Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa
Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma akitoa
maelezo ya namna wanavyoendesha shughuli zao kwa Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla
aliyefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo, Januari 4, 2016.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza
watanzania wote wasikubali kutozwa rushwa kwa ajili ya damu salama na
baadala yake kwa mtu atakayefanya hivyo watamchukulia hatua kali.
Kauli hiyo imetolewa mapema Januari 4
(jana) na Naibu huyo wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Dkt. Kingwangalla alipofanya ziara katika Ofisi za
Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dares Salaam.
Dk. Kigwangalla amefafanua kuwa, kwa watu
wote ikiwemo Nesi, Daktari ama mtaalamu wa afya, atakayemtoza mtu damu,
atachukuliwa hatua kali ikiwemo kufukuzwa kazi.
“Kwa watanzania wote, msikubali kutoa
rushwa kwa ajili ya damu. Na kama itatokea Nesi ama Daktari ama nani,
anakuambia ulipie ili upate damu!. Kwa sababu kuna uhaba wa damu kwa
sasa.. Ripoti kwa Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa ama Daktari Mkuu husika
ama fika Wizara ya afya moja kwa moja na kuna namba tutaitoa kwa
watanzania wote mtupatie ripoti.
Mtu atakayekutoza damu, wewe tuambie,
huyo tutamfukuza kazi moja kwa moja, hatuwezi kuendekeza watu wa namna
hii... Serikali inaingia gharama kubwa kukusanya damu kwa watu, Kuna
watu wanajitolea damu zao bure. Leo wewe nesi ama mganga ukauze damu,
hilo jambo hatutakubali hata kidogo kwa hiyo natoa rai kwa watanzaia
hiyo damu ni bure na haiuzwi na usikubali kuuziwa damu hata kidogo.”
Ameeleza hilo Dk. Kigwangalla.
Awali katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla
ameipongeza Ofisi ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama kwa kazi
wanayofanya na ubunifu waliofikia wa kuhusisha Halmshauri katika
ukusanyaji wa damu huku wao wakisimamia kudhibiti viwango vya damu ya
matumizi kwa watanzania huku akitumia wasaha huo kutoa maelekezo ya
kuboresha mfumo wa motisha kwa wanaochangia damu salama ambapo kwa
wachangiaji damu kuingizwa kwenye mfumo wa kieletroniki wa kuwatambua
watu wanaochangia damu, kutoa taarifa jinsi damu zao zilivyookoa miasha
ya wagonjwa na kuwapa motisha ili waweze kuwa wachangiaji endelevu.
“Motisha sio soda na maji kwa
wanaochangia damu. Motisha ni hata kupewa taarifa kwamba damu yake
imesaidia kuokoa maisha ya mwanadamu mwenzake aliyekuwa anaumwa ugonjwa
fulani, hii ni motisha kubwa sana kuliko hata pesa, ama soda ama maji
yanayotolewa anapochangia damu..
Lakini kama imeshajitokeza mtu kuwa na
tabia ya kuchangia damu, huyu sio wa kumpoteza, maana yake kuna
uwezekano mkubwa wa akarudi tena kuchangia damu, mtu huyu ni lazima kuwe
na mfumo wa kielekrioniki wa komputa wa kumtakia salamu, taarifa na
anakuwa kwenye database yenu.
“Mnatakiwa muwe na mfumo wa kumpa
taarifa pindi damu yake imetumika, ikiwemo kumueleza kuwa damu yako
imemsaidia Mama mjamzito aliyejifungua na kutokwa damu nyingi, na mtu
huyo akipata taarifa hiyo ni motisha tosha hivyo ni lazima muwe na huo
mfumo kutoa motisha zaidi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla na msafara wake
wakishuka ngazi kuelekea kukagua idara mbalimbali katika ofisi hizo,
Januari 4, 2016
Awali akielezwa na Meneja wa kanda ya
Mashariki katika Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini
Dar es Salaam, Eveline Mgassa kwamba changamoto zilizopo katika
upatikanaji wa damu nchini ni halimshauri kutenga bajeti za kutosha kwa
ajili ya huduma hiyo, Kwa hatua hiyo, Dk. Kigwangalla ameziagiza
Halmshauri zote nchini kuhakikisha zinatenga bajeti za kutosha
ilikusapoti mpango wa damu salama.
Katika hilo Dk. Kigwangalla ameapa
kuwashughulikia wale wote watakaozembea na kuwachukulia hatua kali Ma
DMO, Wakurugenzi na kushtakiwa kwa mamlaka zilizopo na kufukuzwa kazi.
“Naziagiza Halmashauri zote kuhakikisha
zinatenga bajeti za kusapoti mpango wa ukusanyaji damu salama. Na
Halmashauri zitakazoshindwa, DMO na Mkurugenzi wake tutahakikisha
tunawashtaki kwa mamlaka zilizowateua ili uteuzi wao ukome mara moja.
Maana hatuwezi kuacha akinamama wajawazito wapoteze damu wakati wa
kujifungua, watu wanaopata ajali wapoteze maisha kwa sababu ya watu
hawataki kutimiza wajibu wao.
Hilo haliwezi kukubalika, Mfumo wa hali
ya damu kwa Tanzania kwa sasa unatisha. Kwa sasa nchi inakiwango cha
chini mno, tokea wafadhili wajiondoe katika hili. Ni lazima tuwe makini
sana maana leo mzima kesho umepata ajali, umepasuka mfupa wa kwenye paja
damu nyingi zimemwagika unahitaji damu!!
Kwa upande wa watu wote wanaopata damu
salama nchini, huduma hiyo wanazipata bure kwani damu hizo ni za
Serikali, Hata hivyo mifuko na vitu vinavyotumika kuhifadhia damu hiyo
vina gharama kubwa.
“Damu inatolewa bure na serikali. Mtambue
kuwa, vifaa vya kutunzia damu hii ni gharama kubwa. Hivyo mifuko
mashirika ya Bima, na mashirika mengine kuanzia leo kutazama namna ya
kulipa gharama za vifaa vya utunziaji damu hizo. Damu ni bure, lakini
mfuko ule wa kutunzia ile damu ni gharama kubwa sana na hata vifaa vya
kupimia damu ile nayo ni gharama kubwa hivyo walipie kwa kila damu
watakayochukua.” Alieleza Dk. Kigwangalla.
Meneja wa kanda ya Mashariki Ofisi za
Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Eveline
Mgassa (mwenye miwani) akielezea utaratibu wa ukusanyaji wa damu
unavyofanyika kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla aliyefanya ziara ya kushtukiza
katika ofisi hizo, Januari 4, 2016 jijini Dar.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla (aliyeipa
mgongo kamera) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Uendeshaji wa Ofisi
za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Bw.
Abdu Juma ya namna wanavyopokea watu wanaofikia kuchangia damu kwa hiari
na kuhifadhiwa kwenye benki hiyo yaTaifa ya Damu Salama, alipofanya
ziara ya kushtukiza, Januari 4, 2016 katika ofisi hizo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akitoa mkono wa
pongezi kwa wananchi walioonyesha uzalendo kwa kufika katika ofisi za
Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Januari 4, 2016 na kuchangia damu kwa
hiari yao ambapo mmoja kati yao alisema hii ni mara yake ya nne na ni
utararibu aliojiwekea.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akisalimiana na
kumpongeza mmoja wa wananchi (jina lake halikuweza kupatikana) aliyefika
kuchangia damu kwa hiari, Januari 4, 2016 katika makao makuu ya ofisi
za Mpango wa Taifa wa Damu Salama.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akiwa ndani ya
maabara ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama alipofanya ziara ya kushtukiza
kwenye ofisi hizo, Januari 4, 2015 jijini Dar es Salaam.
Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa
Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma
akimwonyesha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla moja ya damu ambayo ni maalum kwa wamama
wajawazito wakati wa kujifungua zilizohifadhiwa kwenye jokofu katika
mabara hiyo.
Mmoja wa watumishi katika maabara ya
ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama (ambaye jina lake halipatikana)
akiendelea kutekeleza majukumu yake kama alivyokutwa na mpiga picha
wetu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akisaini vitabu
vya wageni nje ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo
jijini Dar es Salaam, Januari 4, 2016 wakati alipofanya ziara ya
kushtukiza katika ofisi hizo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akizungumza na
waandishi wa habari baada ya kufanya ziara ya kushtukiza na kuzungikia
vitengo mbalimbali katika ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama jijini
Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment