JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
TAARIFA KUHUSU
UGONJWA WA
MNYAUKO FUSARI WA PAMBA NA MBEGU ZISIZOOTA
Serikali
imewataka wachambuaji na wasambazaji wa
mbegu za pamba kuacha kuwasambazia wakulima mbegu zilizozalishwa katika maeneo
yaliyobainika kuwa na ugonjwa wa mnyauko fusari (Fusarium Wilt Disease). Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa
Huduma za Usimamizi, Bodi ya Pamba Tanzania, Bwana James Shimbe.
Katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari, Bwana Shimbe amesema, ugonjwa wa mnyauko fusari
unaweza kudhibitiwa ikiwa wakulima wa pamba watatumia mbegu bora kutoka kwa
wasambazaji wanaotambulika na Bodi ya Pamba Tanzania.
Akizungumzia
tatizo la kuenea kwa ugonjwa huo Bwana Shimbe amesema kwa kiasi fulani limetokana
na baadhi ya wachambuaji wasio waaminifu kuendelea kusambaza mbegu za pamba za
kupanda ambazo zinaweza kuwa zimetoka katika maeneo yaliyobainika kuwa na ugonjwa wa mnyauko fusari.
“Tulishatoa maelekezo kwa kuwataka
wasambazaji wa mbegu za pamba za kupanda kutosambaza mbegu zilizozalishwa
katika maeneo yenye ugonjwa.”
Hivyo
tunaendelea kusisitiza kuwa wakulima wawe makini wanapo nunua mbegu kutoka kwa
wasambazaji wasiotambulika na watoe taarifa haraka kwa Bodi wanapoona mbegu
hizo hazioti ili hatua za haraka zichukuliwe za kupeleka mbegu zingine mbadala
ili kuendana na msimu wa kilimo.
Aidha,
Bwana Shimbe amewataka wachambuaji wa pamba ambao ndio wasambazaji wa mbegu
kuacha mara moja kuwasambazia wakulima mbegu ambazo zimetoka kwenye maeneo
yaliyobainika kuwa na ugonjwa na badala yake mbegu za pamba hizo zisindikwe
kuzalisha mafuta ya kula kama walivyokuwa wameelekezwa na Bodi hapo awali.
0 comments:
Post a Comment