Mjasiliamali
wa mjini Bukoba Adamu Hemed akipokea cheti kutoka kwa meneja biashara
wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Mohamedi kabeke baada ya
kuhudhuria mafunzo ya ujasiliamali yaliyoendeshwa na mradi wa Airtel
FURSA kwa Zaidi ya vijana 200. kati ni Afisa ujasilimali wa VETA mjini
bukoba Bw, Frabius Ngemela na Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando
mwishoni mwa wiki hii mkoani Kagera.
.Mkulima
wa mboga mboga kutoka Bukoba mjini Agnetha Frenk akipokea cheti toka
kwa meneja wa biashara Airtel BUkoba Mohamed kabeke baada ya kuhudhuria
mafunzo ya ujasiliamali yaliyoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel mjini Bukoba kati ni Afisa ujasilimali wa VETA mjini bukoba Bw,
Frabius Ngemela na anaefuata ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson
Mmbando. Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwa siku mmoja na
kuhudhuriwa na vijana zaidi ya 200 mkoani Kagera.
Mkazi
wa mtaa wa Nshambya mjini Bukoba Janath Shafi anayejishughulisha na
biashara ya ufugaji wa mbuzi akipokea cheti toka kwa meneja wa biashara
Airtel BUkoba Mohamed kabeke baada ya kuhudhuria mafunzo ya ujasiliamali
kwa vijana yaliyandaliwa na kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi
ya Airtel mkoani Kagera. Cheti baada ya kuhudhuria mafunzo ya
ujasiliamali yaliyoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel,
Katikati ni mwalimu wa mambo ya ujasiliamali ambae pia ni Afisa
ujasilimali wa VETA mjini bukoba Bw, Frabius Ngemela na anaefuata ni
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando. Semina hiyo ilifanyika
mwishoni mwa wiki kwa siku mmoja na kuhudhuriwa na vijana zaidi ya 200
mkoani Kagera.
Kijana
anayejishughulisha na ufugaji wa kuku kutoka Kijiji cha Katoka Wilaya
ya Bukoba Vijijini Lucas Joseph akipokea cheti toka kwa meneja wa
biashara Airtel BUkoba Mohamed kabeke baada ya kuhudhuria mafunzo ya
ujasiliamali kwa vijana yaliyandaliwa na kampuni ya mawasiliano ya simu
za mkononi ya Airtel mkoani Kagera. Katikati ni mwalimu wa mambo ya
ujasiliamali ambae pia ni Afisa ujasilimali wa VETA mjini bukoba Bw,
Frabius Ngemela na anaefuata ni meneja uhusiano wa Airtel Jackson
Mmbando. Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwa siku mmoja na
kuhudhuriwa na vijana zaidi ya 200 mkoani kagera.
Baadhi
ya washiriki wa mafunzo ya ujasiliamali yaliyofanyika mjini Bukoba
yaliondaliwa na kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Airtel
kupitia mpango wake wa fursa tunakuwezesha. Semina hiyo ilifanyika
mwishoni mwa wiki kwa siku mmoja na kuhudhuriwa na vijana zaidi ya 200
mkoani kagera
· Bukoba zaidi ya wajasiliamali vijana 200 wanolewa na Airtel Fursa
KAMPUNI
ya mawasiliano ya simu za mkononi airtel imewataka watanzania
kuchangamkia fursa zilizopo kwa kufanya ujasiriamali kwa mtazamo mpana
kwa lengo la kuondokana na umasikini au maisha duni yasiyo na kipato
maalum.
Hayo
yamesemwa na mwalimu wa mambo ya ujasiliamali ambae pia ni Afisa
ujasilimali wa VETA mjini Bukoba Bw, Frabius Ngemela kwa zaidi ya
wajasiliamali 200 waliohuduria semina ya ujasiliamali ya Airtel Fursa
BUKOBA akiwataka vijana wajasiliamali kutumia ujuzi na maarifa katika
kuboresha miradi yao kama njia mojawapo ya kukabiliana na suala la
umasikini na kuwataka wajasiliamali hao kutokata tamaa ya maisha badala
yake waongeze juhudi katika uzalishaji mali bila kuogopa vikwazo ili
kujikomboa.
Airtel
Fursa imekuja Bukoba leo kuwaambia msikate tamaa, nawafundisha leo
kuvitambua vikwazo na msiviogope katika shughuli zenu, mkashirikiane na
mradi wa Airtel Fursa ili kujikwamua.
Kwa
upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alieleza “Airtel
Fursa sio tu tunawasaidia vijana kuzitambua fursa pia tunawapatia mitaji
na vitendea kazi muhimu ambavyo vimekua ni vikwazo vya kutimiza malengo
yako ili uweze kuzalisha zaidi na kusaidia jamii zao.
“Hadi
sasa tumeshazunguka mikoa zaidi ya 12 ndani ya miezi hii minne
tukiwaeleza vijana jinsi wanavyoweza kukamata FURSA na kuwasaidia
kupitia warsha kama hizi pia kuwapatia vitendeakuzalis kazi na vifaa
mbalimbali waweze kuzalisha zaidi” alisema Mmbando.
wakiongea
mara baada ya kupatiwa elimu ya ujasilimali baadhi ya wajasiliamali
wadogo Peace Ruben MJASIRIAMALI, alisema licha ya kupatiwa elimu hiyo
bado wanakabilina na changamoto mbalimbali ikiwemo mitaji ya kuendeshea
biashara zao ambapo pia wametumia nafasi hiyo kuiomba kampuni ya airtel
kwa kutumia mradio wao wa Airtel fursa kuwapatia mitaji itakayo wasaidia
kuendesha biashara zao.
“Mi
kazi yangu ni kufuma vitambaa na nguo za kuzuia baridi kwa watoto ,
wateja wangu wanapatikana kwa urahisi hapa bukoba na nje ya bukoba yaani
hapo mpakani mwa Tanzania na Uganda lakini tatizo ni vitendea kazi vya
kutosha ili kuongeza uzalishaji, ikiwa Airtel Fursa itanitoa nitafurahi
sana” alieza Peace Ruben
0 comments:
Post a Comment