Shabiki wa Msanii Vanessa Mdee akiwa kwenye pozi la Red Carpet wakati
wa Tamasha la “Trust Divas Only” ambalo lilifanyika katika hoteli ya
Malaika Beach Resort jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo
ambalo ni maalum kwa ajili ya akina dada ni mahususi kwa ajili ya utoaji
elimu ya afya ya uzazi na maendeleo yao ya baadae.
Msanii wa Bongo fleva Vanessa Mdee, akipiga picha na baadhi ya
mashabiki wake wakati wa Tamasha la “Divas only” ambalo ni mahusisi kwa
ajili ya kuwaelimisha madiva mbalimbali kuhusu elimu ya afya ya uzazi.
Tamasha hilo la mwisho lilifanyika katika ukumbi wa Malaika Beach Resort
jijini Mwanza baada ya kuzunguka katika majiji ya Dodoma na Mbeya
katika wiki zilizopita.
Msanii wa Bongo fleva Vanessa Mdee akiwa kwenye picha ya pamoja na
wafanyakazi wa TRUST wakati wa Tamasha la “Divas only” ambalo ni
mahusisi kwa ajili ya kuwaelimisha akina dada kuhusu elimu ya afya ya
uzazi. Tamasha hilo lilifanyika katika ukumbi wa Malaika Beach Resort
jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Wafanyakazi wa TRUST wanaohusika na mpango wa kuelimisha wasichana
juu ya elimu ya uzazi wakiwa jukwaani tayari kwa kufungua Tamasha la
“Divas Only” kwa kucheza muziki. Tamasha hilo lilifanyika katika ukumbi
wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Madiva mbalimbali wakijiandikisha wakati wa ufunguzi wa Tamasha la
“Divas Only”ambalo lilikuwa maalum kwa ajili ya kuwaelimisha akina dada
juu ya afya ya uzazi na maendeleo yao ya baadae. Tamasha hilo ambalo
lilipambwa vilivyo na burudani toka kwa Msanii Vanessa Mdee lilifanyika
mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza.
Msanii
wa Bongo fleva Vanessa Mdee akitumbuiza kwenye Tamasha la “Trust Divas
Only” lililofanyika katika hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza
mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo ni maalum kwa ajili ya kina dada na
limekua likitoa elimu juu ya afya ya uzazi na maendeleo ya baadae ya
madiva hao tokea uzinduzi wa mfululizo wa matamasha hayo jijini Dodoma
wiki mbili zilizopita.
TAMASHA la “Trust Divas only” limefunga pazia lake rasmi usiku wa
kuamkia leo katika ukumbi wa Malaika Beach resort uliopo pembezoni mwa
ziwa Victoria jijini Mwanza. Wakazi na madiva wa mkoa huo walijitokeza
kwa wingi kushuhudia Tamasha hilo la mwisho na la aina yake lakini
kikubwa zaidi kupata elimu na hamasa juu ya uzazi wa mpango na mambo
yanayowahusu wakina dada katika kupanga maendeleo yao ya baadae.
Aliyelipamba Tamasha hilo si mwingine bali ni diva wa nguvu na msanii
wa kizazi kipya Vanessa Mdee ambaye tokea awali amekua akishirikiana na
Trust katika mfululizo wa matamasha hayo yaliyoanza rasmi wiki mbili
zilizopita jijini Dodoma.
Mara baada ya kupanda jukwaani na kuporomosha burudani ya nguvu
Vanessa alionekana kushangiliwa kila kona na madiva hao waliokuwa
wakiimba sambamba na msanii huyo ambae alifanikiwa kukata kiu ya madiva
wengi wa mkoa huo waliojitokeza kwa wingi kushuhudia burudani yake.
Mfululizo wa matamasha hayo ya Trust ambayo ni chapa ya njia za
kisasa za uzazi wa mpango zenye kuaminika pamoja na bidhaa na huduma za
maisha na urembo zinazotengenezwa kwa ajili ya wanawake yamefikia tamati
baada ya kuzunguka kwa muda wa wiki tatu kwenye miji mitatu tofauti ili
kuhamasisha madiva mbalimbali wajipange kwa ajili ya mafanikio yao ya
baadae. Trust ipo katika kumsaidia diva wakati wote wa safari hii.
“Ni furaha yangu kubwa kuwa tumeweza kukamilisha zoezi hili kwa
ufanisi mkubwa tangu tulipozindua matamasha haya jijini Dodoma”… alisema
Meneja Masoko wa Trust Sialouise Shayo.
Bi. Shayo aliongeza kuwa katika zoezi zima wamefanikiwa kuwafikia
madiva lukuki katika mikoa yote mitatu waliyoitembelea ambapo kwa pamoja
wameweza kufurahi, kuelimishana na kujifunza kutoka kwa wataalamu mambo
mbalimbali zikiwemo njia nyingi bora za uzazi wa mpango kama njia ya
kitanzi ambayo ni bora sana na ina ufanisi wa zaidi ya asilimia 99.9.
Kama wewe ni Diva wa Trust ama unataka kujua Trust inahusu nini,
Tutafute kupitia ofisi zetu zinazopatikana Dodoma, Mbeya na Mwanza au
kwa kupitia tovuti yetu (trustlife.co.tz) na ututembelee leo.
0 comments:
Post a Comment