Afisa Mkuu
wa Fedha wa Benki ya Exim Tanzania, Bw. Selemani Ponda, (wa pili kulia)
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusiana na uzinduzi wa kituo kipya cha huduma
kwa wateja wa benki hiyo kwa njia ya mawasiliano ya simu ikiwa ni sehemu
ya mkakati wa benki hiyo kuboresha huduma zake kupitia teknolojia ya
mawasiliano. Pembeni yake ni Mkuu wa Hazina wa Benki hiyo, Bw George Shumbusho (wa pili
kushoto), Afisa masoko wa benki hiyo, Bw Abdulrahman
Nkondo (kushoto) na Meneja Mwandamizi Huduma kwa wateja Bw. Frank Matoro.
BENKI
ya Exim Tanzania imezindua kituo chake kipya cha huduma
kwa wateja kwa njia ya mawasiliano ya simu ikiwa ni sehemu ya mkakati wa
benki hiyo kuboresha huduma zake kupitia benki hiyo teknolojia ya mawasiliano.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,
Meneja Mwandamizi Huduma kwa wateja wa Benki hiyo Bw. Frank
Matoro alisema
pamoja na kusogeza upatikanaji wa huduma kwa wateja wa benki hiyo, vituo hivyo
pia vitasaidia kuboresha mahusiano na wateja wa benki hiyo.
“Ni
matarajio yetu kwamba wateja wetu watafurahia zaidi huduma bora kutoka kwa wahudumu
wenye vigezo na uelewa wa kutosha kuhusiana na masuala ya kibenki kila siku za
Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 1:00 jioni na siku za
Jumamosi kuanzia saa 2:30 asubuhi hadi saa 7:00 mchana kupitia namba yetu ya
0784 107600,’’ alisema
Kwa
mujibu wa Bw Matoro kituo hicho kinatarajiwa kuleta mabadiliko kwenye biashara
kupitia huduma za kibenki huku akiongeza: “Ni adhma yetu kuhakikisha kwamba
tunapambana siku zote ili tu hali ya kiuchumi kwa wateja wetu iendelee kuwa
bora na ni hicho tu ndio kimekuwa kikitusaidia
kuwa na matokeo mazuri,’’.
Alibainisha
kuwa huduma hiyo ilibuniwa mahususi ili kuleta tija kwa wateja wa benki hiyo
kwa kuwa inaenda sambamba na mahitaji yao, mfumo wao wa maisha pamoja na hadhi
yao hatua aliyoilezea kuwa itaiongezea benki hiyo uaminifu miongoni mwa wateja
wake.
“Pia
tunatarajia kwamba huduma hii itatuongezea ukubwa wa soko kwa kuwa itapanua
wigo wa kuwafikia wateja, kujiongezea ukuaji wa fursa sambamba na kutoa fursa kwa wateja wetu
waweze kutupa mrejesho wa huduma mbalimbali tunazowapatia,’’ alisema.
Akizungumzia
hati fungani za benki ya hiyo zinazouzwa katika soko la hisa la Dar es
Salaam DSE, Mkuu wa Hazina wa benki hiyo Bw. George Shumbusho alisema
idadi kubwa ya watu wameendelea kujitokeza kununua hati hizo huku
akibainisha kuwa hati hizo zilizoanzwa kuuzwa tarehe 23 Novemba, 2015 huku zikitarajia kufungwa tarehe 18 Disemba mwaka huu zinalenga kukusanya takribani bilioni 15.
0 comments:
Post a Comment