Mkurugenzi wa Idara ya
Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Aloyce Msigwa (kushoto) akifungua
kikao kilichowakutanisha watumishi wa
Ofisi ya Rais-Utumishi, na Taasisi zake katika hafla fupi ya kuwapokea Katibu
Mkuu mteule Bw. HAB Mkwizu (wa pili kutoka kushoto) na Naibu Katibu Mkuu mteule
Bw. Tixon Nzunda (wa pili kutoka kulia).
Naibu Katibu Mkuu Bw. Tixon
Nzunda (aliyesimama) akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi katika hafla
fupi, iliyowakutanisha watumishi wote, wa kwanza kutoka kushoto ni Katibu Mkuu
Bw. HAB Mkwizu.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala katika Utumishi wa Umma, Ofisi
ya Rais-Utumishi Bw. Nyakimura M. Muhoji akizungumza kwa niaba ya watumishi wa
Ofisi ya Rais-utumishi wakati wa hafla fupi ya kuwapokea viongozi walioteuliwa
kuongoza Utumishi.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais- Utumishi Bw. HAB Mkwizu
akizungumza na na watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi katika hafla
iliyowakutanisha watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.
Viongozi wa Ofisi ya
Rais-Utumishi, na Menejimenti katika picha ya pamoja.
Viongozi wa Ofisi ya
Rais-Utumishi pamoja na watumishi wa Idara ya Ukuzaji Maadili katika picha ya
pamoja, Naibu Katibu Mkuu-Utumishi Bw. Nzunda aliwahi kuwa Afisa katika Idara
ya Ukuzaji Maadili.
0 comments:
Post a Comment