Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile na Balozi wa Japani
nchini Bw. Masaharu Yoshida wakibadilishana hati ya mkataba wa mkopo wa
Shilingi Bilioni 210 kwa ajili ya mradi wa Umeme kati ya Tanzania na
Kenya.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile na Balozi wa Japani nchini
Bw.Masaharu Yoshida wakisaini mkataba wa mkopo. Nyuma yao kushoto ni
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Omar Chambo, kulia ni
Waziri wa Mambo ya Nje wa Japani Seiji Kihara wakishuhudia tukio hilo
katika ukumbi wa Wizara ya Fedha Jijini Dares Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile akitoa ufafanuzi wa
matumizi ya mkopo wa bilioni 210 baada ya kusaini mkataba wa mkopo huo
katika ukumbi wa Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam.
SERIKALI
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini mkataba na Serikali ya
Japani kiasi cha shilingi Bilioni 210 kwa ajili ya maendeleo ya mradi wa
njia ya kusafirishia umeme kati ya Tanzania na Kenya ambao utasaidia
upatikanaji wa umeme wa kutosha.
Mkataba
huo wa masharti nafuu ulisaininiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile na Balozi
wa Japani nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya kusaini mkataba huo Dkt. Likwelile
alisema kuwa fedha hizo zitaelekezwa katika kusambaza nyaya za umeme
zenye KV400, na urefu wa kilometa 414.5 kati ya Singida na Namanga
kupitia Babati na Arusha.
Alisema
kuwa kukamilika kwa mradi huo kutachochea maendeleo ya jamii na uchumi
nchini kwa kuleta muungano wa kibiashara katika nchi za Afrika
Mashariki.
Naye
Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida alisema kuwa mkopo
huo utafanikisha kusambaza nyanya za umeme zenye urefu wa takribani
kilometa 508 kati ya Tanzania na Kenya ambapo Tanzania itasambaza
kilometa 415 wakati Kenya itakuwa na kilometa 93.
Japani
imekuwa ikisaidia Tanzania katika miradi ya umeme kwa muda mrefu,
miradi ambayo tayari imekamilika ni pamoja na usambazaji umeme Zanzibar,
mradi wa usambazaji nyaya za umeme mkoani Kilimanjaro na mradi wa
kutengeneza nyaya mpya za umeme jijini Dar es Saalam.
0 comments:
Post a Comment