Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
wa Benki ya DCB, Balozi Paul Rupia akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck
Sadiki sehemu ya katoni 58 za dawa za maji (Water Guard) kuajili ya kupambana
na ugonjwa wa Kipindupindu leo katika katika a Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es
Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
SaidMeck Sadiki akizungumza na watendaji wa Manispaa ya Kinondoni (hawapo
pichani) juu ya kusimamia usafi wakati makadhibiano ya dawa za maji katoni 58
ilifanyika leo Katika viwanja vya Manispaa hiyo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
wa Benki ya DCB, Balozi Paul Rupia akimukabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck
Sadiki sehemu ya katoni 58 za dawa za maji (Water Guard) kuajili ya kupambana
na ugonjwa wa Kipindupindu leo katika katika a Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es
Salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki amewataka watendaji
wa Manispaa ya Kinondoni kusimamia kikamilifu usafi katika kupambana na ugonjwa
wa kipindupindu.
Meck Sadiki ameyasema hayo wakati akikabidhiwa dawa za maji katoni 58
zenye thamani ya Sh. Milioni Tano (5) zilizotolewa na Baenki ya DCB ,amesema
umefika wakati wa kutofumbia macho watu ambao hawatimizi wajibu wao katika
suala la kufanya usafi.
Amesema watendaji wote ni lazima
wawajibike katika kusimamia suala la usafi kwani kinondoni ndio ilikuwa ya
kwanza kuwa na mgonjwa wa kipindupindu hivyo ni lazima kuwa ya kwanza ya
kutokuwa na ugonjwa huo katika Manispaa ya Kinondoni.
Aidha amewataka watu kufuata ushauri
wa watendaji katika masualanya afya
kutokana na kuwepo kwa magonjwa ya milipuko nambayo yanatokana na uchafu katika
mitaa mbalimbali katika manispaa hiyo.Meck Sadiki amesema Benki ya DCB
imetoa dawa ya maji kutokana na kutambua watu wanaogua wanamchango katika taifa
pamoja na benki .
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya
DCB, Balozi Paul Rupia amesema kuwa kutoa dawa hizo ni kutokana na kutambua
wanaougua ni watu ambao wanazalisha hivyo wanawajibu kutoa msaada huo kadri ya
uwezo wao.
Rupia amesema benki itaendelea
kushirikiana na serikali katika masuala mbalimbali yanayohusu jamii kuweza
kwenda sambasamba na serikali katika kutatua changamoto kwa namna moja au
nyingine.
0 comments:
Post a Comment