Aliyekuwa
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda 
akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa ofisi ndogo za 
Bunge  jijini Dar es Salaam kuhusiana na kuachana na uongozi katika 
siasa.
ALIYEKUWA 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda 
amejing'atua rasmi na kuachana na  uongozi katika siasa kutokana na 
kufanya kazi za Siasa kwa miaka 40.
ameyasema hayo alipokua akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam leo.
Anne 
amesema kuwa "Sitagombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya 
Muungano wa Tanzania  wala sitachukua fomu ya kugombea nafasi ya uspika 
wala sifikilii kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Uspika"
Aidha 
Anne amesema kuwa katika awamu yake ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya 
muungano wa Tanzania kulikuwa na changamoto nyingi kutokana na kuwepo na
 wabunge vijana.
Hata 
hivyo kuwa na changamoto nyingi ila amesema kuwa alilifurahiya sana 
Bunge hilo kutokana na kuwaelewa wabunge mbalimbali tabia zao hasa 
wakiwa Bungeni.
Anne 
amepsema kuwa Spika wa sasa atakaye shinda nafasi awe si mwepesi wa 
kukasirika kutokana na changamoto atakazo zipata Bungeni wakati 
wakijadilia masuala mbalimbali ya Serikali, pia awe mtulivu na 
kukabiliana na changamoto zitakazo jitokeza.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
 
 
 
 
 
 



 
 
0 comments:
Post a Comment