Pages

Ads 468x60px

Thursday, December 17, 2015

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu azindua Bodi Mpya ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.




Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road, Bwana Diwan Msemo (kushoto) akimuonyesha Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) jengo linalojengwa katika Hospitali hiyo ambalo litatumika kuweka mashine zitumikazo kufanyia mionzi kwa jili ya wagonjwa wa saratani hospitalini hapo.
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road iliyopo jijini Dar es Salaam, Bwana Diwan Msemo (kulia) akimueleza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) baadhi ya majukumu wayafanyayo katika Hospitali hiyo alipowasili kufanya Uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Saratani ya Hospitalini hapo, ikiwemo kuangalia vitendea kazi na kero wazipatazo wagonjwa wenye matatizo ya saratani katika hiyo mapema 17 Desemba, 2015.
Mama wa mgonjwa (kulia) akimueleza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) juu ya changamoto za gharama za kupata matibabu wazipatazo wakati Waziri huyo alipofanya ziara katika Hospitali ya Saratani ya Ocean Road iliyolenga kufanya Uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Saratani ya Hospitalini hapo, ikiwemo kuangalia vitendea kazi na kero wazipatazo wagonjwa wenye matatizo ya saratani katika hiyo mapema 17 Desemba, 2015.
Muuguzi wa wagonjwa (kushoto) akimueleza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) juu ya changamoto za dripu wazipatazo wakati Waziri huyo alipofanya ziara katika Hospitali ya Saratani ya Ocean Road iliyolenga kufanya Uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Saratani ya Hospitalini hapo, ikiwemo kuangalia vitendea kazi na kero wazipatazo wagonjwa wenye matatizo ya saratani katika hiyo mapema 17 Desemba, 2015.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) akimjulia hali mama mgonjwa wakati alipowasili katika Hospitali ya Saratani ya Ocean Road iliyopo Dar es Salaam kufanya Uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Saratani ya Hospitalini hapo, ikiwemo kuangalia vitendea kazi na kero wazipatazo wagonjwa wenye matatizo ya saratani katika hiyo mapema 17 Desemba, 2015.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akitoa hotuba fupi wakati aliwaposili katika Hospitali ya Saratani ya Ocean Road iliyopo Dar es Salaam kufanya Uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Saratani ya Hospitalini hapo, ikiwemo kuangalia vitendea kazi na kero wazipatazo wagonjwa wenye matatizo ya saratani katika hiyo mapema 17 Desemba, 2015.


Baadhi ya Wajumbe waliohudhuria katika Mkutano wa Uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Saratani ya Hospitalini Saratani ya Ocean Road iliyopo jijini Dar es Salaam uliofanyika 17 Desemba, 2015 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (hayupo pichani).
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Bodi ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar es Salaam 17 Desemba, 2015. (Picha zote na Benedict Liwenga)


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) akipokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road, Bwana Diwan Msemo (kushoto) mara alipowasili katika Hospitali ya Saratani ya Ocean Road ya Jijini Dar es Salaam kwenye Uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road uliofanyika leo 17 Desemba, 2015.
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road, Bwana Diwan Msemo (aliyevaa suti) akimpeleka Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) katika chumba ambacho ukarabati wa mashine za matibabu zilizopata hitilafu ukiendelea katika Hospitali hiyo mara alipowasili hospitalini hapo mapema 17 Desemba, 2015.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kulia) akipatiwa maelezo toka kwa Mganga wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road juu ya matatizo ya kiufundi ilizozikumba mashine za matibabu hospitalini hapo wakati wa ziara yake ya Uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Saratani ya ya hospitalini hapo uliofanyika leo 17 Desemba, 2015. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road, Bwana Diwan Msemo
Baadhi ya Mafundi wakionekana kutengeneza mashine iliyopata matatizo wakati wa ziara ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu hospitalini hapo iliyolenga kufanya Uzinduzi ikiwemo kuangalia vitendea kazi na kero wazipatazo wagonjwa wenye matatizo ya saratani katika Hospitali ya Saratani ya Ocean Road.
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road, Bwana Diwan Msemo (kulia) akimpeleka Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) kuangalia jengo ambalo litatumika kwa ajili ya mashine maalum za kufanyia huduma za mionzi kwa wagonjwa wa saratani katika Hospitali hiyo.


Na Shamimu Nyaki.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee Na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo amezindua Bodi Mpya ya Wadhamini ya Taasisi ya Saratani katika Hospitali ya Ocean Road Ambayo itasimamia programu za elimu ya afya kuhusu Saratani.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Ummy Mwalimu mbali na kutoa pongezi za uundwaji wa Bodi hiyo amewataka watendaji kuhakikisha wagonjwa wa Saratani wanapata huduma bora, ushauri wa namna ya kuzuia magonjwa ya Saratani, kufanya utafiti wa magonjwa ya Saratani kwa kushirikiana na wadau wengine wa ndani na Nje kwa kuwa Taasisi hiyo imeanzishwa ili kuwasaidia wagonjwa hao.

“Tumieni uzoefu wenu,vipaji vyenu, na taaluma zenu katika kutoa huduma kwa kuwa Taasisi hii inategemewa na watu wote”Alisema Mhe.Waziri.

Aidha Waziri huyo amewahakikishia watandaji wa Bodi hiyo kwamba atashirikiana nao kwa karibu zaidi katika kufanikisha ugojwa wa Saratani unatokomea au kupungua kwa vile Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) inaonyesha kuwa Tanzania ina jumla ya wagonjwa 33,884 lakini wanaopata huduma ni Wagojwa 3000 ambao ni sawa na asilimia 16 tu.

Mhe Ummy amesema atahakikisha Taasisi hiyo inatengewa fedha za kutosha ili iweze kutoa huduma na kupunguza tatizo la ugonjwa wa Saratani hapa nchini kwa kufanya tafiti muhimu Ktika maeneo tofauti na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu ugojwa huo kwa vile wananchi wengi wanagundua ugonjwa huo ukiwa tayari umeshakuwa na athari kubwa.

Katika Hatua nyingine Mhe. Waziri Ummy amesikitishwa na kitendo cha Hospitali hiyo kukosa Dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa saratani kama vile damu,dripu ambapo wagonjwa hulazimika kutafuta huduma nje ya Hospitali hiyo tena kwa gharama kubwa ya Shilingi 800,000 wakati Sera ya Afya yaTaifa inasema huduma kwa wagonjwa wa Saratani hutolewa bure.

Kutokana na Ukosefu wa dawa hizo Waziri Ummy ameitaka Bohari kuu ya dawa (MSD) kuandaa maelezo kuhusu ukosefu wa Dawa za Saratani katika hospitali na waharakishe wanatafuta njia ya kupatikana kwa dawa hizo haraka ili wagonjwa Wapate huduma na kuwaagiza watendaji kuwashawishi wagonjwa na wananchi kwa ujumla kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) ambao utawasaidia katika matibabu.

Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo ya Ocean Road Bw Hamisi Diyenga alitoa ufafanuzi kuhusu ukosefu wa dawa za kupunguza Makali ya ugonjwa wa Saratani kwamba umetokana na uhaba wa Bajeti,ukosefu wa Mashine za kutosha kwa ajii ya matibabu ya mionzi kwa wagonjwa kwakuwa silimia 90 ya wagonjwa wa Saratani wanatibiwa kwa mionzi.

Kaimu Mkurugenzi huyo amemueleza Waziri huyo wa Afya jitihada wanazozifanya kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wagonjwa kwamba wametenga shilingi Bilion 15 kwa ajili ya kununua mashine za kutoa huduma ya mionzi pamoja na kukarabati mashine ambazo zimeharibika.

“Huduma ya mionzi kwa wagonjwa wa Saratani ni muhimu sana katika kumpa nafuu hivyo tunalazimika kutoa kwa wale wanaohitaji huduma za dharura tuu” Alisema Mkurugenzi huyo.

Katika ziara hiyo Mhe. Waziri aliwatembelea wagojwa waliolazwa,akakagua Mashine za mionzi pamoja na jengo linalojengwa kwa ajili ya kutoa huduma ya mionzi kwa wagonjwa wa Saratani ambapo huduma hiyo inapatikana hospitali ya Ocean Road pekee.

0 comments:

Post a Comment

 
Blogger Templates