(Picha zote na Benedict Liwenga)
Na Shamimu Nyaki.
Serikali kupitia Mpango wa wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yasiyopewa
kipaumbele leo imetangaza tarehe 19
hadi 23 mwezi huu kuwa itaanza zoezi la kugawa dawa kwa makundi yanayopaswa
kupata dawa za magojwa hayo.
Tamko hilo limetolewa
na Katibu mkuu wa Wizara Ya Afya na Ustawi wa Jamii,Wazee,na Watoto Bw. Donald Mmbando
alipokuwa anazungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake jijini Dar es
Salaam na kusema kuwa Magonjwa ambayo hayapewi
kipaumbele ni Usubi,Vikope (Trakoma), Matende,
Mabusha,Ngiri maji, na Minyoo ya tumbo hivyo dawa hizo zitasaidia kupunguza tatizo.
Ameongeza kuwa zoezi hilo la ugawaji
wa dawa litatekelezwa katika vituo vyote vya Afya, Zahanati,Hospitali, shule za
msingi na sekondari,sokoni,vituo vya usafiri,pamoja na Ofisi za Serikali na
Mashirika ya Umma na hivyo wananchi wanaombwa kujitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo ambayo haina malipo
yoyote.
Katibu Mkuu huyo amesema
kuwa wahusika wakuu katika kupatiwa dawa hizo ni Watu wote kuanzia miaka
mitano na kuendelea,isipokuwa watoto chini ya miaka mitano,wajawazito, mama anaenyonyesha mtoto chini ya siku saba na
Wagonjwa Mahututi.
“Tunataka kulinda afya zao na Uhai
wao hivyo tunaomba wafuate maelekezo vizuri”.Alisema Bw Mmbando.
Aidha zoezi hilo litatekelezwa katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Singida,
Dodoma,Mtwara, Lindi na Pwani kwa ajili ya kujikinga na kutibu
magonjwa hayo na Mikoa mingine iliyobaki
itafanya zoezi hilo katika ngazi ya
jamii na shuleni mwishoni mwa mwezi Januari kuendelea hadi Februari
2016.
Naye Mratibu wa Mpango huo Dkt
Edward kirumbi ameeleza kuwa takwimu zainaonyesha kuwa magonjwa
yasiyopewa kipaumbele hapa nchini ni kubwa ambapo ugonjwa wa Usubi umeenea
zaidi katika mikoa sita ikiongozwa na Dodoma, Ugonjwa wa Minyoo ya tumbo
wagonjwa million 13, kichocho ,Matende na Mabusha tathmini za awali zinaonyesha
mikoa 18 imeathirika kwa kuwa na
wagonjwa million 12.
Vile vile Dkt
Kirumbi ameeleza kuwa Magonjwa haya yamekuwa na athari kubwa hasa kwa
kuathiri nguvu kazi ya Taifa hivyo wananchi wanapaswa kupata dawa hizo ambazo
zitakuwa zinatelewa kwa mwaka mara moja ili kukinga upungufu wa Damu, kuuwa vimelea
vya ugonjwa huo, kupungua kwa magonjwa ya ngozi, na kuongeza virutubisho bora
mwilini.
Hata hivyo jamii inapaswa kupewa
elimu zaidi kuhusu Magonjwa haya kwa vile bado haijaelewa athari za magonjwa
haya kwa kiasi kikubwa hasa kwa maeneo
ya vijijini ambayo ndio waathirika wakubwa.
0 comments:
Post a Comment