Pages

Ads 468x60px

Friday, November 13, 2015

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU ASHIRIKI MSIBA WA MJUKUU WA RAIS MAGUFULI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisaini kwenye Kitabu cha maombolezo ya msiba wa Mjukuu wa Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, Maryfaustna Mlyambina, aliyefariki Nov 11, 2015. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu zilifanyika leo Nov 13, 2015 Kimara jijini Dar es Salaam, na baadaye msiba huo kusafirishwa kuelekea Mkoani Mwanza kwa maziko.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais John Magufuli, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo Nov 13, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimfariji Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu Maryfaustna Mlyambina zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo. Marehemu ni mjukuu wa Mhe Rais. 
Wazazi wa marehemu wakiwa na baadhi ya wanafamilia, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu.
Rais Dkt. John Magufuli (wa tatu kuli) Makamu wake (wa Nne kulia) Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Mke wa Rais,Mama Janeth Magufuli (kulia) na Mke wa Rais Mstaafu, Mama Salma Kikwete (kushoto) wakishiriki ibada maalum ya kumuombea marehemu wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika Kimara jijini Dar es Salaam, leo Nov 13, 2015.


Sehemu ya wanafamilia ya wafiwa katika ibada hiyo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais John Magufuli, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo Nov 13, 2015.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo Nov 13, 2015.
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais John Magufuli, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo Nov 13, 2015.
Baadhi ya kinamama wakibeba Jeneza lenye mwili wa marehemu Mjukuu wa Rais Dkt. John Magufuli, baada ya shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Kimara, jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Mama mzazi wa marehemu na baadhi ya wanafamilia wafiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wakati aliposindikiza msiba wa mjukuu wa Mhe. Rais, marehemu Maryfaustna Mlyambina, leo Nov 13, 2015.

WADAU WA AFYA MKOANI MBEYA WAKUTANA NA KUJADILIANA KUELEKEA SIKU YA MAADHIMISHO YA UKIMWI DUNIANI


Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa wa Mbeya Ndugu Stellah Kategile akiwasilisha maada kwa wadau wa Sekta ya Afya Mkoani Mbeya katika kikao cha kujadili juu ya kuelekea katika siku ya maadhimisho ya Ukimwi Duniani Tarehe 1 Desemba mwaka huu.
Mratibu wa kudhibiti Ukimwi Mkoani Mbeya (RACC-Regional AIDS Control Coodinator ) Dkt Francis Philly akizungumza katika kikao hicho ambacho kimehudhuriwa na wadau mbalimbali wa masuala ya afya mkoani  katika ukumbi wa Cofee Garden jijini Mbeya.
Mrakibu wa Polisi Mkuu  dawati la jinsi na watoto Mkoa wa mbeya Ndugu Debora Mrema akielezea masuala mbaliimbali  yanayolikumba Dawati hilo katika kupambana na ukatili wa kijinsi Mkoani humo huku akisisitiza juu ya wadau kujitokeza na kutoa michango yao ya kifedha sanjali na rasilimali nyingine ili kuweza kutoa elimu kwa jamii katika maeneo mbalimbali mkoani humo hususani maeneo ya vijijini.
Wadau wakiendelea na majadiliano katika mkutano huo.

JK ATINGA OFISINI KWAKE LUMUMBA AANZA KUPIGA MZIGO FASTA

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Mohamed Seif Khatib mara baada ya kuwasili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi,Ofisi Ndogo Lumumba.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu wa Sekretarieti Ndugu Anamringi Macha mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za CCM Lumumba.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wapenzi na wanachama wa CCM waliojitokeza kumpokea kwenye Makao Makuu ya Chama Ofisi Ndogo Lumumba.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisani kitabu cha wageni mara baada ya kuingia kwenye ofisi yake,waliosimama ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Mohamed Seif Khatib (kulia) na Naibu Katibu Mkuu CCM (Bara) Ndugu Rajab Luhwavi.

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA, JIJINI DAR

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. John Mngodo akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Kamishna Jenerali wa Magereza alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Novemba 13, 2015.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa taarifa fupi ya Hali ya Magereza nchini kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. John Mngodo(katikati). Naibu Katibu Mkuu  yupo katika ziara ya kikazi katika Idara mbalimbali zinazounda Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi(wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Stephen Pancras.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. John Mngodo akiongea na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani). Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja.

RC KILIMANJARO,AMOSI MAKALA AKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI KUZUNGUMZIA TISHIO LA UGONJWA WA KIPINDUPINDU.


Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala akizungumza nawanahabari pamoja na Waganga wakuu wa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro juu ya tishio la ugonjwa hatari wa Kipindupindu.
Baadhi ya Waganga wakuu wa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Amos Makala

SITOGOMBEA NAFASI YA USPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA-ANNE MAKINDA



Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa ofisi ndogo za Bunge  jijini Dar es Salaam kuhusiana na kuachana na uongozi katika siasa.

ALIYEKUWA Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda amejing'atua rasmi na kuachana na  uongozi katika siasa kutokana na kufanya kazi za Siasa kwa miaka 40.

ameyasema hayo alipokua akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam leo.

Anne amesema kuwa "Sitagombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  wala sitachukua fomu ya kugombea nafasi ya uspika wala sifikilii kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Uspika"

Aidha Anne amesema kuwa katika awamu yake ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kulikuwa na changamoto nyingi kutokana na kuwepo na wabunge vijana.

Hata hivyo kuwa na changamoto nyingi ila amesema kuwa alilifurahiya sana Bunge hilo kutokana na kuwaelewa wabunge mbalimbali tabia zao hasa wakiwa Bungeni.

Anne amepsema kuwa Spika wa sasa atakaye shinda nafasi awe si mwepesi wa kukasirika kutokana na changamoto atakazo zipata Bungeni wakati wakijadilia masuala mbalimbali ya Serikali, pia awe mtulivu na kukabiliana na changamoto zitakazo jitokeza.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kuzungumza nao leo katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA IDARA YA UHAMIAJI KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM – AWATAKA WATENDAJI KWENDA NA KASI MPYA

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (kushoto), akisalimiana na Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha), Piniel Mgonja , wakati wa  ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji,Kurasini jijini Dar es Salaam.  Wa kwanza kushoto ni Kamishna Jenerali  wa Uhamiaji, Sylvester  Ambokile.
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester  Ambokile (kushoto), akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, baadhi ya Ofisi za Idara ya Uhamiaji, wakati Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara katika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (mwenye tai),akipewa maelezo alipotembelea Dawati la Mapokezi wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji,Kurasini, jijijni Dar es Salaam.
 Afisa Uhamiaji, Lilian Maleko akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (mwenye tai), jinsi  taarifa za muombaji pasi ya kusafiria zinavyohakikiwa, wakati wa ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam.

BARAZA KUU LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA LAIJADILI BURUNDI


Matthew Rycroft, Mwakilishi wa Kudumu wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa na Rais wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa,  kwa mwezi  Novemba, akizungumza na waandishi wa habari   hawapo pichani, mara baada ya  Baraza Kuu la Usalama kumaliza kikao chake kilichojadili hali ya  Burundi, kikao ambacho pia kilipitisha azimio ambalo pamoja na mambo mengine linamuunga mkono  Rais wa Uganda  Yoweri Museven ambaye aliteuliwa na  Viongozi  wenzie wa Jumuiya ya Afrika  Mashariki kuwa msimamizi na mwezeshaji wa majadiliano  kati ya pande zinazopinga  nchini Burundi.
 
Na Mwandishi Maalum, New York
BARAZA Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa  limelaani vikali  hali ya  kuendelea kwa matukio ya mauaji, utesaji na vitendo vingine vya  vinavyokiuka haki za binadamu nchini  Burundi.

Pamoja na kukemea hali hiyo,  Baraza Kuu la Usalama  limeeleza  kusudio la kuchukua hatua zaidi kwa nchi hiyo ya  Burundi.  Pamoja na  kumwomba  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, katika kipindi cha siku  kumi na tano awasilishe mbele ya Baraza hilo taarifa kuhusu  uwepo wa Umoja wa Mataifa nchini  Burundi katika siku za baadaye. 

Jana ( Alhamisi) Baraza hilo  lilikutana katika kikao chake cha 7557   ajenda  ilikuwa ni Burundi ambapo,   Baraza kwa kauli moja  lilipitisha Azimio namba 2248 (2015). Kupitia  Azimio hilo, Baraza limetoa wito kwa  pande zote nchini Burundi kujiepusha na kukataa   fujo ikiwa ni pamoja na kujiepusha na vitendo vyovyote  vinavyoweza kutishia Amani na  utulivu wa taifa hilo.

Vile  Vile Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo kwa mwezi huu wa  Novemba  Rais wake ni Uingereza limekema vikali kauli za  uchochezi zinazotolewa na baadhi ya  watu ndani na nje ya Burundi, kauli  ambazo kwa mujibu wa Baraza hilo zinalenga katika kushawishi chuki baina ya  makundi ya watu  nchini humo.

 Kufuatia  kauli hizo za uchochezi,  Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa,  limeitaka Serikali ya Burundi kuheshimu, kulinda na kuhakikisha haki za binadamu na  misingi ya uhuru,  kuheshimu utawala wa sheria pamoja na uwajibikaji wa uwazi dhidi ya   fujo na  itoe ushirikiano kwa  Ofisi ya Kamisheni ya Haki za Binadamu.

  Kupitia  Azimio hilo  Baraza Kuu pia  limeitaka serikali ya Burundi kuwawajibisha wale wote watakaopatikana na hatia  ya ukiukwaji ya Sheria ya Kimataifa ya haki za binadamu na unyanyasajji wa haki za binadamu.

Aidha  kupitia  Azimio hilo,  Baraza Kuu la Usalama limetoa wito kwa Serikali ya  Burundi kutoa ushirikiano katika majadiliano yanayoongozwa na Jumuiya ya Afrika  Mashariki  na ambayo yameridhiwa na Umoja wa Afrika na limetaka  kuitishwa haraka majadiliano yatakayokuwa jumuishi yakiwashirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya Burundi  ili kutafuta muafaka utakaokubaliwa na pande zote.

Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa pia kupitia Azimio hilo limesema linamuunga mkono kwa nguvu zote  mwezeshaji wa  majadiliano hayo  ambaye ni Rais Yower Museveni wa Uganda aliyeteuliwa na  Viongozi wa Jumuiya ya Afrika  Mashariki.

 Katika kusaidia  mchakato wa majadiliano hayo, Baraza Kuu la Usalama  la Umoja wa Mataifa limemkaribisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  kupeleka  timu  ya wataalam ambao kwa kushirikiana  na Serikali, Umoja wa Afrika na wadau wengine watabuni   mbinu  za  kushughulikia matatizo ya kisiasa na kiusalama.

KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MITARO NA MAENEO YALIYOATHILIWA NA KIPINDUPINDU JIJINI DAR

Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Mbazi Msuya (wa katika) akieleza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki (wa kwanza kushoto) na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka (wa kwanza kulia) wakati wa ziara ya kukagua mtaro uliojengwa eneo la Buguruni kwa Mnyamani.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka (wa kwanza kulia mwenye miwani) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki wakiangalia hali ya daraja la Buguruni Visiwani walipofanya ziara ya maeneo yaliyoathiriwa na ugonjwa wa kipindupindu.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AKABIDHIWA RASMI OFISI NA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA NNE DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE LEO IKULU, DAR ES SALAAM

 Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais leo Novemba 12, 2015
  Rais Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono kwa furaha na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais
  Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Obeni Sefue alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais
   Rais Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza  Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
  Rais Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza  Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakati akiongea kabla ya kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais  Ikulu jijini Dar es salaam 
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akipokea kwa furaha hati ya makabadhiano ya Ofisi kutoka kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2015

Rais Dkt John Pombe Magufuli akipokea kwa furaha hati ya makabadhiano ya Ofisi kutoka kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2015
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akiiangalia kwa furaha hati ya makabadhiano ya Ofisi aliyoipokea kutoka kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2015
 Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Makiamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu Kiongozi  baada ya hafla ya makabidhiano rasmi ya Ofisi  Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi leo Novemba 12, 2015
Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Makiamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan baada ya hafla ya makabidhiano rasmi ya Ofisi  Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi leo Novemba 12, 2015.
 
Blogger Templates