Mmoja
wa wateja wa Benki ya Exim Tanzania, Bw Kakili Juma (wa pili kushoto)
akiokota karatasi yenye jina la mshindi wa droo ya mwisho na kubwa ya
kampeni ya akaunti ya malengo ya Benki ya Exim Tanzania iliyofanyika
makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni kwa
wiki.Wanaoshuhudia kushoto ni pamoja na Meneja Bidhaa ya benki hiyo, Bw
Aloyse Maro, Mwakilishi kutoka Bodi ya Taifa michezo ya kubahatisha
nchini (GBT), Bw Bakari Maggid, Meneja Masoko wa benki hiyo Bw.
Abdulrahman Nkondo pamoja na Ofisa wa benki hiyo Bw. George Musetti.
BENKI
ya Exim Tanzania imeendesha droo yake ya mwisho na kubwa ya kampeni ya
akaunti ya malengo huku mteja wa benki hiyo Bw.Dileshkumar Solanki mkazi
wa wa jijini Dar es Salaam akiibuka mshindi na hivyo kujishindia gari
ndogo aina ya Toyota IST.
Kampeni
hiyo ilizinduliwa mwezi Mei mwaka huu ambapo kupitia kampeni hiyo benki
hiyo imekua ikitoa zawadi mbalimbali za kila mwezi zikiwemo simu aina
ya iPhone 6 kwa wateja waliobahatika kuibuka washindi kutoka maeneo
mbalimbali hapa nchini.
Akizungumza
kwenye hafla fupi ya uendeshaji wa droo hiyo iliyofanyika mwishoni mwa
wiki kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, Meneja
Bidhaa wa benki hiyo Bw Aloyse Maro alisema benki hiyo imeridhishwa na
mwitikio mkubwa kutoka kwa wateja wake wakati wote wa kampeni hiyo
inayolenga kuhamasisha utamaduni wa kuweka akiba miongoni mwa
watanzania.
“Kampeni
hii imekuwa ni yenye mafanikio. Imepokelewa kwa mwamko mkubwa kutoka
kwa wateja wetu hatua ambayo tumeitafsiri kwamba ni wazi wateja wetu
wananufaika na wanafurahia huduma zetu,’’ alisema Bw Maro muda mfupi
baada ya kufanyika kwa droo hiyo iliyosimamiwa na Bodi ya taifa michezo
ya kubahatisha nchini (GBT)
Bw.
Maro aliongeza kuwa sambamba na zawadi hizo kampeni hiyo inaambatana na
utoaji wa riba nzuri zaidi kwa wateja wanaofungua akaunti hiyo ya
malengo.
“Hatujaishia
tu kwenye kutoa zawadi hizi kwenye kampeni hii bali tulihusisha pia
utoaji wa riba nzuri zaidi kwa wateja wanaofungua akaunti yetu ya
malengo,’’ alibainisha.
0 comments:
Post a Comment