MFUKO wa Pensheni wa PPF, umeibuka kidedea kwa kutwaa tuzo ya uwasilishaji bora wa hesabu zake katika kipindi cha mwaka 2014.
Katika hafla ya kutoa tuzo kwa taasisi za serikali na za watu 
binafsi, Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu, NBAA, imetoa 
tuzo hizo kwa makampuni na taasisi mbalimbali nchini, ambapo kwa upande 
wa kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, PPF ndiyo iliibuka ya kwanza 
ambapo Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko huo, Bw. Martin Mmari kwa niaba ya 
Mkurugenzi Mkuu Bw. William Erio, alipokea tuzo hiyo kutoka kwa mgeni 
rasmi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Khamis Mwinyimvua. Pichani
 Bw. Mmari akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya 
Fedha, Bw. Khamisi Mwinyimvua. 
Bw. Khamisi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na umuhimu wa kuwasilisha taarifa sahihi za hesabu.
Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. Martin Mmari,
 (katikati), akiwa amekamata tuzo wakati wa kupiga picha na baadhi ya 
wafanyakazi wa Mfuko huo kwenye hafla ya kutolewa tuzo ya taasisi 
iliyowasilisha taarifa za mahesabu za mwaka 2014 kwa kuzingatia taratibu
 na kanuni za mahesabu kwenye kituo cha mikutano cha Bodi ya Uhasibu na 
Ukaguzi wa hesabu NBAA, huko Bunju nje kidoto ya jiji la Dar es Salaam, 
Desemba 5, 2015. PPF ilishika nafasi ya kwanza katika kundi la Mifuko ya
 Hifadhi ya Jamii. Tuzo hizo hutolewa na NBAA
Bw. Mamri (wapili kulia), akigongesha glasi na mmoja wa waalikwa wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wawakilishi wa PPF katika hafla hiyo.
 
 
 
 
 
 






 
 
0 comments:
Post a Comment