Mkazi
 wa eneo la Duluti wilayani Arumeru mkoani Arusha, Juma Isangu akiwa na 
mkewe Janet Tinai pamoja na mwanao, Issa Juma (katikati) wakiangalia 
nyaraka mbalimbali nje ya nyumba yao mara baada ya kufukuzwa na kisha 
kuvunjiwa nyumba yao wilayani humo na kampuni ya Majembe Auction Mart 
kwa amri ya mahakama.
Mkazi
 wa eneo la Duluti wilayani Arumeru mkoani Arusha, Janet Tinai 
akilalamika mbele ya waandishi wa habari akiwa na baadhi ya vyombo vyake
  mara baada ya kuhamishwa kwa amri ya mahakama na kampuni ya Majembe 
Auction Mart.
 Mkazi
 wa eneo la Duluti wilayani Arumeru mkoani Arusha, Juma Isangu akiwa na 
mkewe, Janet Tinai wakitafakari nje ya nyumba yao mara baada ya 
kuhamishwa na kisha kuvunjiwa nyumba yao na kampuni ya Majembe Auction 
Mart kwa amri ya mahakama.
(Picha na moses mashalla).
Mahmoud Ahmad.
SERIKALI
 imeombwa kuingilia kati sakata la familia ya Juma Isangu mkazi wa eneo 
la Duluti wilayani Arumeru mkoani Arusha kuondolewa na kisha kuvunjiwa 
nyumba waliyokuwa wakiishi kwa amri ya mahakama kwa madai haki 
haikutendeka.
Familia
 hiyo iliondolewa juzi majira ya saa 6:30 mchana na kampuni ya udalali 
wa mahakama ya Majembe Auction Mart Ltd  tawi la Arusha kwa madai kwamba
 waliagizwa na msimamizi wa mirathi wa nyumba hiyo aitwaye,Janeth 
Fosbrooke kuwaondoa  kwa kuwa hawastahili kuwepo ndani yake.
Akizungumza
 mbele ya waandishi wa habari waliofika katika eneo hilo, Isangu akiwa 
na mkewe, Janet Tinai pamoja na mtoto wao wa kiume, Issa Juma alisema 
alisema kwamba kwa sasa hawaelewi ni wapi wataishi kwa kuwa kitendo cha 
kuondolewa katika nyumba hiyo na kisha kutupiwa virago hakikufuata 
sheria.
Alisema
 kwamba wameondolewa kinyemela ndani ya nyumba waliyokuwa wakiishi bila 
taarifa ingawa  hapo awali waliwahi kushinda kesi ya mgogoro wa nyumba 
hiyo nambari 33 ya mwaka 2011 iliyofunguliwa katika mahakama ya ardhi.
Akielezea
 tukio hilo Tinai alisema kwamba mnamo juzi majira ya saa 6;30 mchana 
watu wapatao sita ambao walijitambulisha kwamba ni madalali  wa mahakama
 kutoka kampuni ya Majembe Auction Mart walifika katika nyumba 
wanayoishi wakiambatana na askari wa jeshi la polisi na kuwataka kutoka 
nje ya nyumba hiyo.
Tinai,alisema
 kwamba wakiwa wanajiuliza ndipo watu hao waliingia ndani na kisha 
kuanza kutoa baadhi ya mali mbalimbali na kisha kuzipeleka ndani ya lori
 mojawapo lililokuwa limeegeshwa nje ya nyumba hiyo na kuacha baadhi ya 
vitu nje ya  eneo la nyumba hiyo.
Alisema
 kwamba na mara walipohoji walijibiwa ya kwamba hawakutakiwa kuendelea 
kuishi ndani ya nyumba hiyo kwa kuwa kuna  amri kutoka mahakama kuu 
inayowataka kuondoka mara moja ndani ya nyumba hiyo .
Hatahivyo,
 kwa nyakati tofaiti wanafamilia hao walisema kwamba nyumba hiyo ni 
halali kwa kuwa walipewa na marehemu Henry Fosbrooke ambaye alikuwa 
mmiliki halali wa eneo hilo  tangu mwaka  1980 ambaye aliacha wosia 
waliuwasilisha mbele ya mahakama kuu kanda ya Arusha kama moja ya 
vielelezo na kisha kukubaliwa.
Hatahivyo,Mwenyekiti
 wa kitongoji cha Duluti,Elias Kaaya akihojiwa na waandishi wa habari 
katika eneo la tukio alisema kwamba hivi karibuni baadhi ya watu ambao 
walijitambulisha kwamba ni madalali wa mahakama kutoka  kampuni ya 
Majembe Auction Mart walifika ofisini kwao na kuwapa taarifa kuwa 
wataendesha zoezi la kumtoa mpangaji aitwaye,Isangu kwenye kitongoji 
chake.
Huku
 akionyesha barua ya mnamo Novemba 11 mwaka huu yenye KUMB 
No,REF.NO.MAM/ARJHF/10/2015  mwenyekiti huyo alidai kwamba watu hao 
waliomba uwepo wa usimamizi kutoka ofisi yake kumtoa mkazi huyo na kudai
 waliwasilisha pia taarifa kwake na jeshi la polisi wilayani Arumeru.
“Majembe
 Auction Mart Ltd madalali ya baraza la ardhi na nyumba (court blockers)
 ukiwa msimamizi wa amani kwenye kata yako ya Akheri tunakuomba uwepo 
katika zoezi la kumhamisha/kumtoa mpangaji ndugu Juma Isangu aliyekuwa 
amepangishwa na marehemu Henry Albert Fosbrooke ambapo kwa sasa 
msimamizi wa mirathi aliyeteuliwa m/s Janeth Fosbrooke ndiye ametuteua 
kutekeleza zoezi hili la kumtoa mpangaji kwenye nyumba”ilisema sehemu ya
 barua hiyo
Hatahivyo,
 msimamizi wa mirathi wa nyumba hiyo, Fosbrooke hakuweza kupatikana 
kuzungumzia tukio hilo lakini msimamizi wa  kampuni ya Majembe Auction 
Mart Ltd tawi la Arusha, Suleiman Mdoe alisema ya kwamba wao walifuata 
taratibu zote kabla ya kuwahamisha wakazi hao ikiwa ni pamoja na 
kubandika notisi ya siku 44 kabla ya zoezi kufanyika.
 
 
 
 
 
 



 
 
0 comments:
Post a Comment