Kaimu mkuu wa mkoa wa Mtwara ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Mtwara Bi. Fatma Ally akikagua wodi ya watoto katika hospitali ya mkoa na rufaa ya Ligula mkoani Mtwara ambayo benki ya Ecobank Tanzania ilijitolea kukikarabati wakati wa hafla ya kuadhimisha siku ya Ecobank ambayo ilifanyika mkoani humo mwishoni mwa juma.
Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Enoch Osei-Safo akitoa hotuba yake kwa wakazi wa mkoa wa mtwara katika hafla ya kuadhimisha siku ya Ecobank ambayo ilifanyika mkoani Mtwara kitaifa mwishoni mwa juma. Benki ya Eco Tanzania ilisherekea siku hii kwa kukarabati moja ya wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya Ligula mkoani Mtwara ambapo walichangia kiasi cha dola za kimarekani elfu kumi na tano.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Mtwara ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Mtwara Bi. Fatma Ally (katikati) akiwasili kwenye hafla ya kuadhimisha siku ya Ecobank ambayo ilifanyika mkoani Mtwara kitaifa. Katika kusherekea siku hii, wafanyakazi wa benki hii barani Afrika huhamasishwa kujitolea muda wao kwa ajili ya shughuli za kijamii zenye manufaa kwa jamii husika. Ecobank Tanzania ilisherekea siku hii kwa kukarabati moja ya wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya Ligula mkoani Mtwara.
0 comments:
Post a Comment