Mkalimani wa lugha ya alama
akifafanua mazungumzo kwa alama kwa baadhi ya wajumbe wa Shirikisho la
Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) wakati wa mkutano wa
shirikisho hilo na Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Dk. Abdalla Possi
(hayupo pichani), jana jioni (Jumatano, Desemba 16, 2015), katika ukumbi
wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera,Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi
Jenista Mhagama (Mb), (katikati) akimsikiliza Mwenyekiti wa Shirikisho
la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Amon Mpanju
wakati shirikisho hilo lilipo kutana na Naibu Waziri (Watu wenye
Ulemavu) Dk. Abdalla Possi (wa kwanza kushoto), jana jioni (Jumatano,
Desemba 16, 2015), katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu,
Jijini Dar es Salaam, (wa tatu kulia), Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu, Bibi. Regina Kikuli.
Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu)
Dk. Abdalla Possi, akiteta jambo na mmoja wa wajumbe wa Shirikisho la
Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) mara baada ya
kukutana na wajumbe wa shirikisho hilo jana jioni (Jumatano, Desemba
16, 2015), katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar
es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Shirikisho la
Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) wakifuatilia
mazungumzo ya mkutano huo, wakati wa mkutano wa shirikisho hilo na
Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Dk. Abdalla Possi, jana jioni
(Jumatano, Desemba 16, 2015), katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya
Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………………………………….
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia,
(Sera,Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi
Jenista Mhagama (Mb), amelitaka Shirikisho la Vyama vya Watu wenye
Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) kuondoa tofauti zao ili kuweza
kushirikiana na serikali ya awamu ya tano ambayo imedhamiria kuimarisha
na kulinda haki za watu wenye ulemavu.
“Mnapaswa kuhakikisha kuwa wale wote wanaoleta tofauti zenu
kuwashughulikieni mapema katika vikao vyenu ili muweze kushirikiana na
sisi katika kuhakikisha mnapata haki ya kulindwa , kuheshimiwa na
usalama. Tunataka nchi yetu baada ya miaka mitano iwe katika historia
nzuri kwa kuwajali watu wenye ulemavu”. Amesema.
Ametoa wito huo wakati akizungumza na Shirikisho la Vyama vya
Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) jana jioni (Jumatano, Desemba
16, 2015), katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar
es Salaam.
Bibi Mhagama alisema: “Tunapaswa tusimuangushe Rais Magufuli kwa
imani aliyoionesha kwenu na kuteua Naibu waziri anayeshughulikia
masuala yanayowahusu ambayo yanaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu,”
alisema.Awali akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa shirikisho
hilo, Amon Mpanju pamoja na kumshukuru Waziri na Naibu Waziri
anayeshughulikia (Watu wenye ulemavu) kwa kuitisha mkutano uliolenga
kujadili vipaumbele vya watu wenye ulemavu nchini pamoja na nchi
zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi alimuomba waziri huyo kuhairisha
ili waweze kukamilisha uaiinishaji changamoto zao vizuri.
“Tunaomba mheshimiwa waziri utupatie muda zaidi tuweze ili
tuweze kuainisha vizuri zaidi changamoto zetu ambazo naamini Naibu
waziri mwenye dhamana ya kushughulikia watu wenye ulemavu amabye pia
tunaimani naye sana ataweza kubaini masuala yanayotuhusu na kuweza
kuyatekeleza katika majukumu yake” alisema.
Mkutano huo uliandaliwa na Naibu Waziri anayeshughulikia watu
wenye Ulemavu Dk. Abdalla Possi, pia ulihudhuliwa na Katibu Mkuu Ofisi
ya Waziri Mkuu aliye wakilishwa na Naibu wake, Bibi. Regina Kikuli na
Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri
Mkuu, Obey Assery.
0 comments:
Post a Comment