Waziri
 wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye aliyekuwa 
mgeni rasmi akimuwakilisha Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan 
akizindua rasmi albam mbili za kwaya ya Wakorintho wa Pili kwenye 
tamasha la Krismas lililofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee leo, 
ambapo mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini 
Rebecca Malope amefanya onesho kubwa lililovuta hisia za mashabiki wengi
 waliohudhuria katika tamasha hili akishirikiana na waimbaji mbalimbali 
wa hapa nyu mbani na nchi jirani ya Kenya.
Akizungumza
 wakati wa uzinduzi huo Nape Nnauye amewaomba watanzania kuzidi 
kumuombea Rais Dk . John Pombe Magufuli kwa kazi ya kutumbua majipu 
ambayo amekwishaianza kwani kazi hiyo ni ngumu na ina vikwazo vingi, 
lakini pia amewataka watanzania na waumini wa madhehebu mbalimbali 
kuwaombea wasaidizi wake ili waweze kuwa bega kwa bega na Mh. Rais Dk. 
John Pombe Magufuli ili kutekeleza kazi hii kwa ufanisi na kisha 
watanzania wafaidi matunda na rasilimali zao wenyewe.
Waimbaji
 kutoka Kenya walikuwa ni Faustine Munishi na Sara K na Solomon Mukubwa 
kutoka jiji la Nairobi huku waimbaji wa hapa nyumbani wakiwa ni Rose 
Muhandom Upendo Nkone, Christine Shusho, Edson Mwasabwite, Joshua Mlelwa
 na wengine wengi, Tamasha hilo pia lilikuwa na lengo la kumshukuru 
mungu kwa nchi yetu ya Tanzania kufanya uchaguzi kwa amani, Kulia ni 
Akex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ambayo ndiyo 
imeandaa tamasha hilo.(PICHA NA JOHN BUKUKU- FULLSHANGWEBLOG-DAR ES 
SALAAM)
Akex 
Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ambayo ndiyo imeandaa 
tamasha hilo. akimkaribisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na 
Michezo Ndugu Nape Nnauye ili kuzungumza na wananchi katika tamasha hilo
 kushoto ni Mbunge Martha Mlata na MC Mwakipesile mshereheshaji wa 
Tamasha hilo.
Waziri
 wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye akiwahutubia 
wananchi na mashabiki waliohudhuria katika tamasha hilo katikati ni Akex
 Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ambayo ndiyo imeandaa 
tamasha hilo na kushoto ni MC Mwakipesile.
Waziri
 wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye akiimba moja 
ya mapambio na kuitikiwa na mashabiki wa nyimbo za injili waliohudhuria 
katika tamasha hilo.
Waziri
 wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye pamoja na 
maaskofu na viongozi mbalimbali wakishiriki katika sala maalum ya maombi
 iliyofanyika katika tamasha hilo,
Wamumini
 na mashabiki mbalimbali wa muziki wa injili wakishiriki katika maombi 
maalum ya kumshukuru mungu yaliyofanyika kwenye tamasha hilo.
Waziri
 wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs 
Rhobi Nape Nnauye wakicheza pamoja na mwimbaji Upendo Nkone kutoka kulia
 ni Mbunge Martha Mlata na Alex Msama wakishiriki kucheza.
Mwimbaji Rebecca Malope akiimba katika tamasha hilo.
Waimbaji wa mwimbaji Rebecca Malope akiimba katika tamasha hilo.
Mwimbaji Rebecca Malope akiimba kwa hisia huku meza kuu pamoja na mashabiki wake wakiwa wamesimama.
Waziri
 wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs 
Rhobi Nape Nnauye akicheza na mwimbaji Rebecca Malope wakati wa tamasha 
hilo kulia ni mbunge wa viti maalum mkoa wa mbeya Mary Majelwa na kulia 
ni Mbunge Martha Mlata.
Waziri
 wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs 
Rhobi Nape Nnauye pamoja na maaskofu mbalimbali wakiwa wamesimama wakati
 mwimbaji Rebecca Malope akifanya vitu vyake katika tamasha hilo.
Mwimbaji Christine Shusho na Mbunge Martha Mlata wakiimba pamoja wakati wa Tamasha hilo.
Waziri
 wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs 
Rhobi Nape Nnauye,Alex Msama na Mkewe na baadhi ya wabunge kulia ni 
Martha Mlata na kushoto ni Mary Majelwa wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwimbaji Faustine Munishi kutoka nchini Kenya akiiimba katika tamasha hilo.
Wanakwaya wa Wakorintho wa pili wakiimba wimbo wao mara baada ya kuzinduliwa kwa albam zao katika tamasha hilo.
Mwimbaji
 kutoka nchini Kenya Solomon Mukubwa akiimba na mwimbaji mwenzake kutoka
 kushoto Sara K. huku mbunge Martha Mlata akishiriki kuimba nao.
Mwimbaji Joshua Mlelwa naye amefanya mambo makubwa jukwaani katika tamasha hilo.
Mwimbaji Rose Muhando pamoja na waimbaji wake wakifanya vuti vyao jukwaani.
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment