Chama 
cha Mapinduzi CCM kimekanusha Taarifa iliyozagaa katika Mitandao ya 
Kijamii kwamba Chama hicho kimeridhia aliyekuwa Mgombea wa Urais wa CUF 
Maalim Seif Sharif Hamad akabidhie nchi kuiongoza kwa miaka mitano. 
Akikanusha
 Taarifa hiyo mbele ya Waandishi wa Habari Afisini kwake Kisiwandui 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai amesema taarifa hiyo ni uzushi 
uliotungwa ili kuwatia taharuki WanaCCM na Wananchi kwa Ujumla. 
Amesema
 toka kusambaa kwa Taarifa hiyo Jana amekuwa akipigiwa simu na Watu 
mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kujua ukweli wa Taarifa hiyo hasa 
ikizingatiwa kuwa ilidaiwa kusainiwa na Naibu huyo. “Huu ni Uzushi 
Mkubwa na kwamba unafaa kupuuzwa maana hauna lengo jingine zaidi ya 
kuwagawa WanaCCM” Alismema Vuai. 
Amesema
 kilichopo nikwamba CCM inajiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa Marejeo kama
 ambavyo Tume ya Uchaguzi ilitangaza kuufuta Uchaguzi na hivyo kurudiwa 
upya. Aidha Vuai amesema kuwa tayari wamewasiliana na Wanasheria wao 
pamoja na wataalamu mbalimbali ili kuwabaini waliohusika kusambaza 
Taarifa hizo na kuwapeleka katika Vyombo vya Sheria. 
“Tumeshafanya mawasiliano na Wataalam wetu na tukiwabaini Sheria ya Makosa ya mtandao itachukua nafasi yake” Alisema Vuai. 
Katika
 taarifa hiyo iliyosambaa na kudai kusainiwa na Vuai Ali Vuai ilisema 
kuwa Chama cha mapinduzi kimeridhia na kukubali kumpa nchi Maalim Seif 
Sharif kupitia chama chake cha Cuf kuwa ndio rais wa uchaguzi ulopita,na
 yeye ndio atakayeongoza serikali ya umoja wa kitaifa. 
Taarifa
 hiyo ilieleza kuwa CCM imekubali kushirikiana na maalim Seif katika 
kuongoza nchi chini ya serikali ya umoja wa kitaifa na kukubali kutoa 
makamo wa kwanza wa rais na nusu ya mawaziri. 
Vuai 
amerejea kauli yake kuwa mazungumzo yanayofanywa na Viongozi wa Kitaifa 
kwa kushirikiana na Viongozi Rais Wastaafu wa Zanzibar hayawezi 
kubatilisha maamuzi ya Tume ya kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu 
uliopita. 
 
 
 
 
 
 

 
 
0 comments:
Post a Comment