Katibu
 wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiongea na waandishi wa habari 
mara baada ya Wabunge wa CCM kupitisha jisha la Spika.
Katibu wa NEC (CCM) Itikadi na Uenezi ambaye pia ni mbunge wa Mtama, Nape Nnauye alisema “Kamati ya Wabunge wote wa CCM imekamilisha kazi yake ya kwanza kuchambua na kupitisha moja kati ya majina matatu yaliyoteuliwa na Kamati Kuu.
“Kama tulivyoona wagombea wawili walijitoa, hivyo Job Ndugai
amepitishwa kwa kauli moja kugombea nafasi ya uspika. Tunamuombea kura kwa
sababu sifa zote anazo, bila shaka hakutatokea mgombea wa upinzani atakayezidi
sifa zake,” alisema Nape.
Mbunge
 wa Jimbo la Kongwa Ndugu Job Ndugai akiongea na waandishi wa habari nje
 ya ukumbi wa NEC baada ya jina lake kupitishwa na wabunge wa CCM.
Katibu Mkuu wa CCM akihutubia kwenye kikao maalum cha wabunge wa CCM kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma.
Katibu
 Mkuu wa CCM akipokea pongezi alizopewa na wabunge wa CCM kwa kazi nzuri
 iliyowapa CCM ushindi mkubwa katika uchaguzi uliofanyika oktoba 2015.
Sehemu ya wabunge wa CCM walioshiriki kwenye kikao maalum cha uchaguzi wa Spika kutoka Chama Cha Mapinduzi.
Mbunge
 Mteule wa Nzega mjini Hussein Bashe akizungumza na Mbunge mteule wa 
jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye pamoja na Jerry Slaa (katikati) kabla 
ya zoezi la upigaji kura kwenye ukumbi wa NEC.
 
 
 
 
 
 






 
 
0 comments:
Post a Comment