi na moja ya familia katika kambi ya Wakimbizi ya 
Nyarugusu.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa 
Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisalimiana na Rais wa 
kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, Bi. Abilola Angelique wakati wa ziara 
yake ya kutembelea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani 
Kasulu mkoani Kigoma.
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment