Mkemia Mkuu wa Serikali Samuel Manyele leo amekutana
na waandihi wa habari katika ofisi yake, Dar es salaam na kuzungumzia
suala zima la kemikali hatarishi zinazoingia nchini kinyume na sheria
pamoja na mikakati waliyojiwekea.
Sheri za kuingiza kemikali nchini..“Kila
mtu anayetaka kuingiza kemikali nchini lazima apate kibali na
kuhakikisha kwamba ni salama kwa afya za wananchi..tumetayarisha
muongozo kwa watendaji wa bandari ili kushughulikia kemikali hatari na
utasambazwa kwa wadau kabla ya kuanza kutumika”.
“Tumeanzisha bandari kavu kwa ajili ya
kuhifadhi kemikali hatarishi na kusimamiwa kabla ya kuanza safari ya
kwenda kwenye nchi kavu..kuhakikisha viwango vimezingatiwa., utaratibu
huu utarahishisha usimamizi wa kukabiliana na madhara yoyote
yatakayoweza kujitokeza”..Prof. Samuel Manyele
Kiasi cha kemikali zilizoingia nchini tangu Januari hadi oktoba 2015..“Jumla
ya tani zilizoingia kwenye mipaka mbalimbali na bandari jumla ya tani
472,393 za Kemikali ziliingizwa nchini kwa kipindi cha miezi kumi,
bandari ya Dar es salaam ndio inaongoza kwa kuwa na tani nyingi 281,468
ikifuatiwa na Tunduma yenye tani 199, 000, Mtwara, Tanga, Horohoro,
Mwanza na Sirari…tuna list kubwa inayoonyesha ni kiasi gani kemikali
hizo zinapita katika bandari hizo”...Prof. Samuel Manyele
Mpaka wa Tunduma unapitisha Kemikali nyingi kutoka Tanzania kwenda
nchi za nje na ni 80% ya kemikali hupita katika bandari hiyo..
Pia amezungumzia mikakati ya Serikali..”Kuongeza
watumishi kwa wakala ambao wameanza kupelekwa kwenye mipaka inayoingiza
kemikali kwa wingi, kuiwezesha Serikali kufuatilia kemikali hizo kwa
ukaribu, Serikali kufanya maamuzi ya ajira kiasi gani zitolewe na tayari
watumishi wameanza kusambazwa katika mipaka yote inayoingiza Kemikali
hizo”..Prof.Samuel Manyele
Vibali vinatolewaje?..“Kuna kemikali ambazo ni hatari sana kwa binadamu na haziruhusiwi kuingia nchini..”Hutolewa kwa matumizi ya Serikali tu”.
Katika kufanikisha ilo Serikali imeandaa mafunzo ya siku mbili yanayoanza kesho ambayo yatakuwa maalum kwa kutoa elimu ya kemikali hizi na yatashirikisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Afrika Kusini pamoja na Ghana.
0 comments:
Post a Comment