Meneja
Mawasiliano na Mahusiano wa Efm Radio, Denis Ssebo akizungumza na
wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya wasanii zaidi ya 50 wa Bongo
Movie akiwamo Steve Nyerere, Wema Sepetu na Vicent Kigosi (Rey)
wataungana na kituo cha redio cha EFM na Benki ya DTB kufanya usafi
Desema 9 mwaka huu. Usafi huo utaanzia katika barabara ya Morocco hadi
Magomeni, mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni
Mkuu wa Bidhaa na Masoko wa benki ya Diamond Trust Bank (DTB), Sylvester
Bahati.
Mkuu
wa Bidhaa na Masoko wa benki ya Diamond Trust Bank (DTB), Sylvester
Bahati akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya usafi
ni nguzo moja wapo katika benki hiyo na si kwa ajili ya agizo la Rais
John magufuli bali ni zoezi endelevu, kulia ni Meneja Mawasiliano na
Mahusiano wa Efm Radio, Denis Ssebo.
Wandishi
wa habari wakimsikiliza Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Efm Radio,
Denis Ssebo, mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii.
WASANII wa
Bongo Movie zaidi
ya 50 akiwamo Steve Nyerere, Wema Sepetu na Vicent Kigosi (Rey)
wataungana na kituo cha redio cha EFM na Benki ya DTB kufanya usafi
Disemba 9 mwaka huu.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa EFM,
Denis Ssebo, amesema usafi huo utaanzia katika barabara ya Morocco hadi
Magomeni.
Ssebo
amesema katika usafi huo EFM, DTB pamoja na wasanii hao watashirikiana
na viongozi mbalimbali walioko madarakani pamoja na wakazi wa Kinondoni
chini ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.
Kauli
mbiu ya siku hoyo isemayo ‘Naona aibu kuishi na uchafu’ huku tukiunga
kauli mbiu ya kinondoni ‘Usafi uanze na mimi’ endapo kila mmoja
atatambua umuhimu wa usafi wake, mazingira yake tutaweza kwa pamoja
kulimaliza tatizo la uchafu nchini,”amesema Ssebo.
Kwa
upande wake mwakilishi wa DTB Silvesta Bahati alisema usafi ni nguzo
moja wapo katika benki hiyo na si kwa ajili ya agizo la Rais John
magufuli bali ni zoezi endelevu.
0 comments:
Post a Comment