Askari
 wakipita karibu na kiwanda cha urafiki jijini Dar es Salaam huku 
wakiwaangalia kwa makini wafanyakazi wa kiwanda hicho waliomo katika 
mgomo wakidai manejimenti yakiwanda hicho kiasi cha shilingi Bilioni 9.
Bidhaa
 zinazouzwa katika moja ya eneo la kiwanda cha urafiki yaliyokodishwa na
 uongozi wa menejimenti ya kiwanda hicho unaolalamikiwa na wafanyakazi 
kwamba wanajipatia mapato kwenye maeneo ya kiwanda hicho huku wao 
wakiwalipa kiduchu.
 Baadhi
 ya wafanyakazi wa kiwanda cha urafiki wakiwa kwenye geti la kuingilia 
kiwandani hapo wakimngoja Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ili 
kuzungumza nao.
Mkuu 
wa Wilaya ya kinondoni Paul Makonda, akiwasili na msafara wake kiwandani
 hapo kwa ajili ya kuzungumza na wafanyakazi walio katika mgomo. 
Mkuu wa Wilaya ya kinondoni Paul Makonda akizungumza na wafanyakazi wa Kiwanda cha Urafiki leo jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Urafiki wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment