Washiriki
wa warsha hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na mwakilishi wa mgeni
rasmi ambaye ni mshauri wa mradi huo Bw. Ahmed Athumani.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa Soko la Ajira ,Mipango na Maendeleo wa VETA, Ahmed
Athuman akizungumza katika warsha ya wadau wadau wa viwanda,umeme na
magari kujadili utekelezaji wa mradi wa mafunzo yanayotolewa kwa
ushirikiano kati VETA na wadau hao iliyofanyika katika ukumbi wa
Giraffee Hoteli jijini Dar es Salaam.
Sehemu
ya wadau wakifatilia maada mbalimbali katika kujadili utekelezaji wa
mradi wa mafunzo yanayotolewa kwa ushirikiano kati VETA na wadau hao
iliyofanyika katika ukumbi wa Giraffee Hoteli jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii
MAMLAKA
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)imekutana na wadau wa
viwanda,umeme na magari kujadili utekelezaji wa mradi wa mafunzo
yanayotolewa kwa ushirikiano kati yake na viwanda.
Akizungumza
na wadau wa mamlaka hiyo wakati akifungua warsha hiyo Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa Soko la Ajira ,Mipango na Maendeleo wa VETA, Ahmed
Athuman alisema moja ya sababu zinazokwamisha ajira kwa vijana nchini ni
ukosefu wa mafunzo ya vitendo kwa vijana wanaohitimu katika taasisi
mbalilmbali unaosababishwa na kutokukwepo kwa ushirikiano thabiti kati
ya Taasisi za Mafunzo na Viwanda.
Amesema
kuwa VETA inatoa mafunzo yatakayomuwezesha muhitimu kuajiriwa
au kujiajiri kutokana na mafunzo ya vitendo yanayotolewa kutokana na
mahitaji yaliyopo nchini
Ahmed
amesema kuwa ushirikiano wa wadau utaleta matokeo chanya kwa vijana
kuweza kufanya kazi kutokana mafunzo walioyapata katika taasisi za
mafunzo ya ufundi Stadi.
0 comments:
Post a Comment