Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, 
akisaini kwenye Kitabu cha maombolezo ya msiba wa Mjukuu wa Mhe. Rais 
Dkt. John Magufuli, Maryfaustna Mlyambina, aliyefariki Nov 11, 2015. 
Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu zilifanyika leo Nov 13, 2015 Kimara
 jijini Dar es Salaam, na baadaye msiba huo kusafirishwa kuelekea Mkoani
 Mwanza kwa maziko.
Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, 
akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe 
Rais John Magufuli, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli 
za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo Nov 13, 2015.
Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, 
akimfariji Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, wakati wa shughuli za kuaga 
mwili wa marehemu Maryfaustna Mlyambina zilizofanyika Kimara jijini Dar 
es Dalaam,leo. Marehemu ni mjukuu wa Mhe Rais. 
Wazazi wa marehemu wakiwa na baadhi ya wanafamilia, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu.
Rais 
Dkt. John Magufuli (wa tatu kuli) Makamu wake (wa Nne kulia) Rais 
Mstaafu Jakaya Kikwete, Mke wa Rais,Mama Janeth Magufuli (kulia) na Mke 
wa Rais Mstaafu, Mama Salma Kikwete (kushoto) wakishiriki ibada maalum 
ya kumuombea marehemu wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika 
Kimara jijini Dar es Salaam, leo Nov 13, 2015.
Sehemu ya wanafamilia ya wafiwa katika ibada hiyo.
 Rais 
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, akitoa heshima 
za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais John 
Magufuli, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga 
zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo Nov 13, 2015.
Mke wa
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli, akitoa 
heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais, 
marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga 
zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo Nov 13, 2015.
Rais 
Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, akitoa heshima za mwisho 
mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais John Magufuli, 
marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga 
zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo Nov 13, 2015.
Baadhi
 ya kinamama wakibeba Jeneza lenye mwili wa marehemu Mjukuu wa Rais Dkt.
 John Magufuli, baada ya shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo 
Kimara, jijini Dar es Salaam.
 Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, 
akiagana na Mama mzazi wa marehemu na baadhi ya wanafamilia wafiwa 
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wakati aliposindikiza 
msiba wa mjukuu wa Mhe. Rais, marehemu Maryfaustna Mlyambina, leo Nov 
13, 2015. 
 
 
 
 
 
 












 
 
0 comments:
Post a Comment