Mkurugenzi Msaidizi wa usimamizi na udhibiti wa uendelezaji miji Wizara ya Ardhi na maendeleo ya Makazi, George Pangawe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Zoezi la bomoa bomoa linaliendelea katika kingo za mto Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi
 Msaidizi wa usimamizi na udhibiti wa uendelezaji miji Wizara ya Ardhi 
na maendeleo ya Makazi, George Pangawe jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.
Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
SERIKALI
 yawaomba wananchi waliojenga makazi kwenye sehemu hatarishi, kingo za 
mito na maeneo ya wazi kuhama kwa hiyari yao ili kupisha Oparesheni ya 
bomoa bomoa kuendelea bila kikwazo.
Hayo 
yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa usimamizi na udhibiti wa uendelezaji
 miji Wizara ya Ardhi na maendeleo ya Makazi, George Pangawe wakati 
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Pangawe
 amesema kuwa Serikali itahakikisha haki inatendeka kwa wananchi wote 
pia itahakikisha haki na usawa wa pande zote wakati wa utekelezaji wa 
zoezi la bomoabomoa linaloendelea tangu lilipoaza tena Januari 5 mwaka 
huu.
Zoezi 
la bomoabomoa linaendelea jijini Dar es Salaam katika kingo za mto 
Msimbazi ili kuepusha wananchi kupatwa na madhara mbalimbali ambayo huwa
 yanakitokeza wakati wa mvua kubwa na masika.
Pangawe
 pia amesema kuwa bonde la mto msimbazi liliainishwa kama ni sehemu 
hatarishi kwa makazi ya binadamu tangu 1979 na wananchi wa maeneo ya mto
 huo wakaanza kuvamia kutokana uhaba wa maeneo ya makazi na kuanza 
kujenga katika kingo za mto huo.
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment