Matthew
 Rycroft, Mwakilishi wa Kudumu wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa na 
Rais wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa,  kwa mwezi  Novemba, 
akizungumza na waandishi wa habari   hawapo pichani, mara baada ya 
 Baraza Kuu la Usalama kumaliza kikao chake kilichojadili hali ya 
 Burundi, kikao ambacho pia kilipitisha azimio ambalo pamoja na mambo 
mengine linamuunga mkono  Rais wa Uganda  Yoweri Museven ambaye 
aliteuliwa na  Viongozi  wenzie wa Jumuiya ya Afrika  Mashariki kuwa 
msimamizi na mwezeshaji wa majadiliano  kati ya pande zinazopinga 
 nchini Burundi.
Na Mwandishi Maalum, New York
BARAZA Kuu
 la Usalama la Umoja wa Mataifa  limelaani vikali  hali ya  kuendelea 
kwa matukio ya mauaji, utesaji na vitendo vingine vya  vinavyokiuka haki
 za binadamu nchini  Burundi.
Pamoja
 na kukemea hali hiyo,  Baraza Kuu la Usalama  limeeleza  kusudio la 
kuchukua hatua zaidi kwa nchi hiyo ya  Burundi.  Pamoja na  kumwomba 
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, katika kipindi cha siku  kumi na tano 
awasilishe mbele ya Baraza hilo taarifa kuhusu  uwepo wa Umoja wa 
Mataifa nchini  Burundi katika siku za baadaye. 
Jana
 ( Alhamisi) Baraza hilo  lilikutana katika kikao chake cha 7557   
ajenda  ilikuwa ni Burundi ambapo,   Baraza kwa kauli moja  lilipitisha 
Azimio namba 2248 (2015). Kupitia  Azimio hilo, Baraza limetoa wito kwa 
 pande zote nchini Burundi kujiepusha na kukataa   fujo ikiwa ni pamoja 
na kujiepusha na vitendo vyovyote  vinavyoweza kutishia Amani na 
 utulivu wa taifa hilo.
Vile
  Vile Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo kwa mwezi huu wa
  Novemba  Rais wake ni Uingereza limekema vikali kauli za  uchochezi 
zinazotolewa na baadhi ya  watu ndani na nje ya Burundi, kauli  ambazo 
kwa mujibu wa Baraza hilo zinalenga katika kushawishi chuki baina ya 
 makundi ya watu  nchini humo.
 Kufuatia
  kauli hizo za uchochezi,  Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, 
 limeitaka Serikali ya Burundi kuheshimu, kulinda na kuhakikisha haki za
 binadamu na  misingi ya uhuru,  kuheshimu utawala wa sheria pamoja na 
uwajibikaji wa uwazi dhidi ya   fujo na  itoe ushirikiano kwa  Ofisi ya 
Kamisheni ya Haki za Binadamu.
 
 Kupitia  Azimio hilo  Baraza Kuu pia  limeitaka serikali ya Burundi 
kuwawajibisha wale wote watakaopatikana na hatia  ya ukiukwaji ya Sheria
 ya Kimataifa ya haki za binadamu na unyanyasajji wa haki za binadamu.
Aidha
  kupitia  Azimio hilo,  Baraza Kuu la Usalama limetoa wito kwa Serikali
 ya  Burundi kutoa ushirikiano katika majadiliano yanayoongozwa na 
Jumuiya ya Afrika  Mashariki  na ambayo yameridhiwa na Umoja wa Afrika 
na limetaka  kuitishwa haraka majadiliano yatakayokuwa jumuishi 
yakiwashirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya Burundi  ili 
kutafuta muafaka utakaokubaliwa na pande zote.
Baraza
 Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa pia kupitia Azimio hilo limesema 
linamuunga mkono kwa nguvu zote  mwezeshaji wa  majadiliano hayo  ambaye
 ni Rais Yower Museveni wa Uganda aliyeteuliwa na  Viongozi wa Jumuiya 
ya Afrika  Mashariki.
 Katika
 kusaidia  mchakato wa majadiliano hayo, Baraza Kuu la Usalama  la Umoja
 wa Mataifa limemkaribisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  kupeleka 
 timu  ya wataalam ambao kwa kushirikiana  na Serikali, Umoja wa Afrika 
na wadau wengine watabuni   mbinu  za  kushughulikia matatizo ya kisiasa
 na kiusalama.
 
 
 
 
 
 

 
 
0 comments:
Post a Comment