Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akisaini
kitabu cha wageni baada ya kufika katika Tume ya Mipango. Kulia ni Kaimu Katibu
Mtendaji Bi. Florence Mwanri.
Baadhi ya wafanyakazi wa Tume ya Mipango wakimpokea Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipowatembelea kwa lengo la kuwaaga.
Mmoja ya watumishi wa Tume ya Mipango Bw. Mohamed Ally
akiongea mawili matatu na waziri mara baada ya mkutano kuisha.
Baadhi ya wafanyakazi wa Tume ya Mipango wakimpokea Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipowatembelea kwa lengo la kuwaaga.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiongea na
watumishi wa Tume ya Mipango alipowatembelea kwa kusudi la kuwaaga.
Kaimu Katibu Mtendaji Bi. Florence Mwanri akimsikiliza kwa
makini Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.
WAZIRI wa Fedha na Mipango,
Dkt. Philip Mpango ameiagiza Tume ya Mipango kufanya utafiti kuhusu mapato ya
Serikali na namna ya kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato.
Amesema Tume ya Mipango
kama chombo cha ushauri kwa Serikali kuhusu mipango na uchumi wa nchi, ni
lazima ifanye utafiti juu ya ufanisi wa ukusanyaji wa mapato na kuongeza vyanzo
wa kukusanya mapato ya Serikali ili kuiwezesha Serikali kuwahudumia wananchi
wake.
“Serikali isipokusanya kodi
kwa ufanisi haiwezi kuwahudumia wananchi hivyo, ni lazima kodi ikusanywe
ipasavyo ili kuiwezesha kujiendesha” alisema.
Dkt Mpango aliyasema hayo alipokutana
na wafanyakazi wa Tume ya Mipango kwa lengo la kuwaaga baada ya kuteuliwa na
Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli
kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.
Waziri wa Fedha amesema
mianya yote ya ukwepaji kodi ni lazima izibwe ili kuiwezesha Serikali kukusanya
mapato ya kutosha suala ambalo litairahisishia utoaji wa huduma za msingi kwa
wananchi.
Amesema Serikali haiwezi
kutegemea kila kitu kutoka kwa wafadhili wakati nchi ina rasilimali za kutosha hivyo.Dkt. Mpango amesema Tume ya
Mipango ni lazima iongoze nchi kuelekea katika uchumi wa viwanda ambavyo
vitafanya pato la taifa kuongezeka na kutoa ajira kwa wananchi.
“Sisi kama wataalamu
tunatakiwa kuiongoza nchi katika kufikia kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo
mwaka 2025 jambo ambalo linawezekana” alisema.Waziri pia amesema ni
lazima tujenge uchumi imara na madhubuti utakaowezesha kupunguza umaskini
miongoni mwa wananchi.
“Serikali ya Awamu ya Tano
imedhamiria kuboresha ufanisi na utendaji wa Serikali kwa ujumla hivyo ninyi
kama wataalamu mna mchango mkubwa katika kutimiza hilo” alisema.
Tume ya Mipango ni chombo
mahususi cha fikra rejea na ushauri kwa serikali kuhusu sera na mikakati ya
maendeleo, kiuchumi na kijamii ambao unaambatana na ufuatiliaji na utathmini wa
mwenendo wa uchumi nchini.
Aliwataka wafanyakazi wa
Tume ya Mipango kufanyakazi kwa bidii, maarifa na weledi mkubwa ili kuimarisha
utendaji Serikalini.
0 comments:
Post a Comment