Dokta
 Mwele Malecela wa Kituo cha Utafiti wa Madawa (NIMR) Tanzania akifanya 
mahojiano jana na baadhi ya vyombo vya habari vilivyoshiriki katika 
warsha ya siku mbili inayofanyika mkoani Arusha kujadili njia bora za 
kupambana na magonjwa ya mlipuko kwa binadamu na wanyama ukiwemo ugonjwa
 wa Ebola na mengineyo katika bara la Afrika na kwingineko 
duniani.Warsha hiyoimeandaliwa kwa pamoja na taasisi za afya za SACIDS 
na EAIDSNet na kufadhiliwa na taasisi ya afya ya CORDS ya nchini 
Ufaransa.
Wadau
 mbalimbali wa Sekta ya Afya kutoka katika mashirika na taasisi 
mbalimbali za barani Afrika na Ulaya wakiwa katika picha ya pamoja 
walipokutana katika warsha ya siku mbili inayofanyika mkoani Arusha 
kujadili njia bora za kupambana na magonjwa ya mlipuko kwa binadamu na 
wanyama kama Ebola na mengineyo katika bara la Afrika na kwingineko 
duniani. Warsha hiyo imeandaliwa kwa pamoja na taasisi za afya za SACIDS
 na EAIDSNet na kufadhiliwa na taasisi ya afya ya CORDS ya nchini 
Ufaransa.
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment